Maeneo rafiki kwa biashara ya tigo pesa

floow

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2017
Posts
411
Reaction score
855
Habar wakuu
Wiki 3 zilizopita nimeweza kufungua biashara ya miamala ya pesa (tigo pesa&m pesa) matarajio yangu ni angalau kwa mwez iniingizie si chini ya 50,0000 kwa mwezi

Kabla ya kumuweka mtu Wa kumuajili
Nimeamua nikae mwenyewe ili kuangalia upepo Wa mazingira na jinsi miamala inavyo fanyika..

Miamala haiend ,kwa wiki 3 nilizokaa nimegundua nafanya miamala ya Tigo inayo niingizia 4000 kwa siku na miamala ya VODA inayo niingizia 2500 kwa siku...
Mtaji nilioweka ni mil 1:5 lakini kwa wiki 3 nilizo kaa naona pesa inayo zunguka ni lak 3 pekee

Naombeni mnishauli juu ya hii sehemu ya biashara ,,
Nihame mapema ili nitafute sehemu nyingine au nivumilie kidogo

NB Ofisi inahamishika ,sijapanga frame...nime weka BANDA ..
 
External mkuu
Ok, bado ni mapema sana kusema hiyo sehemu sio nzuri coz ndio kwanza umeanza biashara na hauna jina kivile.
Alafu mimi nilikuwa naona hii biashara ukiifanyia kwenye fremu ndio vizur zaidi kwasababu wateja wengi wanaamini watu wa vibandani awana mitaji mikubwa na pia usalama wake unakuwa mdogo.
 
Hii biashara kwa sasa imekua haina issue aisee,me mwenyewe nimeifanya na sehemu niliyoweka ni stand ya daladala ila hiyo commission inayokuja dah inakatisha tamaa,ila kuna mtu alinishauri sehemu nzuri ni za masokoni,ambako kuna movement kubwa ya watu
 
mtaji ni mdogo, katafute eneo mabibo hostel au mabibo sokoni pia pendelea eneo linalofanya miamala midogo midogo sana ndo inafaida, ongeza huduma za kibenk na vifurushi vya kupiga na mb ili wateja wawe na uhitaji wa lazima kuja kwako
 
Dah me pia ninayo hiyo biashara ila nampango mwaka huu nihamie dar sasa ndio nawaza niwapi nitapata sehemu nzuri ambayo itakuwa namzunguko mzuri ambayo itanifanya niishii vzr
 
Dah me pia ninayo hiyo biashara ila nampango mwaka huu nihamie dar sasa ndio nawaza niwapi nitapata sehemu nzuri ambayo itakuwa namzunguko mzuri ambayo itanifanya niishii vzr
Mimi kaka yako, naifanya hii biashara, njoo huku dar mdogo wangu
 
Mimi kaka yako, naifanya hii biashara, njoo huku dar mdogo wangu
Mpaka nikiwa nauhakika waeneo lakazi napakuishi kabisa maana huku mkoani mzunguko wapesa kwahii biashara yangu nimdogo sana
 
Ushaur mzuri sana katoa Dividend lakin kuongezea hapo kama ukitafuta frem hakikisha mtaji unaongeza kidogo..

Ila kama ndio unaanza maeneo ya masoko ndio mazuri hautaji frem... Na miamala midogo midogo itakuwa mingi...

All the best jamaa..
 
Sawa dogo, Pambana
Ujue nini kaka me nataka nikifika huko nipange naroom kabisa sitaki kufikia home so ninachotaka nipate sehemu yakufanyia biashara kwanza kama utakuwa tayari kunisaidia kupata itakuwa vizuri sana
 
mtaji ni mdogo, katafute eneo mabibo hostel au mabibo sokoni pia pendelea eneo linalofanya miamala midogo midogo sana ndo inafaida, ongeza huduma za kibenk na vifurushi vya kupiga na mb ili wateja wawe na uhitaji wa lazima kuja kwako
mtaj kama uo unaweza fanya miamala ya kibenk kwer?
 
Ujue nini kaka me nataka nikifika huko nipange naroom kabisa sitaki kufikia home so ninachotaka nipate sehemu yakufanyia biashara kwanza kama utakuwa tayari kunisaidia kupata itakuwa vizuri sana
Kwani upo mkoa gani !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…