Maendeleo yanadhofiswha na kuagiza bidhaa kutoka nje ya nchi

Maendeleo yanadhofiswha na kuagiza bidhaa kutoka nje ya nchi

Umutimbaru

Member
Joined
Jul 22, 2011
Posts
91
Reaction score
5
Maendeleo ya nchi yanatokana wananchi kutumia fulsa zilizopo katika nchi na serikali kutambua fulsa hizo na kuzilinda badala ya kutafuta njia ya mkato kujinufaisha na kunufaisha wachache kwa kupitia wengi.

1. Mfano mdogo zamani kuna wanafunzi waliosoma shule,kwa kununua madaftari, kalamu hata nguo za shule kwa kusokota kamba za kufungia ng'ombe kutokana na katani. Lakini bila kujali fulsa hiyo na kuendelea kuilinda ikaruhusiwa kuagiza kamba za manila ili kuididimiza fulsa hiyo na faida itokanayo na zao la mkonge.

2. Kuna kinamama wantengeneza batiki kwa mikono yao na kuuza kwa bei ya wastani ili kukidhi mahitaji yao na familia, lakini fulsa hiyo haikuonekana.ambapo kungewekwa utaratibu wa kuwalinda akinamama hao, kwa kutokutoa vibali vya kuagiza batiki kutoka nje ya nchi au vazi linalofanana kwa bei wanao ijua wenyewe kuja kuuza sambamba na wale akinamama kwa bei ya chini ili kuua soko lao. Na huyo anaefanya hivyo ni tajiri mmoja anauwa soko la kinamama wengi.

3. Mashamba ya katani yanakufa kutokana mifuko ya plastic kuagizwa kwa wingi toka nje hivyo ajira inapungua.ambapo katani hiyo ingelikwa inatengeneza majunia hapahapa na kuongeza ajira. Pia fedha za kigeni.

Kwanini kusiwe na utaratubu wa kulinda wajasiriamali wake kwa kulinda bidhaa wanazozalisha pia hata kuwahamasisha na kuwadhamini vitendea kazi?
Kwa nini kusiwepo utaratu wa kutokutoa vibali vya kuagiza bidhaa zisizofanana na zile zinazozalishwa na wananchi ili kukomaaza wajasiliamali ?

Kuagiza mwekezaji kuja kulima, Kwani wananchi wameshindwa kulima ?mwekezaji huyo akilima mazao anauza kwa wakati anajua bei imepanda badala ya kupunguza bei ya chakula ana sababisha bei kupanda.

Miaka michache ilopita wakati wa mavuno ukionda sokoni kariako unakuta bei ya mazao imeshuka, laikini hivi sasa hakuna utofauti wa msimu.
Mi nashauri utaratibu wa kulinda bidhaa zinazozalishwa nchini zilindwe na kama kuna ushindani basi uwe wa manufaa kwa nchi sio wa kujinufaisha mtu mmoja
 
Back
Top Bottom