RESOLVED KERO Maeneo ya Stendi ya Mbezi Malamba, Darajani, korido la jengo la Abiria na Gereji (Stendi ya Magufuli) kunanuka mikojo

Imefanyiwa kazi au kupatiwa ufumbuzi na Mamlaka husika
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
Mbezi Stendi ya Malamba, Darajani, jengo la Abiria Stendi ya Magufuli na Gereji yake kunanuka mikojo

Nimepita Mbezi Luis maarufu kwa jina la Mbezi Mwisho, nikitokea Kinyerezi, nimeshuka Stendi ya chini maarufu kama Stendi ya Maramba nikapandisha ngazi kuelekea Stendi ya Daladala, maeneo mengi pale yananuka mkojo, tena mkojo uliovunda, najiuliza hapo stendi hakuna uongozi, hakuna mamlaka? Hawasikii harufu?

Kinachosikitisha ni kuwa kwa wale wauza vyakula nako hali iko hivyohivyo na biashara zinaendelea kama kawaida, hivi kwa nini watu wanalazimisha kutokea kwa magonjwa ya mlipuko, wapiga debe na machinga wanashindana kukojoa ovyo mitaroni, kwenye kuta za vibanda na kwenye chupa na kutupa bila mpangilio.

Nikaendelea na safari yangu kupandisha Daraja la kuelekea Stendi ya Magufuli, ama hakika ukistaajabu ya Firauni utayaona ya Mbezi na mikojo kila kona, Daraja linanuka mkojo kuanzia mwanzo mpaka mwisho, kwenye kona zake zinaonekana ndiko hukojolewa zaidi, nilikuta mkojo ukiwa bado mbichi ukutani licha ya kuwa mchana kweupe, Mbezi ya mikojo! Hivi hakuna vyoo vya umma Mbezi?

Nikiwa nimeshikwa ghadhabu kwa nini haya, nikaendelea mbele, huku nikisikia harufu ya mkojo, nikafika Magufuli Stendi, nikawa napandisha ghorofa kwenye jengo maarufu kama jengo la abiria, ile korido ya kupandia nayo kulikuwa na chupa ya mkojo chini, Aisee Mbezi na mkojo ni kama pafyumu.

Nikashuka, nikaelekezwa niende kule stendi upande wa chini maarufu kama Gereji, huko ndo fainali, unapokelewa na harufu kali ya mkojo ni kama wamepewa pafyumu ya mkojo wakaipuliza, ni mkojo kila kona, kule kwenye mabasi ni mikojo mitupu! Nikauliza mmoja ya waliokuwepo hapo, hivi huku hakuna vyoo, nikajibiwa vipo kule chini kabisa ila havieleweki ndiyo maana watu huchagua kukojoa nyuma ya magari.

Stendi nzuri ya Magufuli inapambwa na harufu ya mkojo, kipi tutakipata tuweze kukitunza vyama? Ama hakika Mbezi inapambwa kwa harufu ya mkojo.
 
Tanzania kila mahali kunanuka mkojo.
 
Stendi hiyo ni chafu sana.kila sehemu kunanuka mkojo na mavi ya chalamila.Ni bora tu warudisha utaratibu wa mwanzo wa kila basi kuwa na stendi yake.Maana stendi ya umma imewashinda kuisimamia.
 
Na mbaya zaidi mnawaona wanao kojoa maeneo hayo halafu mnawachekea.
Chukueni hatu, msisubirie kila kitu askari afanye,
 
Mji wa Dar ni mchafu in Samia's words.
 
Dar ustaarabu hamna, viongozi wamejisahau sana, harufu mbaya kila kona haswa huko mjini.

mitaro wameshindwa hata kuweka magari ya majitaka yawe yanafyonza ule uchafu na kuutupia mbali.
Ili jij likubalike na wageni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…