Uchaguzi 2020 Maendeleo ya vitu, maendeleo ya watu, yote ni maendeleo ya binadamu

Uchaguzi 2020 Maendeleo ya vitu, maendeleo ya watu, yote ni maendeleo ya binadamu

Leslie Mbena

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2019
Posts
207
Reaction score
677
MAENDELEO YA VITU, MAENDELEO YA WATU,YOTE NI MAENDELEO YA BINADAMU.

Leo 13:30hrs 11/10/2020

Ni suala la yai na kuku, bila ya vitu kwa maana ya Miundo mbinu kama Reli, barabara, Umeme,Viwanja vya ndege,ndege,Bandari,Vituo vya Afya hakuna maendeleo ya watu, na ukianza kuwawekea watu hela mifukoni mwao au kupanda na kuvuna leo bila ya miundo mbinu hakuna mahali tutaenda, hivyo kwangu,watu wanategemea vitu,kwa maana barabara ataitumia mtu, Rais John Magufuli yuko sawa kabisa kwa kila Maendeleo afanyayo kwani yote ni Maendeleo ya binadamu,hivyo kama akituacha na fast train SGR treni ya Umeme Dar-Tabora-Mwanza/Kigoma,Bwawa kubwa la Umeme wa zaidi ya 5000 Megawatt,Meli kubwa kwenye Bahari na Maziwa Victoria, Tanganyika,Nyasa,Mafly Over Mwenge,Morocco,Uhasibu kupunguza foleni Dar, automatically Maendeleo ya watu yatakuja yenyewe,

Ndugu zangu Watanzania,hapo zamani tulikuwa tunatumia siku tatu Dar hadi Mwanza,kupitia Nairobi,zamani tulikuwa tunatumia siku tatu Arusha hadi Tabora,tulitumia siku tatu Dar hadi Kigoma lakini Ujenzi wa treni ya Umeme utakufanya utumie masaa sita tu,utaokoa pesa ya kulala lodge njiani,pesa ya kula na kunywa,utaokoa zaidi ya laki moja au mbili ambayo ingepotea njiani wakati ukisafiri toka Dar hadi Kigoma,Dar hadi Mwanza au Arusha hadi Tabora,haya ni Maendeleo ya watu ambayo yamekuja baada ya Ujenzi wa treni ya Umeme ambayo ni Maendeleo ya vitu,kumbuka kwa mfanyabiashara anayepoyeza muda njiani anapoteza pia na mauzo,kuna watu watakuja watamkosa akiwa safarini,vyote vinaingia kwenye kitabu cha hasara kwenye mauzo,lakini treni ya Umeme itamsaidia kuokoa muda na kuwahi mauzo na hivyo kupata faida na mwisho wa siku atalipa kodi Serikalini.

Huwezi kuwa na maendeleo ya watu bila kuwa na maendeleo ya Vitu kwanaza,kwa nini mnapenda kwenda Ulaya au Marekani na mkifika uko mnashangaa mkiangalia barabara za juu,majengo mazuri,miundo mbinu mizuri ya barabara inayowawaisha watu kazini na kwenye biashara zao,It is that simple,ni Maendeleo ya vitu ndio yanaleta Maendeleo ya binadamu,Baba wa taifa,Mwalimu Julius Nyerere ndio muasisi wa Maendeleo ya vitu, Reli ya standard gauge ya miaka ya sabini Tazara,Ujenzi wa Viwanda,Ununuzi wa Ndege za ATCL,Ujenzi wa Bandari ya Dar es Salaam na miundombinu mingi yeye ndio muasisi na wengine hapo katikati waliyavurunda hayo yote lakini Rais John Pombe Magufuli anavirejesha vile vya Baba wa taifa hivyo kwa wale kutwa nzima kulalamika oh kwa nini kaanza na Maendeleo ya vitu,tafuteni chaka lingine la kulaumu ila sio kwenye Maendeleo ya vitu yanayochagiza Maendeleo ya binadamu.

-Scale of Preference;

(Sera ya Maendeleo ya Vitu kwa sasa)

Katika lectures ya "Human centred development" unaweza kuwarejea Julius Nyerere,Kwame Nkrumah ambao walibadilisha msimamo wa socio-economic systems(ujamaa policy -African sociolism,ISI policy from latin ) hizi ni transformation za economics,politics etc baada ya European kuuharibu uchumi wetu kipindi cha ukoloni na baadae kuzitambulisha sera za IMF na World Bank yaani SAPs pengine kutusaidia lakini kwa maslahi yao wazungu,Sasa basi katika wakati tuliopo sasa, Miundombinu bora ina nafasi chanya ya kuwajibu Watanzania wengi na kubariki maisha yao,Nani afanye hilo ambalo kweli Ujenzi wa miundi mbinu mipya ya reli ya Umeme,Viwanja vya Ndege,Ununuzi wa Ndege,Ujenzi wa Bwawa kubwa la Umeme la Mwalimu Nyerere,Wilayani Rufiji,ambavyo ni vitu vya gharama kwa Taifa na kwa Wananchi,Nani afanye hivyo ili kuokoa hatma ya Taifa la Tanzania,lazima awepo mtu wa kujitoa sadaka kwa ajili ya kesho ya Taifa la Tanzania.

