Mafanikio: Jinsi ya Kubadili tabia na Mtindo wa Maisha ili kufanikiwa katika biashara

Mafanikio: Jinsi ya Kubadili tabia na Mtindo wa Maisha ili kufanikiwa katika biashara

Masokotz

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
3,713
Reaction score
6,121
Tabia ni nini:Tabia ni mambo au matendo ya kimazoea ambayo unaweza kuyafanya au kutokuyafanya bila kutafakari,kuhofia au kujali matokeo yake.Ni utaratibu uliozoeleka na kukubalika kwa mtu mwenyewe kutokana na mazoea aliyojijengea.Tabia inaweza kuwa nzuri au mbaya katika muktadha fulani na inaweza kuwa ni matokeo ya mazingira unayoishi,malezi,utamaduni au mfumo mzima wa kijamii.

Tabia inajengwa kwa marudio ya mara kwa mara ya jambo fulani ambalo linajenga hisia fulani ndani ya mtu ambayo inadumu kwa muda mrefu.Hisia hio huathiri mfumo wa kifikra na ufanyaji wa maamuzi.Hili nalo linaweza kuathiri kiwango cha mafanikio.Moja kati ya njia inayotumika katika kujenga tabia ni mfumo wa ZAWADI na ADHABU(REWARD AND PUNISHMENT) ambao ni moja kati mfumo unaotumika katika malezi.

Changamoto inayojitokeza katika mfumo ni pale ambapo kuna kuwa na adhabu lakini hakuna zawadi,yaani unapoonesha tabia Mbaya unapewa adhabu ili ukionesha TABIA NJEMA HUPEWI ZAWADI.Mfumo huu wa kutokuwa na zawadi unaathari kubwa sana katika mfumo wa kujiamini kujituma na hata kuweka bidii.Ndio maana wanafunzi wanaokuwa shuleni wanapopewa zawadi pale wanapofanya vizuri hujikuta wakiongeza bidii na kujikuta wakiendelea kushikilia alama za juu huku wale ambao hawapewi zawadi wakiendelea kuwa chini na kuamini kwamba wao wako nyuma.Kiuhalisia kufanya vizuri katika masomo na matokeo ya bidii,hivyo mwenye bidii zaidi ndio hufanya vyema

Leo nataka nizungumzie namna ya kubadili tabia yako ili uweze kujijenga kama mjasiriamali na uweze kufanikiwa.

Kama mjasiriamali unatakiwa ufahamu kwamba kila ulicho nacho ni sehemu ya mtaji wako,kuanzia PESA yako,Muda wako,Elimu/Ujuzi wako vyote hivyo ni sehemu ya mtaji na ni lazima uwe na namna bora ya kuvitumia ili kufikia malengo yako.Tabia yako inaweza kuathiri matumizi yako ya muda,pesa na hata ujuzi wako.Tabia yako katika kutumia pesa inaweza kukufanya ushindwe kufikia malengo yako.Hivyo basi ni muhimu sana utambue zile tabia ambazo zina kuathiri vibaya na uchukue hatua kuzibadilisha.

Katika safari ya kubadilisha tabia,mambo ya kuzingatia ni kuitambua tabia husika na madhara yake na kuchukua hatua mahususi kuibadilisha tabia hio.

Kwenye kutambua Tabia yako inakuathirije,jaribu kuandika matukio yote katika siku yako kwa mfululizo wa siku tano.Kuanzia unapoamka mpaka unapolala.Unapoyandika unaweza kuweka na muda uliotumia kufanya tukio fulani kama SHAJARA/DIARY.Baada ya hapo jaribu kuyaangalia matukio yote unayofanya na uyaweke katika matukio ambayo unaona yana faida kwako na yale ambayo unaona hayana faida kwako,kisha uangalie pia yale yanayojirudia kila siku ,na yale ambayo unatumia muda mwingi kuyafanya,yale ambayo unatumia pesa kuyafanya,yale ambayo baada ya kuyafanya unajisikia vibaya,yale ambayo yanakufanya utamani kuyaacha hata bila kuambiwa.

Kwa kawaida ujenzi wa tabia mpya hutumia takribani siku 30.yaani kama unafanya jambo fulani kwa kulirudia rudia kwa muda wa siku 30 mfululizo basi linaweza kugeuka na kuwa tabia kwa sababu ya mazoe.Na hii ni kwa mambo yote yale yaani tabia mbaya na hata tabia njema.

Kama mjasiriamali kuna tabia ambazo unapswa kuzizoe ikiwamo,Muda wa kuamka,Kujifunza/kujisomea,kubana matumizi na bajeti.

Ili kuzijenga tabia hizo unapaswa kuanza taratibu kwa kuanza na mazoezi madogo madogo ambayo yanakuwezesha wewe kuzoea tabia fulani.
Tengeneza ratiba yako ya asubuhi-

Kama mjasiriamali unayetaka kukua hakikisha unaamka mapema sana,mfano saa 11 alfajiri ambao ni muda mzuri.Ukiamka unaweza kufanya ibada kidogo na kisha kupitia shughuli zako za siku hio na pia kupanga shughuli nyingine kulingana na mipango yako.Ni muhimu sana kuhakikisha kuwa unakuwa na ratiba fulani ya shughuli zako za siku,na muda wowote wa ziada uutumie kwa ajili ya kujisomea na kujifunza vitu vipya.

Jambo jingine la kufanya asubuhi na mapema unapoamka ni kutafakari kuhusu malengo yako kimaisha na mipango.Asubuhi ni wakati mzuri wa kutafakari big picture ya maisha yako na ambayo inakuwezesha kupata hamasa ya kufanya kazi kwa bidii

Matukio haya ya asubuhi hakikisha unayafanya kwa angalau dakika 60 ili inapofika saa 12 alfajir unaanza kuiishi ratiba yako.

Jambo la msingi ambalo unatakiwa ufahamu ni kwamba ukifanya zoezi hili kwa siku 30 nakulizoea litakuwa tabia na halitakupa shida katika kulitekeleza.Kumbuka ili uweze kuwa na siku njema hakikisha unaanza na ausbuhi njema.

Itaendelea
 
Hii ni kitu nzuri sana

Hii mada unaweza kuisoma kwa pamoja na hadithi ya ndege tai
Ila nikupe pole mleta mada, yaani viewers na comments hazitazidi zile za uzi wa 'kula tunda kimasihara' IPO kule jukwaa la mahusiano.

Hivi vitu ndio vinatofautisha sana mjasiriamali na mchuuzi
Aghalabu huwapembua wenye 'akili' na wale wenye 'degree 4'

Kwa kawaida, kadri unavyoipa akili yako 'new feeds' haswa valuable ones utaona tu trending inabadilika not necessarily materially rather cognitively na atitude as well
 
Back
Top Bottom