SoC02 Maendeleo ya Sekta ya Kilimo kupitia mradi wa ASDP nchini Tanzania

SoC02 Maendeleo ya Sekta ya Kilimo kupitia mradi wa ASDP nchini Tanzania

Stories of Change - 2022 Competition

Lapluto

Member
Joined
Jul 14, 2022
Posts
80
Reaction score
129
UTANGULIZI.

Sekta ya kilimo ni moja ya sekta muhimu na tegemezi kwa uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara kupitia ardhi. Kwa Tanzania asilimia kubwa ya ardhi yake hutumiwa kwa kilimo cha chakula na wakulima wadogo wadogo. Kupitia wizara za kilimo (ASLAMs) serikali imeamua kuendeleza sekta hii kwa kuanzisha programu maalumu iitwayo ASDP yenye awamu tofautitofauti ambazo hadi sasa zimefika awamu mbili. Awamu ya kwanza ili tekelezwa kuanzia mwaka 2006/2007 hadi 2013/2014 , awamu ya pili ni mpango ambao unatarajiwa kutekelezwa ndani ya miaka kumi ulioanza 2017/2018 na unatarajiwa kufanikiwa
au kukamilisha majukimu yake hadi ifikapo mwaka 2027/2028.
download (1).jpeg.jpg

(Picha kutoka mtandaoni)
Mafanikio ya awamu ya kwanza (ASDP I).
Katika mradi huu wa awamu ya kwanza kwa mujibu wa toleo la ASDP II imeonesha awamu ya kwanza imefanikiwa kuboresha uandaaji wa mipango ya maendeleo ya kilimo ya wilaya (DADPs) kwa kushirikisha jamii na utoaji wa fedha kwa mradi huu, ambapo asilimia 75 ni wilayani, asilimia 5 mkoani na 20 ni kwa taifa. Kuboreka kwa utoaji mafunzo, vifaa na usafiri kwa ngazi ya wilaya, mkoa hadi taifa, kuboreka kwa shughuli za utafiti, kuongezeka kwa matumizi ya pembeheo, kukarabati na kujengwa kwa skimu ya umwagiliaji kutoka hekari 264,338 (2006/2007) hadi hekari 461,329 (2014), mabadiliko ya bei hayakubadilika na kusaidia kupungua kwa mfumuko wa bei kutoka asilimia 7.0 (2006) hadi asilimia 5.56 (2010), na asilimia 5.6 (2015); na mwezi Oktoba 2016 mfumuko wa bei ulishuka hadi asilimia 4.5. Ikiwa bei ya mazao ya nje ya nchi ilipungua kwa mazao ya biashara kama vile chai, pamba, kahawa na korosho, uwepo wa masoko nao ulikuwepo.

Changamoto za awamu ya kwanza (ASDP I).
Katika utekelezaji wa programu hii ulikumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo uongozi na usimamizi hafifu kuanzia ngazi ya wilaya ambao ulisababisha kuwepo kwa miradi midogo midogo, mkoa hadi taifa, mabadiliko ya Hali ya hewa , kukosekana kwa mfumo imara wa ufatiliaji na tathimini ambao hukutoa taarifa sahihi, uwezo mdogo wa kupanga, kusimamia na kutekeleza niradi pamoja na uwezo mdogo wa kifedha na kitaalamu.

Awamu ya pili (ASDP II).
Awamu hii ya pili (ASDP II) imetayarishwa ili kuendana na mikakati ya kitaifa. Mikakati hiyo ni pamoja na mpango wa maendeleo wa miaka mitano (2016 - 2021), mpango wa uwekezaji katika sekta ya kilimo (TAFSIP - 2011), dira ya maendeleo ya taifa (2025), mpango wa maendeleo ya muda mrefu (2012 - 2021) ikiwa na lengo la kufanya mageuzi katika sekta ya kilimo na kuhakikisha inaondoa umasikini kwa kukuza pato la mkulima na taifa kwa ujumla ifikapo mnamo mwaka 2025. Kupitia changamoto za awamu ya kwanza, ASDP II imejipanga ili kuhakikisha inapunguza au kuondoa changamoto zote zilizotokea awamu iliyopita (ASDP I).
download (2).jpeg.jpg

(Picha kutoka mtandaoni)
Malengo, mikakati na Matokea ya ASDP II.
Kwa upande wa malengo imepanga kufanya mageuzi katika sekta ya kilimo kwa kuinua pato la mkulima, kuongeza uzalishaji wa mazao na kufanya kilimo kiwe cha kibiashara zaidi pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa chakula kwa lishe Bora. Upande wa mikajati imepanga kuhakikisha kilimo kinakuwa cha kibiashara zaidi kuliko kujikimu na kuhakikisha upatikanaji wa masoko ya mazao. Matarajio ya mradi huu ni kuongezeka kwa uzalishaji, upatikanaji wa masoko, kuongeza pato la mkulima hadi taifa pamoja na kuongezeka kwa thamani ya mazao.
images.jpeg.jpg

