Maeneo ya biashara Mwanza

Financial Analyst

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2017
Posts
1,849
Reaction score
3,506
Habari wakuu,

Nina plan ya kufungua duka lenye mchanganyiko wa bidhaa za umeme na ujenzi. (electrical and hardware)

Ila ndio naanza hii biashara , sipo established kivile, naanza kama mid sized shop, so mdogo mdogo tu.

Najua city centre sitapaweza kutokana na Competition ya hali ya juu na kodi za fremu kuwa kubwa.

So ni maeneo yapi pembezoni mwa city centre au nje ya mji, ambapo pame changaamka na patafaa duka langu la electrical na vifaa vya ujenzi.

Nitashukuru kwa michango yenu.
 
Nenda Buzuruga au Pasiansi mwingiliano ni mkubwa. Ila kama una uwezo fanya city center penyewe sababu kodi itamezwa na faida.
 
Buhongwa kuna centre kubwa tu ya biashara. Na watu ni wengi haswaa
 
Maeneo ambayo bado watu wanajenga yatakua mazuri sana kwa hiyo kitu.
Onyo usije ukafungua mabatini, masikini ni wengi sana. Labda uuze uji na karanga za mia mia.
Dah kweli usilolijua ni usiku wa giza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…