Gwappo Mwakatobe
JF-Expert Member
- Nov 22, 2019
- 1,730
- 2,230
1. UTANGULIZI
Ifuatayo ni simulizi yangu ya kweli na majina yaliyotumika ni halisi kwa watu na mahali.
Kuna kijana mmoja anaitwa Abdul Mohammed. Nadhani sasa ni mtu mzima maana nilisikia alioa na mkewe nikasikia ni Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Tanga. Mwaka 2005/6 akiwa shule ya msingi Mugabe, Sinza, Dar es Salaam, nilimteua awe miongoni mwa watoto yatima na waishio katika mazingira magumu kwa ajili ya kuwapa mafunzo, faraja, ujasiri, kuwa na maono/ndoto chanya, kujua vipaji vyao na kuviendeleza, na kuwajulisha haki zao za kijamii.
Walimu walinipa orodha ya watoto wengi yatima na waishio katika mazingira magumu, lakini nilichagua wachache tu miongoni mwao kulingana na mwongozo na dhima niliyokuwa nayo. Aidha, nikiri kwamba niliwaamini walimu kuwa watoto walionipa ni yatima kweli na/au wanaishi katika mazingira magumu. Sikuwa na namna nyingine yoyote ya kuthibitisha, niliamini na kuheshimu uamuzi na uchaguzi wa walimu.
2. UENDESHAJI MAFUNZO NA MATOKEO YAKE
Mafunzo niliyokuwa nawapa yalifadhiliwa na Family Health International (FHI). Sasa ni FHI360. Katika wilaya 3 za Dar es Salaam (wakati huo) nilichagua shule 3, moja kwa kila wilaya. Kinondoni (Mugabe, Sinza), Ilala (Hekima, Buguruni) na Temeke (Azimio, Tandika).
Kwa msaada wa walimu, niliteua watoto wasiozidi 15 walio katika mazingira magumu zaidi ya wengine katika kila shule. Abdul Mohammed wa shule ya msingi Mugabe akawa miongoni mwao. Kwa wanaoishi Dar es Salaam, shule ya msingi Mugabe ipo kushoto katika barabara ya Shekilango ukitokea barabara ya Morogoro kabla ya kufika Sinza Madukani.
Nilitunga mwongozo (kijitabu) wa mafunzo ambao mpaka sasa ninao. Jina la kijitabu ni Mpango Kazi wa Taifa kwa Watoto Waishio Katika Mazingira Magumu. Ulikuja kumilikiwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii (wakati huo) kwa ufadhili wa FHI kama nilivyoainisha hapo awali. Una mafunzo, nasaha, michoro na mifano muhimu sana ya kumfanya mtoto asonge mbele pasipo kukata tamaa ya maisha hata kama hana mzazi, mlezi au ndugu. Lakini pia unaihamasisha jamii nzima kuwaona watoto ni wetu sote, ijapokuwa wengine hatujawazaa au kuwa na undugu nao.
Kila baada ya kuwasilisha mada moja katika jumla ya mada nane, niliwapa watoto nafasi ya kujadiliana maswali wao kwa wao katika makundi kwa kila mada. Walichaguana wenyewe namna ya kuongozana. Abdul Mohammed hakubaki nyuma, alikuwa miongoni mwa viongozi watatu mahiri. Nami nikabaki mwanafunzi, nikijifunza mengi mno na mazuri kutoka kwao.
Madhila wanayopitia watoto hawa yanatia uchungu na pia yanaleta hisia za huruma. Hata kama wanao udhaifu au hata makosa, bado ni watoto, ila hata sisi wakubwa tunayo pia! Furaha iliyoje jinsi walivyo na matumaini makubwa, vipaji vingi na maono makubwa na ya mbali. Wengine waliitaka nafasi aliyo nayo SSH!
Watoto wengi niliowafunda na kuwafundisha (japo kwa muda mfupi), sasa ni watu wazima, ila sijui wamefikia wapi katika kutimiza ndoto, matamanio na maono ya maisha yao kadri Mungu alivyowajaalia. Naishi mkoani Rukwa kwa sasa lakini natamani sana kuwaona au kuwasikia waliko wote.