(Picha kutoka mtandaoni)
Hali ya sekta ya kilimo kwa sasa ukilinganisha na matarajio.
Hali ya sekta ya kilimo bado ni tete na hata matarajio ya mradi yamefeli kwa kiasi kikibwa kuanzia mradi wa kwanza (ASDP I) na huu wa sasa kutokana na sababu mbalimbali. Sababu hizo ni kutowajibika kwa viongozi kuanzia ngazi ya chini hadi taifa, kuongezeka kwa mfunuko wa bei ya vyakula na mazao ya biashara, kushuka kwa pato la mkulima sababu ya ongezeko la bei za mazao, matumizi duni ya tehama na utafiti wa kina juu ya uzalishaji wa mazao, uwepo wa elimu duni juu kwa wakulima chasa ngazi ya wilaya, mfumo usio bora katika ufatiliaji wa taarifa, kukosekanao ya uhakika nje na ndani ya nchi panoja na kutokuwepo kwa sera bora ya ugawaji wa ardhi kwa vijana. Pia mradi huu wa pili umeshindwa kuendana na mikakati ya kitaifa.

Mapendekezo juu ya mradi (ASDP) ili kuendeleza sekta ya kilimo.

  • Kuhakikisha kiongozi bora anapatikana ili uwajibikaji na utekekezaji wa mradi unafanyika ipasavyo. Utawala bora utachochea mikakati yote inafanya kazi kwa ngazi zote hadi kitaifa.

  • Kuboresha utoaji elimu kwa wakulima kwa kusaidiana na wataalamu kupitia vyuo vya ndani na nje ya nchi. Serikali pamoja na wizara husika inapaswa kuhakikisha kila mkulima anapata elimu kabla ya kuanza utekekezaji wa mradi kwa maendeleo ya kilimo.

  • Kama lengo la mradi ni kuinua hali ya mkulima basi inapaswa ihakikishe upatikanaji wa mazao ya chakula nchini ni wa kutosha. Baada ya hapo ndio zao la kibiashara litekelezwe huku wakulima wakiwa na afya bora kutokana na utoshelezi wa mazao ya chakula.

  • Kushirikiana na makampuni binafsi na kuimarisha mazingira weseshi kwa wawejezaji wa ndani na nje ya nchi kwa mikataba yenye manufaa kwa nchi.

  • Kutafuta masoko ya uhakika jwa mazao ya chakula pamoja na biashara kupitia wawejezaji na matumizi sahihi ya teknolojia.

  • Kuhamasisha matumizi ya teknolojia (uendeshaji namitambo na uundaji programu au mfumo) utafiti wa kisayansi, wataalamu wa masuala ya tehama wanapaswa kukumbukwa na kupewa kipaumbele pamoja na
    wataalamu wa uendeshaji wa mitambo na watafitii kwa ngazi zote ili kuhakikisha ufatiliaji wa na ukusanyaji wa taarifa, pamoja na uzalishaji wa mazao unaketa matokeo chanya.

  • Kuandaa wataalamu katika sekta ya kilimo kwa kuwapekeka wanafunzi katika maeneo ya uzalishaji hata kwa msimu mzima. Kupitia upelekaji wa wanafunzi itasaidia kuongeza utoaji wa elimu kwa wakukima.
    "Kilimo ni uti was mgongo" kama kilimo ni mhimili na kichocheo cha sekta nyingine basi tunapaswa kuwekeza zaidi katika sekta hii.

  • Pia, tunapaswa kuunda mfumo utakao unganisha wataalamu wa hali ya hewa, teknolojia, watafiti, viongozi pamoja na wakulima ili kuhakikisha maendeleo ya sekta ya kilimo yanaenda ipasavyo kupitia usahihi wa taarifa na takwimu zitakazotolewa.

  • Kuboresha miundombinu kwa ngazi zote kama vile barabara ili kurahisisha usafirishaji wa mazao

  • Kutoa elimu juu ya uvunaji wa mvua kwa ajili ya umwagiliaji wa mazao hasa ya chakula.

Hitimisho.
Nipende kutoa shukrani kwa uanzishaji wa mradi huu mzuri wenye malengo ya kuleta tija kwa watanznia. Utekekezaji wa meadi huu unategemea na uwajibikaji wa utawala bora. Kupitia uwajibikaji bora utasaidia kupunguza changamoto za njukima hasa katika suala la umasikini. Mradi wa pili unatarajia kuoata mafanikio jufikia 2025 ila bila ya utekekezaji mzuri hautozaa matunda.

Karibu kwa nyongeza zaidi ili kuimarisha sekta ya kilimo.
 
Upvote 5
Shida kubwa ipo kwenye usimamizi!! Viongozi wengi si wawajibikaji na wengi wanachukulia kilimo kwa mazoea
 
Shida kubwa ipo kwenye usimamizi!! Viongozi wengi si wawajibikaji na wengi wanachukulia kilimo kwa mazoea
structure nzuri ya uongozi imekuwa ni tatizo kubwa pamoja na uwajibikaji katika sekta hii. Tunapaswa kuhakikisha tunapata viongozi Bora na wenye utaalamu na masuala ya kilimo.
 
Back
Top Bottom