Vien
JF-Expert Member
- Mar 6, 2020
- 6,585
- 10,363
Mafanikio yanabebwa na kila jitihada zozote za kuongeza thamani (branding) ya kitu au mtu. Ukiwa kama kijana mwenye ndoto za kuyafikia mafanikio unapaswa kuhakikisha una ongeza thamani kwa kila utakachokifanya.
Tukianza na vitu vya kawaida kabisa, mfumo wa maisha ya kila siku uvaaji, ulaji, maeneo unayopenda kuzunguka haya yote yataamua uwe kwenye kundi lipi katika jitihada zako za kuyatafuta mafanikio.
Muonekano wako, unaweza ukakupa fursa au ukakunyima fursa, Ukiwa kama kijana jiongezee thamani kwa kuhakikisha mavazi yako ni nadhifu na yaheshima.
Watu wengi wanasisitiza ili ufanikiwe unapaswa ufanye kazi kwa bidii sana. Lakini mimi nashauri katika hizo bidii zako hakikisha umeongeza thamani kwenye kitu au vitu unavyovifanya.
Ukiwa kazini umeajiriwa , ili uweze kuongezewa mshahara, ni mpaka uongeze thamani, Thamani utaiongeza kwa kuja na mawazo mapya ili kuweza kuongeza faida nyingi zaidi.
Ukiwa kwenye biashara yako, ili uweze kuwa na wateja wa kudumu lazima uweze kuongeza thamani kwenye biashara yako, hapa unaweza kuongeza thamani kwa kuwa lugha nzuri kwa wateja wako, kuwa na bidhaa zenye ubora, mpangilio mzuri na kadhalika.
Ukija kwenye mahusiano , uwe mwanaume au mwanamke, ili mahusiano yenu yaendelee kudumu lazima uyaongezee thamani msiwe watu wale wale kila siku.
Kuongeza thamani (Branding) ndo imefanya ngozi nyeupe zituache mbali sana kwene mafanikio , Angalia wanavyo fanya branding kwenye product zao, Angalia walivyo wepesi kubadilika kutokana na muda, Angalia wanavyo thamini na kutunza vitu vyao. Hivi vyote ni katika kuongeza thamani.
Sio kwamba wanatumia maarifa makubwa sana hapana ni Uwezo wa kuongeza na ku maintain thamani kwa kila wanachokifanya.
Wajanja walioijua hii siri ya mafanikio wanatumia mwanya huo kujitajirisha kwa haraka Niwape mfano rahisi kabisa haya makampuni ya construction, au supply & delivery.
Kwenye kampuni za construction huwa wanatumiaga hawa mafundi wetu wa kawaida kabisa kufanya nao project kubwa tuu zinazowaingizia fedha nyingi tu.
Ila kwavile mafundi wetu hawajiongezi wamezoea wao kuitwa kufanyishwa kazi kwa siku nzima labda anapata 30000 kama labor charge lakini mwenzake mwenye kampuni anaweza akaingizia hadi 200000 kama labor charges tuu na hapo aliyefanya kazi ni fundi ila anayepata fedha zaidi ni mwenye kampuni.
Ila hiyo anaipata kwavile tayari kashaongeza thamani kwa kusajili kampuni, kulipa kodi n.k
Vijana tusikubali kubaki hivi hivi kila siku, tuamke tujiongezee thamani tutayaona mafanikio.
Stay positive