SoC04 Maendeleo ya kweli yataletwa na mabadiliko kwenye mfumo wa elimu

SoC04 Maendeleo ya kweli yataletwa na mabadiliko kwenye mfumo wa elimu

Tanzania Tuitakayo competition threads

mxrereco

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2014
Posts
1,906
Reaction score
3,986
Habari wana jukwaa.

Ni ukweli usiopingika kuwa maandalizi ya mtu mzima huanza utotoni, na hii ndio sababu binadamu hupewa elimu kuanzia kwenye umri wake wa utoto ili imsaidie kwenye utu uzima wake. Elimunni maarifa ambayo mtu huyapata kwa njia mbalimbali ikiwemo kufundishwa na watu wenye uelewa wa jambo hilo.

Kwenye nchi yetu tumekua na mfumo wetu wa elimu ambao tumeridhi kutoka kwa wakoloni japo yapo maboresho madogo madogo ambayo yamefanyika kwenye mfumo ili kuboresha. Kwa kuzingatiabkuwa elimu ni maarifa ambayo mtu huyapati si tu yamsaidie yeye mwenyewe baadae bali pia kusaidia taifa zima kwa ujula.

Kwa kuzingatia mwenendo wa dunia kwa sasa, ni dhahiri kuwa mfumo wetu wa elimu umepitwa na wakati na unatakiwa kutengenezwa upya kwa maslahi mapana ya taifa. Wakati nchi inapata uhuru, nchi ilihitaji zaidi watu wenye taaluma ili wapate kujaza nafasi zilizoachwa na wakoloni. Nchi ilihitaji madaktari, wahasibu, waalimu na taaluma zingine ili waweze kufanya kazi ambazo tayari zilikuwepo.

Kwa sasa mambo ni tofauti kabisa. Tayari tunao wataalamu wa kutosha kwenye kila taaluma, na wengine wengi wapo wanazo taaluma ila hawana ajira, na bado kila mwaka vyuo vikuu vinaendelea kutoa watu wenye taaluma zilezile ambazo wengine wapo mtaani hawana ajira. Huu ndio muda sahihi sana wakubari mfumo wa elimu ili utoe wataalamu wa vitendo. Kwa sasa nchi inahitaji mafundi “technicians” zaidi na sio wasomi wa makaratasi.

Utengenezwe mfumo wa elimu ambao utamfanya muhitimu akajiajiri. Elimu ianze kumuandaa mtaalamu wa kesho kuanzia akiwa sekondari na sio ilivyo sasa, mwanafunzi anafika sekondari akiwa na miaka 13 bado hata wazazi hawajui anatakiwa kuwa nani ndio maana analazimika kusoma maosmo 7-11.

MAPEMDEKEZO
1. Ianze elimu ya awali mtoto akiwa na miaka 3,4-6. Hapa mtoto aanze kutambuliwa anachoweza au kupendabkufanya na taarifa yake iwepo.

2. Elimu ya msingi kwa miaka 5 (miaka 6- 11). Hapa ni elimunya mwendelezo wa kile alichotoka nacho elimu ya awali. Hapa ni kujua zaidi mtoto anaweza kufanya nini na ripoti yake iandikwe.

3. Elimu ya sekokdari miaka 3 (miaka 12-15). Mtoto aanze ku practice anachokipenda. Huku akipewa elimu ya kumuandaa kuwa na professional flani.

4. Elimu ya sekondari miaka 2 (miaka 16-18) hapa aendeleebkumariswa kwenye uelekeo wa professional yake. Hapa tupate wenye uwezo wa kuwa na professional za darasani tu. Wale wenye bipaji vingine waende kuendeleza vipaji vyao

5. Elimu ya chuo kikuu muda ukiwa kama ulivyo sasa kulingana na taaluma ni vizuri.

Ili ifanikiwe mambo ambayo hayana faida kwa wanafunzi yaondolewe kabisa. Kuna vitu mtoto anafundishwa havina umuhimu kabisa.
 
Upvote 3
Back
Top Bottom