TANZANIA TUITAKAYO MIAKA 5 MPAKA 25 KATIKA MAENDELEO YA KIUCHUMI
Tanzania ni nchi yenye uchumi wa kati-chini (middle lower income) kulingana na tafiti na taarifa ya Benki ya dunia ya tarehe 1 julai, 2020, hiyo ni miaka mitano kabla ya muda ambao Tanzania ilijipangia katika Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025. Uchumi wa kati-chini kwa Tanzania unaonesha bado kuna hitaji kubwa la mapambano kwa mwananchi mmoja mmoja na nchi kwa ujumla. Maendeleo ya nchi si jambo la kutokea kwa ghafla bila kuwepo kwa maandalizi, na maendeleo yanayohitajika zaidi ni yale ya kumgusa mwananchi moja kwa moja na siyo yanayohusisha vitu pekee. Yafuatayo ni mambo machache yanayoweza kusaidia nchi hii kutoka katika uchumi wa kati-chini kwenda uchumi wa kati.
Elimu, ni kutoa maarifa, ufahamu au ujuzi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Maarifa ni njia inayotumiwa kujitoa katika shida ama kuweza kupata kitu kwa kutumia ujuzi. Ujuzi maana yake ni kufahamu, kujua au kuelewa hali, habari na maelezo. Ujuzi huo unaweza ukawa wa kuzaliwa nao, kusikia, kusoma na kujifunza. Ufahamu ni utambuzi wa kitu au jambo unalojihusisha nalo kwa kulinganisha na yale uliojifunza
Elimu inayohusu ufahamu na maarifa kwa kiwango kikubwa Tanzania kama nchi imepiga hatua kwa vile tuna watu wenye kiwango cha elimu ya astashahada, stashahada na shahada. Japokuwa kwa suala la ujuzi (skills) elimu ya Tanzania bado inasuasua kwa vile tumewekeza zaidi katika upatikanaji wa vyeti vyenye alama za kuvutia bila kuzingatia utendaji kazi. Ni nadra sana kumpata mtu mwenye ufahamu na maarifa yanayoendana na ujuzi wake. Ili tuweze kupiga hatua serikali inatakiwa itoe msisitizo katika ujenzi wa shule bora za msingi na sekondari pamoja na wa vyuo vya kati vinavyoandaa watenda kazi na siyo wasimamiaji kwa namna kuu tatu.
Moja, shule na vyuo hivyo vijengwe kwa viwango cha kimataifa vitavyoweza kutoa wabunifu wanaoendana na mahitaji ya dunia ya sasa. Nchi yetu ina shule na vyuo vya kutosha lakini tatizo kubwa ni kwamba ubora wa elimu inayotolewa bado ni wa kiwango cha chini. Mhitimu anapimwa kwa namna moja ya kile anachoweza kuandika na siyo kufanya. Hata kwa vyuo vinavyopima uwezo wa kiujuzi, havipimi kwa kiwango cha juu ili kumfanya mwanafunzi afikirie zaidi ya kile alichokisoma katika vitabu au kufundishwa na mwalimu.
Pili, kuongeza idadi ya wakufunzi wenye viwango vya elimu inayostahili. Idadi ya wanafunzi katika shule zetu na vyuo vyeti ni kubwa ukilinganisha na walimu au wakufunzi. Sera ya elimu ya kimataifa ya mwaka 1976 inaonesha wazi wanafunzi 40 yafaa wasimamiwe na mwalimu mmoja. Kwa takwimu za mwaka 2024 kutoka tume ya utumishi wa walimu (TSC) zinaonesha idadi ya walimu wa shule ya msingi ni 173,591. Idadi ya walimu wa shule za sekondari umetajwa katika takwimu za wizara ya tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) kwa uwiano wa mwaka 2016 kwamba ilikuwa wanafunzi 42 kwa mwalimu mmoja, kufikia mwaka 2022 ikawa wanafunzi 65 kwa mwalimu mmoja. Hii inasababishwa na serikali ya awamu ya tano kutoajiri walimu kwa idadi inayoendana na ongezeko la wanafunzi. Wakati huo huo kuna baadhi ya wilaya iliripotiwa kuwa na uwiano wa wanafunzi 100 kwa mwalimu mmoja. Idadi hiyo ya wanafunzi ukilinganisha na ya walimu inaonyesha wazi kufikia lengo la kutoa elimu bora ni kitendawili kianchohitaji kuteguliwa.
Tatu, kutenga bajeti ya kuendelea kutoa mkopo ya elimu kwa wanafunzi wote wa vyuo vya kati. Elimu bila malipo kwa shule za msingi na sekondari umeongeza idadi ya wanafunzi wa elimu ya kiwango hicho hivyo basi ni vyema wanafunzi watakaochaguliwa kujiunga na vyuo vya kati kuwepo na bajeti itakayowezesha wanafunzi wa vyuo vya kati kunufaika na mikopo hiyo. Kuongezeka kwa wahitimu wa vyuo vya kati kutaongeza wasomi watenda kazi na siyo wasomi wasimuliaji wanaotokana na vyuo vikuu tulivyonavyo.
Utafiti na ubunifu, utafiti ni uchunguzi wa taalamu kuhusu jambo fulani ili kupata majibu yatakayoakisi uhalisia wa mambo katika jamii. Ubunifu ni matumizi ya fikra ili kutengeneza kitu halisi. ubora wa elimu itakayotolewa itasaidia sana katika ubunifu na utafiti. Mao Tse Tsung, Rais wa kwanza wa jamhuri ya watu wa China aliwahi kusema ‘no research no right to speak’ ukiwa hujafanya utafiti huna haki ya kuzungumza. Kwa kiwango hicho cha elimu kilichopendekezwa kitasaidia wasomi hao kuyasoma mazingira yao na kufahamu kitu gani kianchohitajika na kwa kiwango gani. Hii itasababisha ubunifu ambao utawezesha ukuaji wa kisayansi na kiteknolojia. Ukuaji huo utasababisha maendeleo ya viwanda vitavyotengeneza bidhaa zinazohitajika. Ubunifu unaweza kuanzia vitu vinavyochukua nafasi na kipato kidogo. Kiwango cha teknolojia ya sasa umeme ni nguzo muhimu hivyo basi kwa ubunifu vyanzo vya umeme kama vile upepo, joto ardhi, jua na maporomoko ya maji yanaweza kubuniwa kwa kutegemea mkoa au kanda husika.
Ubora wa elimu utaisaidia Tanzania kupata wataalamu kwa ajili ya uendelezaji wa miundo mbinu, huduma za kijamii na shughuli za kiuchumi hivyo kupelekea kupata maendeleo ya kweli.

Upvote
3