SoC01 Maendeleo ya Jamii

Stories of Change - 2021 Competition

Kushboy

Member
Joined
Jul 15, 2021
Posts
6
Reaction score
5
MADA: MAENDELEO YA JAMII
Kwanza kabisa tunapozungumzia maendeleo kwa upana wake zaidi ni like kitendo Cha kuinuka au kuhama kutoka hatua moja kwenda hatua inayofuata au kutoka hatua mbovu kwenda hatua Bora zaidi katika nyanja mbalimbali za kimaisha ya kibinafsi au ya kijamii.

Na jamii ni ule mkusanyiko mkubwa au mdogo wa vitu au viumbe vyenye asili moja au tofauti vinavyo ishi kwa kutegemeana na kushirikiana katika masuala mbalimbali ya kimaisha.
Maendeleo ya jamii hujumuisha nyanja mbalimbali kwa sababu jamii yenyewe ni mfumo unaojitegemea kwa maana imejitosheleza kila kitu na hivyo kugawanywa katika nyanja zifuatazo:

1. AFYA
Katika jamii na masuala ya kimaendeleo Jambo la kwanza na la msingi ambapo kila Mara limekuwa likisisitizwa na baadhi ya watu wa rika tofauti tofauti vijana,wazee,wanawake kwa wanaume ni Jambo zima la afya, ikiwa afya itawekwa katika mfumo mzuri kuhakikisha wanajamii husika(watu) wanapata afya na huduma nzuri kiafya ili kutengeneza utendaji kazi wa miili yao vizuri kuweza kuijenga jamii kimaendeleo.

2.MAZINGIRA
Haya ni jumla ya Mambo yote au vitu vyote vinavyomzunguka binadamu katika mzunguko wa maisha yake ya kila siku.Katika suala zima la maendeleo ya jamii hujumuisha pia mazingira kwa kuwa mazingira yanachukua nafasi kubwa Sana katika kuhamasisha maendeleo ya jamii husika,kulinda maliasili,kuboresha vyanzo vya maji,kupanda miti,kuweka na kuhifadhi vidhibiti taka ili kuhakikisha mazingira yanatunzwa vyema na maendeleo yanafikiwa kwa asilimia kubwa.

3. UCHUMI WA JAMII
Uchumi ni mkusanyiko wa rasilimali hai Kama fedha na madini ambazo hutumika Kama nyenzo kubwa na muhimu ya maendeleo ya jamii au taifa lolote like kwa ujumla. Uchumi ndicho kipimo Cha kutambua Kama ni kwa namna au kiwango gani jamii au taifa limeendelea, maendeleo ya jamii kwa kiasi kikubwa hupimwa kwa kutazama mapato na matumizi ya jamii husika, mapato hayo huweza kuwa yametoka moja kwa moja kutoka ngazi ya serikali au yametokana na vyanzo mbalimbali vya mapato hayo Kama vile kodi,ushuru na tozo mbalimbali ndani ya jamii husika kwa wanajamii, hivyo vyote endapo vikatumiwa ipasavyo na wale wenye mamlaka juu ya kuiongoza na kuisimamia jamii kimaendeleo Basi jamii au taifa litaweza kukwea mbele na juu zaidi kiuchumi ambayo itakuwa ni sababu ya maendeleo na mapato zaidi, kwani uchumi imara ni matokeo ya afya Bora na maendeleo yanafikiwa kwa asilimia stahiki.

4: SIASA
Hii ni mojawapo ya sekta kubwa pia yenye hadhi sawa na hadhi ya jamii na uchumi,siasa ndiyo msingi mkubwa wa tatu Baada ya afya na uchumi kwa sababu siasa imebebwa na jamii yenyewe na wanasiasa ndiyo walioibeba jamii kimaendeleo kwa mfano mwenyekiti, diwani na Wabunge ndiyo wenye dhamana kubwa ya kuhakikisha wanajamii wananufaika na mchango wa viongozi hao wa kisiasa kuchochea maendeleo yao Kama jamii, hivyo basi siasa inatakiwa kulindwa na kuhifadhiwa ili kuhakikisha lengo linafikiwa ipasavyo.

5: UTAMADUNI
Utamaduni ni jumla ya Mambo yote yanayomuhusu na anayoyaishi mwanadamu katika maisha yake ya kila siku. Utamaduni hutofautiana Naina ya jamii na jamii au baina ya watu ndani ya jamii husika kwani tamaduni hutambulika kutokana na uwepo wa watu wa makabila mbalimbali ndani ya jamii hiyo, tamaduni hizo ni kakika Mambo yote ya kimaendeleo kwani kutumika vizuri kwa tamaduni hizo ndiyo chachu ya maendeleo ya jamii.

5: UHUSIANO WA KIJINSIA
Panapo maendeleo basi tambua yanafanywa na watu na Wala siyo wanyama wengine tofauti na binadamu, Jambo zima la jinsia ni uhusiano uliopo baina ya pande zote mbili, wanaume na wanawake kwa ujumla wao wakishirikiana ipasavyo katika nyanja mbalimbali za kimaisha ndani ya jamii husika wataweza kujenga msingi mkubwa Sana wa kimaendeleo kijamii kwa mfano, sekta ya uchumi hasa biashara na kilimo kwa asilimia kubwa Kama 65% huchangiwa na akina mama kwani jamii nyingi za kiafrika maendeleo yake yameshikiriwa na akina mama, kutokuwa na itikadi za kibaguzi ndani ya jamii hasa kijinsia hii imesaidia jamii nyingi Sana kuendelea hasa kiuchumi na kimazingira pia.

HITIMISHO:
Maendeleo ili yawe mazuri na yenye tija kwa jamii husika Basi hakuna budi vijana Kama nguvu kazi ya taifa Kusimama mbele Kama viongozi kuhakikisha wanajamii wengine wakiwamo watoto,wazee na vikongwe wanaishi kwa amani,utulivu huku wakipata huduma Bora zaidi kiafya,kiuchumi,kisiasa na kiutamaduni. Nikinukuu kauli mbiu ya aliyekuwa Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania DK.John Joseph Magufuli, alipendelea Sana anapotoa tamko au hotuba za maendeleo kutumia msemo wa "HAPA KAZI TU" akimaanisha vijana tunayo dhima kubwa kuibeba Tanzania yetu kimaendeleo Zaidi katika sekta zote kiuchumi, kisiasa, kijamii na kiutamaduni. Pia katika masuala ya kimaendeleo hatuna budi kujiepusha na maadui wakiwemo uvivu, kukata tamaaa pamoja na kuwaruhusu mabeberu kutoka nje watushike masikio. Maendeleo ya jamii ni jukumu letu sote.

NAOMBA KUWASILISHA
 
Upvote 1
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…