SoC04 Maendeleo ya miaka 10 ijayo ni kwa nguvu ya wananchi na serikali ya Tanzania

SoC04 Maendeleo ya miaka 10 ijayo ni kwa nguvu ya wananchi na serikali ya Tanzania

Tanzania Tuitakayo competition threads

Hussein Kimosola

New Member
Joined
Jul 23, 2023
Posts
1
Reaction score
0
Tanzania imara Baada ya Miaka mitano , kumi ama zaidi haitawezekana pasina Jitihada za Pamoja baina ya serikali na Wananchi kupitia Asasi za kiserikali na zisizo za kiserikali.
Aidha jitihada hizo zihusishe maeneo nyeti kama Sekta ya ELIMU, UCHUMI, AFYA, KILIMO, VIWANDA, BIASHARA, MIUNDOMBINU YA USAFIRISHAJI, SAYANSI NA TEKNOLOJIA.

Kwa Maono yangu na Tafakuri makini nitagusa maeneo yote muhimu kutokana na namna yalivyo na uhusiano mkubwa katika utekelezaji wake.

1. Kuboresha utekelezaji wa Elimu: serikali inapaswa kuboresha utekelezaji wa Elimu kwa kuhakikisha kwamba kila sehemu ya nchi inapata elimu iliyo bora. Kuhakikisha maeneo ya vijijini yanapata elimu iliyo kuwa bora kama zile za mjini. Pia Taasisi ya Elimu inapaswa kutoa taarifa za elimu kwa njia rahisi kwa wengi Kuzipata na kuzifanyia kazi ili kuepuka changamoto ya wengi wa wanafunzi kufeli ama kushindwa kuendelea na masomo.
Kwa elimu inayotolewa pia inapaswa kuhakikisha mitaala inamsaidia mtu kuwa na uwezo wa kufanya jambo lolote la kimaendeleo na kutosubiri kuajiriwa kama ilivyo sasa maana hali hiyo husababisha kuwa na wasomi wengi mtaani wasio na jambo muhimu la kufanya zaidi ya kusubiri kuajiriwa.

2. Kuboresha sekta ya Kilimo; Ingawa kwa muda sasa Mgongo wa uchumi wa Tanzania ni Kilimo Lakini bado kwa ujumla tunazalisha kwa kiwango kidogo na ubora wa hali ya chini. Hivyo serikali inapaswa kutoa elimu ya Kilimo kwa Wakulima wa mashamba makubwa kwa kwa Madogo pamoja na kutoa mikopo kwa wakulima hao sambamba na kutoa msaada wa kuwapa maeneo yenye rutuba tayari kusaidia sekta ya kilimo. Pia Serikali itafute masoko ya uhakika ya mazao yanayozalishwa hapa nchini na kupelekea tuwe na mazao mengi ya chakula na biashara na kuepusha janga la kupanda kwa bei ya chakula ambapo hukwamisha maendeleo ya nchi yetu na hivyo kuwa na hofu ya kukosa chakula itakayoweza kusababisha njaa.

3. Kuboresha sekta ya Viwanda; ili nchi iwe na maendeleo makubwa inapaswa kuboresha sekta ya viwanda kutoka kwenye viwanda vidogo kuwa na viwanda vikubwa vingi vyenye uwezo wa kuchakata malighafi kutoka kwenye sekta ya kilimo kukua na husaidia kuzalishwa kwa bidhaa nyingi nchini. Sio juhudi za serikali tu bali pia Mtu binafsi Mfano kama vile MO DEWJI , BAKHRESA na Wengine ambao wameendelea kuwekeza katika sekta ya VIWANDA na kutoa fursa ya ajira kwa Watu mbalimbali nchini na kuchochea maendeleo kwa Taifa zima.

