A
Anonymous
Guest
Kuna tabia ya baadhi ya watu kuvamia maeneo ya wazi au barabarani wakifungua biashara na mwishowe wakishindwa kuendelea na biashara ndogondogo hupangisha maeneo hayo kwa kuchukua kodi kila mwezi
Pia tabia hii imeonekana hata kwenye masoko makubwa pale watu wanawahi kuchukua sehemu za biashara halafu wanazipangisha kwa kodi ya juu kwa watu wengine(sublease).
Hii si sawa kwani baadhi ya maeneo ni ya wazi yamekuwa yakichafuliwa sana pia maeneo kama stendi za mabasi yamekuwa kero sana, biashara zimekuwa zikipangwa kwa kutumia meza sehemu za barabarani na hii ni hatari sana.
Pia sehemu hizo zimekuwa zikitumika kama parking za magari ambayo sio sawa kabisa.