Pato la Taifa,GDP likiongezeka ni rahisi kuimarisha miundo mbinu kwa faida ya kila mwananchi,mfano Mimi ni mlala hoi naishi Matombo, Morogoro, mke wangu mjamzito kapata tatizo la ghafla apelekwe Morogoro hosipitali ya Mkoa,na Matombo hadi Morogoro Mjini ni kilomita sabini,sasa maadamu barabara ni imara ni chapchap mpaka hospitali,kama barabara ni mbovu angefia njiani. Hivyo maendeleo ya vitu ni muhimu,pengine naweza nisiende Hospital ya Mkoa wa Morogoro kwa sababu kuna kituo cha afya kimejengwa hapa hapa Matombo, Morogoro.

Kwa Upande mwingine, Maendeleo ya vitu mfano treni ya Umeme inavyokatika katika mikoa mbalimbali,inaongeza uwezo wa jamii kupambana na mazingira yao kwa ujumla wao,na kila Mmoja atafaidika ndio maana uwekezaji kwenye miundombinu/miundo msingi,ujenzi wa barabara za lami,Uimarishwaji wa bandari na kupanuliwa kwa kiwango kikubwa, viwanja vya ndege na ununuzi wa ndege,Ujenzi wa reli ya kisasa, kudhibiti wizi wa mali ya umma na hasa maliasili za taifa hili,Kwa hakika hata nidhamu imerejea kwa baadhi ya viongozi na watumishi wa umma.

Mwalimu Julius Nyerere, alikuwa mchumi, aliyefuata sera za Karl max- Nguzo kuu za uchumi kuwa mikononi mwa umma- state controlled economy. Hata hivyo aliruhusu shughuli nyingine za kiuchumi kuendeshwa na watu binafsi na aliwatoza kodi,Mwalimu Julius Nyerere alijenga benki bora kabisa katika Africa,Benki ya NBC, kati ya benki 100 bora- NBC ilikuwa ya 12 ( 6 za kwanza kutoka South Africa, 4 kutoka Nigeria, 1 ya ghana na NBC ya TZ),Ujenzi wa reli ya Tazara,Mwalimu Julius Nyerere alikuwa ni mtawala pekee wa Africa wa enzi zake aliyeweza kujenga reli ya Standard gauge - ya zaidi ya km 1000- reli ya Tazara,lakini pia Mwalimu Julius Nyerere hakukubali kurusu uchimbaji wa madini hadi watu wetu wapate elimu ya kutosha kusimamia miradi hii,alisomesha watu wake wote bure na kwa scholarship nje ya nchi hadi wakati anatoka madarakani zaidi ya asilimia 80 walijua kusoma na kuandika na wastani wa kuishi ulikuwa miaka 62.

Daktari John Pombe Magufuli alizindua Program ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam muda huu (Juni 04, 2018).Programu hii ni ya miaka mitano na itagharimu Shilingi Trilioni 13.8.hii maana yake tulielekeza nguvu pia kwenye sekta ya kilimo,miundo mbinu itapokamilika,kilimo nacho kitakuwa kipo juu kwa maana kilimo ni priority sector number one kuendelezwa ili izalishe malighafi ya Tanzania ya Viwanda vitakavyokuja baada ya Umeme kutoka katika Bwawa la Julius Nyerere,Wilayani Rufiji.

Ukweli ni kwamba inapokuja ishu ya watu wanaodai ingeanza Maendeleo ya watu,Sasa hayo maendeleo ya watu,haiwekwi wazi ni maendeleo yapi hayo?Ni watu kuwa na pesa, majumba na magari au kuwa na well developed means of transport?Kilimo,Mashule au afya?Ni ukweli usiopingika watu katika kujadili maendeleo ya watu wanaongelea pesa mfukoni na kufanya manunuzi binafsi na ujenzi,Upande mwingine wanaona maendeleo ya miundombinu na uimarishaji wa njia za kiuchumi si maendeleo ya watu,wengine wanaenda mbali kushauri kwamba huwezi kuwekeza kwenye viwanda bila malighafi,Kwa upande wangu haya yote yanatokea Tanzania kwa kuwa tulichelewa kwa muda mrefu kufanya kwa serikali zetu kujisahau kuwekeza kwenye miundombinu,kilimo,ukusanyaji kodi,ajira,afya na kilimo,

Sasa basi kinachotokea sasa inaonekana hakuna priority sababu kila jambo tupo nyuma,ukisema uwekeze katika elimu ukasahau vingine watu wa kilimo watatoka kusema wamesahaulika,Ukisema uwekeze kwenye miundombinu vijana wasio na ajira wataona umewasahau,back to topic,kwa maoni yangu ni ngumu kuongelea maendeleo ya watu kama hujaweka mazingira mazuri ya maendeleo ya vitu,yani kama miundombinu hovyo,usafiri wa ndege hovyo,basi hata maisha kwa ujumla yatakuwa hovyo,ukinunua ndege utavuta watalii,tutapata mapato
Ukijenga miundombinu utarahisisha usafirishaji wa bidhaa,Ukikomalia viwanda utatengeneza automatic market point ya bidhaa zetu za kilimo na zingine,maoni yangu ni ngumu kuzungumzia maendeleo ya watu ikiwa hali ya maendeleo ya vitu iko hoi,

-Mwananchi afanye nini baada ya miundo mbinu yote kujengwa!?

