Mafanikio na Maanguko kimapenzi 2009, Nini tufanye 2010?

Sipo

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2008
Posts
2,139
Reaction score
95
Umefanikiwa lipi kimapenzi, kimahusiano na kirafiki kwa mwaka 2009?
Changamoto gani umezipata katika mapenzi, mahusiano na urafiki 2009?

Nini tufanye kwenye nyanja hizi za mapenzi, mahusiano na urafiki 2010?

Ni mada kwa kila mtu aliyeoa/olewa na wale ambao hawajaoa/olewa.

Naamini kubadilika ni kujifunza

NB
Nawatakia KRISMASI NJEMA PAMOJA NA MWAKA MPYA 2010. NAAMINI PIA KUWA WOTE TUTAKUWEPO JAMVINI HAPO MWAKANI. MUNGU NI MWEMA
 
hata kama umepigwa chini wewe sema tu ni sehemu ya anguko
 
Mambo Sipo! Sijakusikia muda sasa. Hapo nilipokoleza waswahili wanaweza kutafakari vinginevyo! Si unajua tungo tata ili kupunguza ukali wa maneno? Kwangu 09, ilikuwa mswano tu, labda NGULI ndiye alikuwa hakosi kwenye vikao!!!
 
Huu mwaka Mungu kanikaramia mema mengi sana,japo kushiriki kwenye maharusi ya watu kumenirudisha nyuma kimaendeleo ila naamini hizo ndoa zilizo toboa mifuko yangu zitadumu milele/till death assume its place.
 
Mkuu Kyachakiche nipo mkubwa mihangaiko tu. Hongera sana Mpwa kama wewe ghadhabu ya mapenzi haijakukumba mwaka huu. Kuna watu hawajitokezi hapa, sasa nashindwa kuelewa kwao mahusiano mwaka huu yalikuwaje. Pia nashukuru kwa kunisahihisha, i noted it with thanks Sir
 
Huu mwaka Mungu kanikaramia mema mengi sana,japo kushiriki kwenye maharusi ya watu kumenirudisha nyuma kimaendeleo ila naamini hizo ndoa zilizo toboa mifuko yangu zitadumu milele/till death assume its place.
Mkuu si ulikuwa unawekeza? Uliyempa kilo wewe atakupa kilo mbili mwakani, au vipi? Tatizo ni kwetu tuliokuwa tunachangiwa crate moja ya safari au plisner sasa tunarudisha kilo!!
 
Mpwa hongera sana kwanza kwa kumshukuru MUNGU alikuwezesha kwa mengi. Hayo mengine ya michango mimi napenda kuyaita crossing issues kwenye maisha. Hongera Nguli
 
Mkuu si ulikuwa unawekeza? Uliyempa kilo wewe atakupa kilo mbili mwakani, au vipi? Tatizo ni kwetu tuliokuwa tunachangiwa crate moja ya safari au plisner sasa tunarudisha kilo!!
Mpwa Kya
huyu jamaa yetu Nguli kashaoa sasa uko kuwekeza sijui kwaajili ya wanaze au nduguze? Manaze kama ni kwasababu ya wanae basi ipo kazi.

Umenichekesha sana hapo nilipohighlight Mkuu
 
Mpwa usicheke, mtu alikuwa anasimama anaongea saana, kwamba bwana harusi mtarajiwa ni rafiki yangu, tena ni ndugu yangu wa karibu, lake langu langu lake, kwa kweli niko naye bega kwa bega, hivyo basi, kwa kuzingatia hayo yote, naahidi crate moja ya double cola na kazi yoyote ngumu!
 
Mi namshukuru Mungu kwa kutunukiwa Penzi!
Mpwa hauishi kutunukiwa penzi kila kuchapo?
Pendekezo mwakani husitunukiwe tena, yanatosha haya matunukio. Mwe

Naona Fidel80 ameamua kuipotezea thread hii
 
Mwenzenu 2009 imekuwa mbaya sana kwangu,nimeachika mara mbili na kosa ckuwahi kuambiwa
 
..... Mwaka huu 2009 umekuwa ni mwaka wa neema na mafanikio, I hope 2010 utakuwa ni mwaka mzuri pia.
 
Mwenzenu 2009 imekuwa mbaya sana kwangu,nimeachika mara mbili na kosa ckuwahi kuambiwa
Pole sana mgeni kwa kuachika mara mbili ndani ya mwaka mmoja. Unaweza kutupa story ya kuachika kwako japo moja ili wadau wakupe ushauri mwanana yasikupate tena mwaka 2010.

by the way angalia pia na jina lako 'mungiki2' linaweza kuwa sababu ya kuachika. Ukileta story yako uweke kabisa na jinsia yako kwani unaweza kupata wa kukufariji wakati huu wa krismasi
 
Back
Top Bottom