Ila hata nisipomwona hata mmoja au wao wasiponiona, nawatakia afya njema na maisha mema. Kamwe wasisahau kuwasaidia wengine kama walivyosaidiwa!
Pamoja na hayo, nilibahatika sana kumsikia mmoja tu, naye ni Abdul Mohammed akiwa Clouds FM, kisha akaenda RadioOne na baadaye BBC Swahili, London, Uingereza. Mnamo mwaka 2014 aliiwakilisha BBC Swahili kwenye Kombe la Dunia nchini Brazil.
Mtangazaji mkongwe Charles Hillary wa Azam atakubaliana nami kwa hilo. Kote huko nilithibitisha uwepo wake japo sikuwahi na sijawahi kuonana naye uso kwa uso na macho kwa macho.
Baadaye tena, nikasikia amerudi nchini na kuwa Mkurugenzi wa Michezo (kama sikosei) Azam na kisha akawa miongoni mwa maafisa wa ngazi za juu CRDB Bank. Sikumbuki cheo chake!
Juma lililopita nimesikia (bado sijathibitisha), kateuliwa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hussein Ali Mwinyi, kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu ya Zanzibar.
Sijui kama ananikumbuka au atakuja kunikumbuka. Hata mafunzo niliyowapa huenda asiyakumbuke! Lakini nafurahi kuwa yalimsaidia kujitambua, kujiamini na kufanya maamuzi mazuri, hadi kuweza kuaminiwa na kuajiriwa na mashirika na makampuni makubwa duniani, wakiwemo BBC na Azam.
Abdul Mohammed kashika nafasi nyingi kwa kitambo kifupi, wakati baadhi ya wenzake bado wanatafuta ajira au kazi ya kwanza au ya kuanzia. Na sasa yuko ikulu ya Zanzibar. Amefanikiwa sana, tena sana!
Ila hata mimi najisikia kufanikiwa sana, angalau kwa kuhusika kidogo kumwezesha mtoto mmoja yatima au aliyekuwa katika mazingira magumu, kufikia cheo cha kuwa Afisa wa Ikulu. Ikulu ya Zanzibar.
3. HITIMISHO
Niwaase vijana, dunia bado ina fursa nyingi mno kuzidi uwingi wa watu, ila mjitambue, mjiamini na kuwa tayari kujaribu kazi yoyote ilimradi halali pasipo kukata tamaa. Na zaidi sana, msiwe na kisingizio chochote cha kushindwa, bali wakati wote muwe na sababu za kushinda katika kila mnachojaribu. Hakuna anayepata mafanikio bila kuanza kujaribu na kuendelea kujaribu tena na tena, hata akikosa!
Mnaweza mkazidi au msifikie mafanikio ya Abdul Mohammed, lakini kwa hakika hamtakosa cha kufanya madhali mna mtaji wa kwanza - Afya Njema. Adui wa kwanza au rafiki wa kwanza kukufanya ushindwe au ushinde kimaisha ni wewe mwenyewe!
Itoshe kusema, mafanikio si kile tu tunachopata (cheo, usomi, ajira nzuri, utajiri au umaarufu), bali pia watu tunaowawezesha kupata sifa au nafasi hizo, hata kama sisi wawezeshaji tutaambulia patupu. Mafanikio yetu makubwa ni kuwepo kwa hao wanaopata sifa au nafasi hizo! Bila kusahau kuwa wanaowafanikisha wengine huendelea kuishi kwa fikra na matendo yao hata baada ya kufa.
Hongera Abdul Mohammed huko uliko (ikulu ya Zanzibar), japo sijawahi kukuona tangu nikufundishe mwaka 2005 ukiwa shule ya msingi Mugabe, Sinza, Dar es Salaam. Lenga zaidi kuwapa faida au mafanikio wengine, ndipo utakapokuwa na faida au mafanikio yadumuyo. Pengine yatadamu si hapa duniani tu, bali huenda hata milele na milele - mbinguni.
Katika picha hapa chini, Abdul Mohammed (mtoto) ni huyo mbele kushoto. Kijitabu cha mwongozo wa mafunzo nilichotunga kinafuata kisha mojawapo ya michoro ya ndani.

Upvote
3