1.Uzalendo - tutukuze vya kwetu sana vitakavyo zalishwa toka kwenye Viwanda vyetu, kama tukitumia bidhaa zetu hata kwa zile sekta za mashine zaidi itasaidia ukuaji na uhitaji wa bidhaa kutoka sekta zinazotumia binadamu sana.

2. Mwananchi anatakiwa kuja kufanya kazi kwa bidii,watu hawajatofautisha kufanya kazi sana na kufanya kazi kwa bidii.

3.Serikali itahitajika kutengeneza mazingira mazuri ya uendeshaji na ukuaji wa sekta zinazotumia binadamu zaidi mfano,mfano Viwanda,tayari Sera ya Serikali ni Serikali ya Viwanda, Serikali tayari inawekeza kwa wakulima ambao watalisha hivyo viwanda,na bidhaa za viwanda zitoke hapa hapa. Hii inamaanisha viwanda vitategemea wakulima/Wavuvi/Wafugaji na pia ukiachia viwanda na wafanyakazi wa viwanda pia watategemea itatengeneza muunganiko wa mzunguko wa fedha za sekta zote mbili,

4. Japo Watanzania tunategemea kilimo sana lakini asilimia kubwa ya wakulima hawafanyi kilimo cha biashara hasa kile ambacho ni cha uhakika wengi wanalima kwa kutegemea kudra za Mwenyezi Mungu,ni wakati sasa, Watanzania kufanya kilimo cha biashara, Watanzania tusipolima kilimo cha biashara,tusije kumlaumi mtu,na hii itafanya sekta ya Viwanda kukosa Malighafi na muda mwingine kusababisha kutafuta hizo malighafi nje.Serikali ipitishe na kutenga maeneo kwa ajili ya ukulima wa zao fulani kwa muda fulani ili kulinda rutuba na matumizi ikiwezekana hata iwe mfano yenyewe.

5. Serikali kutafuta masoko nje ya nchi pia tuna mabalozi nchi kibao na bado ardhi yetu ni kubwa tu na inarutuba, kama serikali ingekuwa inatangaza mfano kuna uhitaji mkubwa wa dengu sehemu fulani na kukiwa na kilimo cha uhakika wanaweza hata kuchukua tenda na wakulima wakalima kisha wakapeleka zikasafirishwa kwa Ndege zetu, kupitia utaalam na weledi wa kufanikisha hilo.

6.Kupunguza lawana na kufanya kazi, watu wanachukua muda mwingi kulalamikia Serikali kuliko kuwa sehemu ya utatuzi hili linafanya uchumi usipande na kurudi nyuma zaidi tunajikuta wachache wanaoziona fursa wanafanya kazi wanafanikiwa na uchumi unaonekana uko sawa kumbe wengi walikuwa wanaongea na wachache wamefanya.

Nimalizie kwa kusema Maendeleo ya vitu,ndio Maendeleo ya watu na kwa ujumla ni Maendeleo ya binadamu,Unaanza na maendeleo ya vitu, ambavyo vitatengeneza njia ya maendeleo ya watu. Unaanza na miundo mbinu imara ambayo inarahisisha maisha ya watu,unatandaza barabara nchi nzima ili mkulima wa ndizi kule Bukoba aweze kuzifikisha Newala au Tunduru,Unaboresha viwanja vya ndege ikiwezekana vyote, ili mtalii atoke Marekani na kutua Iringa ili aweze kufikia Ruaha kwa urahisi,Unakarabati meli za kwenye maziwa ili mfanyabiashara aweze kutoa bidhaa zake Kigoma na kuzifikisha Rukwa kwa urahisi,Maendeleo ya watu ni mchakato unaotegemea maendeleo ya miundo mbinu (vitu),Mzunguko wa fedha katika nchi kama Marekani na Ujerumani unawezeshwa na uimara wa miundo mbinu,Mtu anaishi New York lakini shughuli zake zipo Florida. Mtu anaishi Hamburg ambapo ni kaskazini ya Ujerumani lakini miradi yake ipo Ulm ambapo ni kusini kabisa, karibu na Switzerland.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master's in Leadership and Management.

-Research; Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Maendeleo ya watu hupimwa kwa vitu walivyonavyo ni ujinga kuamini vitu sio maendeleo. Serikali kusimamia sera na kuwaacha watu wajiletee maendeleo ni jambo jema lakini kwenye hao watu walioendelea kuna nani atajenga daraja atajenga reli atajenga stand nk... so kuamini ujenzi sio maendeleo ni ujinga wa kiwango cha lami...
 
Back
Top Bottom