philosophia1
New Member
- Jun 7, 2024
- 1
- 0
Elimu ya Tanzania imekumbwa na changamoto nyingi kutokana na kutokuwa na mtaala unaoendana na maendeleo ya sayansi na teknolojia.pamoja na kwamba serikali inajitahidi sana kuboresha na kuanza kwa mtaala mpya ila Bado haukidhi matarajio ya miaka 5 Hadi 25 ijayo kutokana na sababu zifuatazo.
wanajua hakuna kufeli..
Nini kifanyike ili kuifanya Tanzania kuwa na elimu Bora itakayoleta watu Bora kwenye nyanja zote.
Hayo ni machache kati ya mengi ninayotamani kuyaona miaka mitano Hadi ishirini na Tano ijayo yakitimia ili kujenga Tanzania yenye wasomi wenye maadili na wanaothamini taaluma zao na kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye maendeleo zaidi kwa watu wake,Afrika na Dunia mzima.
- Umri wa kuanza shule ya msingi kuanza na miaka sita na kumalizia wakiwa na miaka kumi na Moja hawataweza kumudu kuchagua fani wanapokuwa sekondari.
- Somo la kusoma na kuandika halipewi kipaombele ndio maana mpaka sasa Kuna wanafunzi hawajui kusoma na kuandika.
- Masomo yanayofundishwa Bado ni mengi hivyo hayaendani na umri wa watoto hivyo huwafanya wanafunzi kuona shule ni ngumu.
- Mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji hayaendani na mabadiliko yanayotarajiwa.
- Umri wa mtoto kuanza sekondari miaka 11 ni mdogo sana kwa mtoto kutambua fani Gani kweli ananipenda.
- Zana za ufundishaji na ujifunzaji ni duni sana.bado waalimu wapo kwenye kuandika kwenye manila cards ,ubao na chaki badala ya kutumia computer au projector angalau wanafunzi kupata mwangaza wa kile wanachojifunza kimefananaje.
- Mlundikano wa wanafunzi darasani Bado ni tatizo na sio mbali mwaka 2027 darasa la sita na lasaba watamaliza pamoja sekondari zitakuaje kama Bado mpaka sasa darasa Moja watoto zaidi ya mia.
- Hadhi ya waalimu wanaofundisha haziendani kwani mwalimu mwenye c na d ndiye anayedahiliwa kwenda kusoma ualimu ili aje kumfundisha enginear,dactari,pilot ajaye.
wanajua hakuna kufeli..
Nini kifanyike ili kuifanya Tanzania kuwa na elimu Bora itakayoleta watu Bora kwenye nyanja zote.
- Mtoto anayeanza elimu ya primary sharti awe na miaka Saba hii itasaidia akifika darasa la sita na miaka 13 angalau atakuwa na uwezo wa kujieleza vizuri.
- Masomo yanayofundishwa yasizidi matano na yote yaendane na Hali halisi ya maendeleo ya sayansi na teknolojia pamoja na mazingira ya Tanzania.
- Somo la stadi za kazi lipewe kipaombele na mtoto afundishwe shughuli mbalimbali zinazoendana na mazingira aliyopo kwenye jamii inayomzungukamfano. Kustuka,kupamba,kupika,kufuma na mengine mengi.
- Mazingira ya ujifunzaji na ufundishaji yaendane na mabadiliko ya mtaala husika.wanafunzi wajifunze kwa vitendo zaidi kuliko kukaa darasani na kukariri notes.
- Mwalimu anayefundisha elimu ya msingi sharti awe na diploma na sekondari degree na wote wawe wamefanya vizuri matokeo ya kidato Cha nne na sita kama ilivyo kwa kada ya udaktari.
- Mwanafunzi asome masomo yanayoendana na fani anayoipenda.mfano kama anataka kuwa daktari ,asome masomo yanayoendana na fani ya udaktari vivyo hivyo kwa kada nyingine tokea anaanza form one.
- Pawe na maandalizi ya kubadili mtaala miaka kumi Hadi ishirini ili kuwapa fursa waalimu kwenda kupata mafunzo kwa ajili ya mtaala mpya hiyo itasaidia sana kuleta mabadiliko makubwa kwani tayari mwalimu atakuwa na uelewa mkubwa na kuufanyia kazi mtaala kwa vitendo kama unavyotakiwa.
Hayo ni machache kati ya mengi ninayotamani kuyaona miaka mitano Hadi ishirini na Tano ijayo yakitimia ili kujenga Tanzania yenye wasomi wenye maadili na wanaothamini taaluma zao na kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye maendeleo zaidi kwa watu wake,Afrika na Dunia mzima.
Upvote
2