4. Kuboresha sekta ya Afya; Maboresho katika sekta ya afya kwa kujengwa hospitali kubwa kama MUHIMBILI katika maeneo mengi ya nchi ambapo itasaidia kutibu watu wengi na kuepusha adha ya kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma Bora za afya. Katika hili pia Tanzania inapaswa kuhakikisha inahamasisha na kutoa wito kwa wengi wa wanafunzi kusomea Tahasusi za Sayansi hasa kuhusiana na Afya moja kwa moja ili kusudi kuwe na idadi kubwa ya Wataalam watakaoweza kuhudumu maeneo mbalimbali nchini.
Sambamba na hilo Kupitia familia zetu wazazi na walezi wanajukumu kubwa kuhakikisha familia zao zinazingatia mazingira safi na salama ya utunzaji afya zao ili kutopoteza nguvu kazi kwa sababu zinazoweza kuepukika. Aidha pia Matumizi ya Sanaa katika kuelimisha jamii juu ya mbinu za Utunzaji wa Afya hasa katika mambo yanayopendwa zaidi kama vile kuweka matangazo katika Vipindi vya MICHEZO , Nyimbo za Bongo fleva , Filamu na Tamthilia.

5. Kuboresha Miundombinu ya usafirishaji; serikali inapaswa kuboresha na kukuza shughuli za usafirishaji kwa nyanja zote Majini, nchi kavu na hata angani kwa kuongeza idadi ya Ndege zenye uwezo mkubwa na kusafiri kwa umbali mrefu.

Pia kutokana na uwepo wa vyanzo vingi vya Maji kama Bahari, Mito na maziwa pia bado sekta ya usafirishaji kwa njia hii uko chini hivyo tunapaswa kuboresha sekta hii kupitia uwekezaji wa ndani na nje sambamba na ujenzi wa Bandari nyingi zaidi ambazo zitawezesha kupokea meli kubwa zenye uwezo wa kusafirisha bidhaa kwenda kwenye mabara mengine.

Kwa nchi kavu bado jitihada zinatakiwa zaidi hasa katika Ujenzi na uboreshaji wa Miundombinu mibovu ya barabara na reli ili kuruhusu kukua kwa sekta hiyo ambako kutaambatana na sekta nyingine kama vile Viwanda, Biashara na Kilimo.

6. Kukuza Kiwngo cha Sayansi na Teknolojia nchini; kwa kuwa na vifaa vya kisasa vyenye teknolojia ya juu kwenye mitandao na elimu itasaidia kuwezesha utekelezaji wa baadhi ya masuala ya kimaendeleo kwa wepesi na uharaka zaidi. Hapa sio serikali pekee bali hata asasi zisizo za serikali na wanachi wanayo nafasi kuchagiza maendeleo katika hili kama tunavyoona kupanda kutoka Grneration za chini za kimtandao hadi kufikia Generation ya Tano ya kimtandao.

Kwa upande mwingine maendelea ya sayansi na trknolojia yatawezesha mchakato wa Upatikanaji wa Rasilimali mbalimbali kama MADINI na GESI kwa kutumia wataalamu wa ndani ambapo kwa kiasi kikubwa tutakuwa tunazuia mianya ya unyonyoaji wa Makampuni ya nje. Aidha kwa kufanya hivyo itaongeza mapato ya ndani moja kwa moja na kufanya nchi iwe na maendeleo.

7. Kuboresha soko la Biashara ndani na nje ya nchi. Serikali inapaswa kuboresha soko la ndani hali itakayowawezesha Wakulima na wazalishaji wa ndani na nje kupendezwa na mazingira haya hali itakayowafanya waongeze uzalishaji kwa faida yao na Taifa kwa ujumla hasa kupitia KODI.
Pia kwa upande wa Soko la nje serikali inapaswa kuwekeza nguvu kubwa katika kutafuta masoko ya nje ambayo yatatoa bei rafiki kwa bidhaa zetu pasina unyonyaji ili kushawishi wazalishaji wa ndani wapate nguvu zaidi ya kuzalisha. Kupitia Biashara hizi za mauziano ya ndani na nje zitaitambulisha nchi maeneo mbalimbali Duniani hali itakayofungua fursa mbalimbali za kidiplomasia nankuchochea maendeleo.

Kwa ujumla Jitihada hizo zikifikiwa kwa Kina nchi ya Tanzania itakuwa ni nuru njema sana na kitovu cha maendeleo kwa Mataifa ya Africa na Dunia kwa ujumla ila haitafikiwa hatua hii mpaka jitihada ziwe za Pamoja. Inafahamika kuwa Serikal ndiye msimamizi mkuu wa michakato yote ya kimaendeleo lakini watekelezaji halisi ni wanachi.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom