Maeneo mengi inayopita SGR hayana network nzuri ya simu, Je makampuni ya simu hayaoni pesa hii inayopotea?

Maeneo mengi inayopita SGR hayana network nzuri ya simu, Je makampuni ya simu hayaoni pesa hii inayopotea?

Braza Kede

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2012
Posts
3,840
Reaction score
6,844
Hii ni ajabu na kweli ukisafiri na treni ya SGR utakuta maeneo mengi inapopita hiyo treni hayana network nzuri ya simu.

Je makampuni ya simu hayaoni kama wanapoteza fursa ya kupiga pesa? Hawaoni pesa mingi inayopotea hapa au ndo wameshashiba na kuvimbewa hawataki pesa tena?
 
Ukafunge mnara eneo ambalo ndani ya masaa 24 inawezekana ni watu takribani 20 ndio wame connect kwenye base station tena chini ya dakika 3, hiyo itakuwa ni akili au matope? Kiufupi ni kuwa gharama za uendeshaji zitakuwa kubwa kuliko faida kwa kampuni
 
Hakuna nchi duniani inafanya hivyo.

Mitandao hupeleka towers pale ambapo kuna wateja tayari
 
Kwaiyo wakasimike minara ya Network kisa Treni inayopita mara mbili kwa siku...ungesema kwenye station kubwa au vijiji vilivo karibu na njia ya treni viwe na network.
 
Akili za mtoa mada bhana 😂 kwan hy treni inapita hilo eneo kwa muda gani? Kwamba treni inatumia saa 24 kupita hilo eneo?
 
Treni zikianza kupita kila baada ya dk 5 wataweka wala usijali.
 
Hakuna uwezekano kukawa na "mobile tower" kwa maana ya kwamba hiyo tower ikawa installed kwenye treni ili wasafiri wawe na mtandao throughout the journey?
 
Akili za mtoa mada bhana 😂 kwan hy treni inapita hilo eneo kwa muda gani? Kwamba treni inatumia saa 24 kupita hilo eneo?
Halafu yeye anajiona katoa Bonge la Uzi na point kumbe Nonsensical.....
 
Hii ni ajabu na kweli ukisafiri na treni ya SGR utakuta maeneo mengi inapopita hiyo treni hayana network nzuri ya simu.

Je makampuni ya simu hayaoni kama wanapoteza fursa ya kupiga pesa? Hawaoni pesa mingi inayopotea hapa au ndo wameshashiba na kuvimbewa hawataki pesa tena?
Hailipiii wala make business sense.....wazo mfu hilo unapita tu hukai kila kituo...gharama kuweka mnara zitajilipaje ? Rather ukubali boasterkila mtandao ndani train....labda !!!!
 
Ila kadogosa ameshindwa kuweka wi fi kwenye Station za sgr, kama ya morogoro haina network hata ya kupiga simu hazitoki
 
Hakuna uwezekano kukawa na "mobile tower" kwa maana ya kwamba hiyo tower ikawa installed kwenye treni ili wasafiri wawe na mtandao throughout the journey?
Ni kiasi cha TRC kuingia makubaliano na makampuni ya simu ili zifungwe wireless network kwenye station zote ili wateja wenye vifaa vya kielektroniki waunganishwe kwenye mtandao wawapo safarini.
Treni zote kwa makubaliano na mitandao ya simu zifungwe antena zenye uwezo wa kupokea mawimbi kutoka ilipo minara ya simu.
Kiufundi Reli Tanesco na makampuni ya simu wakishirikiana kibiashara, wanaweza kuja na huduma moja bora tena ya mfano.
 
Back
Top Bottom