Mafanikio ni Gharama

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2011
Posts
7,872
Reaction score
9,263
Ni ukweli usio pingika kwamba Mafanikio yana gharama zake, na ukijaribu kusoma baadhi ya story za watu walio fanikiwa utagundua kwamba wengi waligharamika kwa namna moja au nyingine, ni vigumu sana kupata mafanikio bila kuyagharamikia, yaani yaje tu kama mnvua,

Ili ufanikiwe kuna gharama zake, ni vigumu sana kufanikiwa bila kuingia gharama. Tanzania kuna watu mbali mbali wanapambana kuweza kufanikiwa kimaisha hasa kwenye nyanja ya Biashara, na watu wamekuwa wakitumia mbinu mbali mbali kuweza kufikia mafanikio hayo.

Kuna watu wamefanikiwa/walifanikiwa baada ya kuingia gharama ikiwemo kwenda shule au kuajiri watu wawasaidie katika kutimiza ndoto zao, watu wameweza kuwatumia hadi maconsultance, na watalaamu mbali mbali na kuwalipa pesa nyingi sana.

Na kuna watu hutaka kufanikiwa bila gharama hawa wanataka kila kitu bure, wanataka consulatance awape ushauri bure wanataka wataalamu waje wawape ushauri free of charge, inawezekana ila ukweli unabakia kwamba unacho kigharamikia unakuwa na uchungu nacho sana.

Chukulima mfano Mashirika kibao yaliyo jaa vijijini kuondoa umasikini, Sijui kama kuna mtu alisha wahi kujiuliza ni kwa nini umasikini haupungui pamoja na kuwepo mashirika mengi yenye miradi ya kufa mtu, Utakuta shirika linatoa mafunzo halafu wanao fundishwa wanataka walipe kwanza ndo wahudhurie mafunzo kwa staili hii hata umasikini hautaisha kamwe.

Niliwahi kuandaa semina ya bure kuelimisha watu ila watu waligoma kwa sababu hakuna malipo, yaani walitaka niwalipe n then niwafundishe.

Mara nyingi nimekuwa nafanya safari zangu nchini Kenya, kwenda kujifunza na kwa kweli Kenya hawana biashara za bure kama huku, mashirika kule yanatoa service ila ni lazima ulipie au uchangie, Kule hata ukitaka kwenda kutembelea mtu mwenye project yake ni lazima umulipe, mtu hawezi kukupatia ushauru bure,

Hivyo Basi ni vizuri na sisi tubadilike, mtu kaandaa kitabu chake kinacho elimisha mambo fulani, kinunue kilipie, na si utake upewe bure, unataka kwenda kujifunza kwa mtu aliye fanikiwa katika ishu fulani basi lipia inapendeza sana na unakuwa na uchungu na hicho ulicho jifunza,

Tujaribu kuwekeza kwenye utafiti na mafunzo, hata kama elimu inapatikana Nchi nyingine ifungie safari ukajifunze, wenzetu wameweza kufanikiwa kwa sababu wana uchungu na yale wanayo jifunza kwa sababu hakuna cha bure wanaya gharamikia 100%
 
Hongera xana heshimowa Chacha nd nitakpokuwa nasafiri kwenda dar napanga kufanya stop over nd visit your farm nd natumaini kuna mengi ya kujifunza toka kwako
 
Ni kweli kabisa mkuu Chasha Poultry Farm. Ukimuona mtu anabeza huduma ya kitaalam inayohitaji kuchangia ili upate kunufaika basi ujue kabisa hana nia ya dhati kujifunza maarifa hayo.
Watu kama hao aghalabu huwa nawapotezea.
Nikija R ntakutembelea hakika kuna kitu ntatokanacho hapo kwako.
 
Last edited by a moderator:

Karibu Sana Mkuu,
 
Nikweli kabisa, ata wakulima wengi wame kuwa wakipata mazao duni kwa sababu za kuto wafuata wataalamu waje kuwa fanyia audit ya mashamba yao pind yanapo kuwa na mazao, hiki mm huwa nakiita kilimo cha mazoea.

Penda kugalamikia kituchako ili kiwe na thamani flani mwisho wasiku ata product yako ita kuwa more valuable in the market.

Bwana chasha nami napenda kuja kutembelea poutry farm yako ninge penda unipe contact zako ili niweze kukupata, kwa mafunzo zaidi + gharama.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Kwa Tanzania elimu inahitajika tena waajiliwa wengi ndio wanahizo habari za kutaka kulipwa kila kikao wakati faida kuu ni kwao,tuamke na tuache kusikia tetesi tu za mtahani eti mtu ameuza karanga mpaka sasa anamaisha poa,kaa ufahamu ugumu aliokumbana nao ndio utafahamu unafanyaje
 
Ukweli mtupu tena waeleze kaka kwani wana_jamii wanapenda bure lkn wanasahau kuwa bila malipo hawezi kufanikiwa kwani hatakuwa NA uchungu nacho &ataweza kuwa jasiri katika shughuli zake zote...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…