Maeneo hatarishi Kwa Ajali Dar

PAGAMECO

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2016
Posts
1,206
Reaction score
1,237
Habari Zenu Wana Jamvi Kwa Hapa Dar Kuna Baadhi ya Maeneo yani Mwezi hauwezi Ukapta haujashuhudia Ajali yaweza Kuwa Kwa Uzembe Au Emergency

Mojawapo Ni hili la Kuanzia Kiluvya Gogoni Pale Kuna Mteremko wa Kawaida But Madereva Huwa Wanapuuzia haswa Madereva wa Malori

Sehemu ya Pili" Ni kibamba Chama Mpaka Pale Kibamba Kwa Mangi Madereva Wengi hujikuta Wako Kichwa Chini Miguu Juu

Waweza Share Maeneo Mengine hatarishi Kwa Vyombo Vya Usafiri na watembea kwa Miguu unayoyafahamu kwa Hapa Dar

"Updates"
Mida hii ya saa 11 Asubuhi Nimepita hpa Kibamba Chama Kwenye mteremko Kwenda Kibamba kwa Mangi Kuna Roli lipo mtaroni Mida hii

Madereva Tuwe Makini[emoji53][emoji53]
 
mbeya kuna sehemu inaitwa 'MBEMBELA! baada ya mteremko wa meta hospitali pale! balaaa! kuna mteremko mmoja safi sanaaa, lakini kabla hujakaa vizuri unajikuta nymbani kwa mtu! (nimetoka mbeya miaka 12 imepita sijajua kama wameparekebisha)
 
mbeya kuna sehemu inaitwa 'MBEMBELA! baada ya mteremko wa meta hospitali pale! balaaa! kuna mteremko mmoja safi sanaaa, lakini kabla hujakaa vizuri unajikuta nymbani kwa mtu! (nimetoka mbeya miaka 12 imepita sijajua kama wameparekebisha)
[emoji3] [emoji3] [emoji3]

@m G00d Br0ther
 
Nilivosoma tu heading nikataka nikuambie gesti, lakn baada ya kusoma content ya uzi jibu nikwamba sijui
 
kwa walevi pale kona ya Aga khan kama unatokea surrender kwa usiku ni pabaya sana na hile kona ya collesium kama unatokea st peters ni hatari sana kwa usiku n then umepiga maji
 
mataa ya chang'ombe pale umeme ukiwa hakuna ukienda kichwa kichwa unakuwa breki za malori yanayotoka bandari
Wanapaita machinjioni hapo,hatari sana.
Pia hata pale mataa uhasibu napo panachinja sana.
 
-Njia panda ya kawe ukiwa unatokea kawe na kuingia kulia kuelekea mbezi beachh mmmh hasa kama hakuna taa;
-ukiwa unatoka kituo cha daladala airport kuelekea banana hapa kabla ya kuvuka barabara inayotoka airport terminal one kuja mjini wengi hawajui nani mwenye kipaumbele, mwenye kipaumbele ni yule anaetoka terminal one wewe wa kwenda gongolamboto subiri alafu kuna maua na miti inazuia kuona anaekuja kutoka terminal one noma.
-Kilima cha mombasa kuja banana oooooohhhh pale hatari hasa ukiwa unashuka, zimegawika njia tatu katika ile barabara sasa wengi hawajui kuhusu muda upi nani atumie njia mbili nani atumie moja either kwenda mjini au wa kwenda gongo la mboto vifo pale balaa.
-Uwanja wa taifa gari zinatoka uhasibu kuja tazara na za kutoka duce kuingia mandela road ayaaaa hatari sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…