SoC03 Mafanikio thabiti juu ya elimu shuleni na vyuoni

SoC03 Mafanikio thabiti juu ya elimu shuleni na vyuoni

Stories of Change - 2023 Competition

My beginning

Member
Joined
May 31, 2023
Posts
11
Reaction score
8
Mafanikio thabiti juu ya elimu Kwa ngazi zote hupelekea hamasa ya utendaji na uwajibikaji wa hali ya juu katika sekta au kazi fulani. Hii hutokana na kuundwa Kwa msingi imara kipindi mwanafunzi anapokuwa katika taaluma yake. Katika mafanikio thabiti juu ya elimu huundwa na tabia au mikakati fulani Kwa kufikia malengo makubwa juu ya elimu na hii hupelekea ufaulu na mafanikio makubwa Kwa Kila mwanafunzi ambaye anakuwa na tabia au mikakati fulani juu ya elimu yake.

Wanafunzi wengi hushindwa kupata mafanikio ya juu kuhusiana na suala zima la elimu. Hii ni kutokana na ukweli kwamba hakuna mkakati mathubuti juu ya elimu yao. Ifuatayo ni mikakati inayoweza kusaidia wanafunzi katika taaluma na ufaulu wa mitihani na kuleta mafanikio thabiti juu ya elimu;

Mkakati wa kusoma.
Usomaji mzuri huleta mafanikio ya hali ya juu. Katika njia hii mwanafunzi ni lazima awe na ratiba ya kujisomea maana kutokuwa na ratiba ya kujisomea ni moja ya sababu inayopelekea kuanguka au kufeli Kwa mitihani. Utumiaji wa mkakati huu, humpa mwanafunzi nidhamu na mpango mzuri katika masomo na mafanikio thabiti juu ya elimu. Inapaswa mwanafunzi afahamu nini cha kusoma,wakati gani wa kusoma, sehemu ya kusomea na kufahamu ni nani wa kusoma nae ni mambo muhimu ya kuyajua wakati wa kusoma.

Mkakati wa maandalizi ya vifaa vinavyoitajika.
Katika jitihada za kupata ufaulu mzuri shuleni, wanafunzi wanaitajika kuwa na maandalizi mazuri ya vitendea kazi vyote vinavyoitajika katika usomaji. Mpango mbovu wa vifaa vinavyoitajika humaanisha mpango mbovu alionao mwanafunzi. Ni muhimu kuweka vifaa vinavyoitajika mahali ambapo itakuwa ni rahisi kuviona Kwa sababu itatoa nidhamu nzuri ya muda badala ya kuanza kutafuta Kwa muda mrefu.

Mkakati wa kurudia kusoma.
Njia hii ni muhimu sana Kwa maana chochote mtu anachosoma mara ya kwanza ni rahisi kusahau Kwa sababu kitakaa katika kumbukumbu ya muda mfupi. Mkakati wa kurudia kusoma haimaanishi kutokuwa na akili. Hapa ni muhimu kurudia kusisitiza yale yaliyosomwa, kurudia kukumbuka, kupanga mawazo vizuri na Kwa mtiririko mzuri.

Mkakati wa kupumzika.
Mkakati wa kupumzika huifanya akili na ubongo kuwa bora zaidi. Hii hutokana na ukweli kwamba unapo pumzika ubongo unapata sura mpya na itasaidia kuhifadhi vitu vidogo vidogo vya muhimu. Ndio maana inashauriwa kufanya bidii sana mwanzoni mwa masomo kabla ya mitihani kusudi kuwepo na muda mzuri wa kupumzika kipindi cha mitihani. Kutokosa usingizi au kutopumzika usiku wa kuelekea kwenye mtihani itaathiri afya ya ubongo na akili na kupeleka kushindwa kujibu mitihani kwa ubora na viwango vya juu.

Mkakati wa kupima uwezo wa masomo.
Katika njia hii ni muhimu kupima uwezo na tathmini juu ya masomo. Katika njia hii ni kuangalia udhaifu na uwezo wa kimasomo. Kama wanafunzi inatupasa kujiuliza vitu mbalimbali kulingana na uwezo wa kimasomo. Mfano inabidi kutambua udhaifu na nguvu ya somo fulani, hii itasaidia kupata muda zaidi Kwa masomo ambayo Kuna udhaifu na kuwekeza muda mchache Kwa masomo yenye nguvu. Hii itasaidia mafanikio thabiti juu ya elimu zetu na kufaulu Kwa viwango vya juu.

Mkakati wa makundi ya kujadiliana.
Moja ya njia inayosaidia katika mafanikio ya juu ya elimu ni makundi ya kujadiliana. Hii inasaidia sana hata mwanafunzi asipoweza kuelewa Kwa ufasaha darasani anaeweza kuelewa kupitia makundi ya majadiliano. Muhimu ni kuzingatia utayari na kuwa na kundi maalumu la majadiliano, kundi ambalo itakuwa ni rahisi kuelewa na kuondokana na kundi la mabishano. Hii itasaidia kukuza upana na uwezo wa kuelewa zaidi Hali inayopelekea kufaulu Kwa viwango vya juu.

Mkakati wa kuchunguza mpangilio wa mitihani.
Uchunguzaji wa mpangilio wa mitihani husaidia kufahamu mpangilio wa mitihani kwa ubora na Kwa undani zaidi na kufanya mwanafunzi ajiandae vizuri na kuwa na kujiamini Kwa sababu tayari atakuwa amejipanga kujibu na kuchagua maswali na hii huweza kusaidia mkakati wa kukumbuka kuhusiana na mada husika. Mkakati huu utausika na mgawanyo wa sehemu za mitihani pamoja na mgawanyo wa alama.

Mkakati wa kukumbuka.
Lengo la mkakati huu ni kusaidia kushika vitu vyote vya msingi ambavyo ni rahisi kusahaulika kipindi cha mitihani. Baadhi ya taarifa zinazoweza kusahaulika ni kama vile kanuni, majina na michoro. Mkakati wa kukumbuka ni njia nzuri ya kujua uwezo katika somo fulani. Kumfundisha mwingine,kuweka uwiano, kutumia ramani au michoro na kupumzisha akili ni njia nzuri katika mkakati wa kukumbuka ulichosoma, hali inayopelekea mafanikio thabiti ya na upataji wa alama za juu.

Kubwa zaidi, kama wanafunzi wenye kutafuta mafanikio thabiti juu ya elimu zetu tunapaswa kuwa makini ndani na nje ya chumba cha mtihani. Usomaji mzuri wa maswali, chaguo la maswali ya kuanza kutokana na uelewa wa maswali, muda wa kujibu maswali, maandalizi imara na mazingira ya kujiweka salama ni sehemu muhimu tunazopaswa kuzielewa kusudi tupate ufaulu wa viwango vya juu na vyenye mafanikio thabiti na yenye ubora.

Hali ya kukosa maandalizi bora,kukosa mikakati imara, kujadili kabla ya mitihani na mitazamo mibovu ni sababu zinzazopelekea hali ya ya uwoga na kushindwa kujibu maswali vizuri, hali inayopelekea kufeli Kwa wanafunzi wengi na kushindwa kufikia malengo yao na mafanikio ya hali ya juu kuhusu elimu kiujumla.

Msingi mkuu wa kufikia malengo ni suala la kujiamini na kumuamini Mungu na kunyenyekea baraka zake Kwa maana pasipo yeye sisi hatuwezi kufanya kitu kwenye maisha yetu kiujumla. Imani hii itatusaidia kuwa na juhudi zaidi katika safari ya mafanikio yetu kielemu.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom