taj mashair
New Member
- Jun 8, 2023
- 3
- 2
Tulikuwa tupo chuoni katika darasa la kozi yetu, kama ilivyo chuoni lazima kuwe na wawakilishi wa darasa"(cr's)ili kuliwakilisha darasa kwenye uongozi wa chuo lakini katika uongozi wao hawa wawakilishi hawakuwa na utawala mzuri ambao haukupendezwa na wana darasa wengi kwani hawakufanya vitu kwaajili ya maslahi ya wengi kwa darasa bali walifanya kwa maslahi yao zaidi ili kuimarisha maslahi ya viongozi wa juu na uhusiano wao tu na sana hufanya vitu kwa maamuzi yao bila kushirikisha wana darasa na kupelekea kutopendezwa na hawa wawakilishi.
Na katika darasa letu walikuwepo wanadarasa wachapakazi mno na wenye kuwajibika japo hawakuwa viongozi kwa maslahi ya wenzao lakini pia hawa wawakilishi hata kuchaguliwa kwao hakukuzingatiwa vigezo vyovyote labda iwe kuwahi chuoni wakati masomo yalipoanza.
Maisha ya chuo yaliendelea, hadi zikafika siku za kuchukua fomu za kuwania nafasi za ubunge, na katika kozi yetu alichukua fomu huyu mwakilishi wa darasa wa kiume na mwanadasara mmoja mchapakazi sana ambaye hakuwa mwakilishi wa darasa"(cr)" lakini alipendwa sana na wana darasa na kupendwa kwake kulitokana na uchapakazi na kuwajibika katika baadhi ya kazi za darasa kwa ujumla na kujitolea kwa ajili ya wengine kwani alithubutu kukusanya barua za kazi kwa vitendo"(za field)" za wanadarasa wengi na kwenda kuwaombea nafasi hizo katika taasisi na kampuni mbalimbali.
Katika kuomba kura ukweli ulijidhihirisha kwa yule mwakilishi wa darasa hakukubaliwa na wanadarasa kwani hata sera zake zilipuuzwa na wakamuona hana cha maana alichokifanya katika utawala wake, na kwa upande mwingine yule mgombea mwenza alikubalika bila hata ya kupigwa na walio wengi maana mtu sahihi anaonekana kwa matendo yake kwa wengine .
Basi kura zilipopigwa, mwakilishi wa darasa alishindwa na mgombea mwenza akapata ubunge kutokana na kujitoa kwa wengine na kuwajibika kwa wengine na akawa mbunge wa kozi yake katika serikali ya wanafunzi wa chuo hicho.

Upvote
1