Maendeleo ya zao la kahawa na maamuzi yenye kuleta tija

thinks b4 speak

Senior Member
Joined
Nov 23, 2017
Posts
142
Reaction score
121
Nawasalimu wote

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu.
Week iliyopita nilimsikia waziri mkuu wa tanzania akieleza nia yake ya dhati katika kuboresha zao la kahawa na kuakikisha linawanufaisha wakulima

Na kitu alichokisisitiza ni kutaka kurudisha vyama vya ushirika ndio wawe wana deal na uchakataji wa kahawa mbivu na uuzwaji wa kahawa hiyo ili kuakikisha mkulima anafaidika.

Malengo ya waziri mkuu ni mazuri kabisa but inabidi afanye utafiti zaidi na aelewe kwamba zao la kahawa lina process defu sana mpaka kufikia kupata kahawa iliyobora sio kama zao la korosho ambalo haliitaji gharama kubwa baada ya kuvunwa

kahawa upata bei nzuri kama imeandaliwa kwa kufuata taratibu zote ambazo zinapelekea kupata certificate either RFA au CAFE ambayo inampa mzalishaji access ya kuuza kwa premium price katika soko la dunia

Upataji wa kahawa yenye viwango vya kimataifa inaitaji gharama kubwa sana
Na gharama hizo uamzia katika kutoa elimu kwa mkulima jinsi ya kuandaa kahawa bora,uchakataji wa kahawa hiyo ambayo inapelekea ongezeko la gharama kwa zaidi ya asilimia 40% mpaka inapelekwa ghalani na hizo ni primary cost kuna other like milling,trasport so on.

Nilikuwa natafakari serikali wamejiandaa vipi katika kufanikisha mabadiliko makubwa hivyo ya mfumo wa zao la kahawa

Ngoja nizungumzie why vyama vya ushirika vinashindwa kufanya vizuri katika kahawa
Kwa kiasi kubwa ushirika unafell kucompite na private company kutokana uongozi mbovu wa ushirika
Wakulima wanazulumiwa sana na kudanganywa kwa kiasi kikubwa sana

Kwanini nasema hivyo.
Miaka kama minne nyuma kulitokea uwizi wa kahawa za vikundi vya ushirika MCCO(mbinga cooperative milling) ambapo kwa taarifa zilizozagaa kwa kipindi hicho sikumoja kontena zaidi ya mbili ft 40 zilipakiliwa usiku wa manane na kutokomea kusiko julikana kwa araka haraka ni zaidi ya gunia 1200 za clean coffee zilipotea but hizo ishu zinaimwa kimya kimya
Vile vile Wakati wa ukoboaji kahawa zinaibwa sana paka kupelekea lot moja ya kahawa kuwa na curing loss 40% hadi 45% ambayo ni wizi mkubwa sana ambapo normal inatakiwa icheze 17% to 20% losses
Hii hali inapelekea ushirika kushindwa kulipa malipo ya pili na wakulima na kuona ushirika sio sehemu sahihi ya kupeleka kahawa zao
Haya mambo almashauri wanayajua but inavyoonekana wanashirikishwa ndio maana wanakaa kimya

Kwa Ushauri wangu
Haya mambo yasichukuliwe kisiasa zaidi but namshauri waziri mkuu akutane na wadau wa kahawa na kuzungumza nao ili kupata njia iliyokuwa bora.
Kwenye korosho iliwezekana ila tukitaka kufanikiwa kwenye kahawa inaitaji umakini mkubwa sana

Mwaka jana TCB walikuja na mfumo mzuri sana wa makampuni kupewa bei elekezi ya kahawa za mitamboni na kahawa za majumbani na walifanikiwa sana kuna haja ya kupaendeleza hapo

Nawasilisha mkulima wa kahawa mbinga
 
WAZIRI MKUU AUVUNJA MFUKO WA WAKFU WA KUENDELEZA KAHAWA

By: Issa Michuzi / Posted: Sunday 14th January 2018

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameuvunja Mfuko wa Wakfu wa Kuendeleza zao la Kahawa (CDTF) na amemuagiza M
dhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
(CAG) kuchunguza mwenendo wa mfuko huo tangu ulipoanzishwa.
Ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Januari 14, 2018) wakati akizungumza na wadau wa zao hilo kwenye kikao cha kujadili maendeleo ya zao la kahawa alichokiitisha, mjini Dodoma.
Waziri Mkuu amechukua hatua hiyo baada ya kubaini kwamba uundwaji wa mfuko huo si wa kisheria bali ni wadau wa zao hilo kwa kushirikiana na Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB).
“Wakati Serikali inapambana kupunguza makato ya hovyo kwa wakulima, kumbe huku kuna chombo cha kuwachukulia fedha wakulima hii haikubaliki.”
Pia aliagiza kufungwa kwa ofisi za CDTF ili kupisha uchunguzi na baada ya CAG kukamilisha uchunguzi na kukabidhi ripoti, kazi zote zilizokuwa zinafanywa na mfuko huo zitafanywa na Bodi ya Kahawa.
Hata hivyo, Waziri Mkuu ameongeza kuwa majukumu ya kuundwa kwa mfuko huo yanaingiliana na yale ya Bodi ya Kahawa, ambayo ni pamoja na kufuatilia maendeleo ya zao hilo, hivyo hakuna haja ya kuwa vyombo viwili vinavyofanya kazi moja.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amepiga marufuku wanunuzi wa kahawa kwenda kununua kwa wanavijiji na badala yake kahawa yote itauzwa kwa njia ya minada.
“Kahawa itauzwa katika minada tu na utaratibu wa kutoa vibali kwa wanunuzi wa kahawa kwenda kununua kwa wananchi vijijini marufuku kuanzia sasa, kama kuna watu wamepeleka fedha zao wazirudishe kwani hazitafanya kazi.”
Amesema Wakuu wa Mikoa na Wilaya wasimamie uuzwaji wa zao hilo na kuwachukulia hatua wote watakaokutwa wananunua kahawa kwa wakulima. “Anayetaka kahawa akanunue mnadani na si kwa wanavijiji lengo ni kuhakikisha mkulima anapata tija.”
Pia ameziagiza halmashauri zote zinazolima kahawa nchini kuanzisha vitalu vya miche ya kahawa na kisha kuigawa bure kwa wakulima, pia Maofiza Kilimo wawaelimishe walkulima wote wenye miti mikongwe waanzisha mashamba mapya.
Kuhusu suala la utafiti wa zao hilo, Waziri Mkuu ameiagiza Wizara ya Kilimo itumie vyuo vyake vya kilimo ianzishe vituo vyake vya utafiti vitakavyofanya kazi ya utafiti wa zao hilo.
 
Wakati huo huo, Waziri Mkuu amepiga marufuku wanunuzi wa kahawa kwenda kununua kwa wanavijiji na badala yake kahawa yote itauzwa kwa njia ya minada.
“Kahawa itauzwa katika minada tu na utaratibu wa kutoa vibali kwa wanunuzi wa kahawa kwenda kununua kwa wananchi vijijini marufuku kuanzia sasa, kama kuna watu wamepeleka fedha zao wazirudishe kwani hazitafanya kazi.”

Kutokana na hicho kipengele makampuni ya kahawa yatapunguza skills person more than 2000 all over tanzania kwasababu hawatakuwa na kazi hili ni jana kwa taifa
 
Back
Top Bottom