Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Ngoja waongozwe kwa mfumo huu kama hawatalia. Maana huwezi kuwa na mfumo huu bila kuwa na akina Bashite wa kusaidiana nao.
 
UN itunge sheria za kukodisha viongozi wachapakazi.Mfano inaweza kuwa Rais wa nchi zaidi ya moja.
 
Aisee, habari njema sana hii. Ila wengi wanamsikia tu maana hawajawahi kuja hapa na wala yeye kwenda huko!
 
Mleta mada acha kupunguza "utukufu wa mtakatifu wetu", si ulimwenguni tu hata mbinguni na kuzimu wote wanaimba sifa za mtukufu wetu.Juzijuzi tu kulitaka kufanyika mapinduzi huko kuzimu wakidai wamechoka kuongozwa na ibilisi,wanataka mabadiliko na wanamuhitaji ili ainyooshe jehanamu,upo!
 
mh!anayemkubali mheshimiwa lazima atakuwa yupo kijijini au ana elimu ya hapa na pale!!!!
 
Nianze na Salamu mh nakusalimu katika jina la bwana,mh umefanifanya nishike ssimu yangu kukupongeza kwa kazi nzuri unayofanya uko vizuri nafurahi unavyofanya hubagui chama wala kabila nakupongeza sana, natamani niungane na kauli ya rais mstaafu mh mwinyi lakini yatosha kukupongeza watu wà chini sasa tunaonekana nasi ni watu umefuta ule msemo unajua mi nani ,MSEMO huo ulitutesa sana sasa tunahudumiwa friendly bila rushwa wala takrima hongera sana baba ,ningepata nafasi kufika ulipo Nina ZAWADI ya sala maalum ya ulinzi na novena maalum juu ya kazi ngumu ufanyayo natamani ningepata nafasi kukusaidia lakini acha niendelee kukusaidia huku chini ,Mungu akulinde,malaika wakulinde ufanye kazi zaidi ilikutuletea Maendeleo.simama imara kama ulivopokea kipa imara yako ... Asante
Mimi Paschal Maziku 0673044423
 
Hakuna ubishi pengo la Hayati Julius Nyerere laweza kuzibika.

Rais wa sasa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli anaelekea kuziba pengo la JK Nyerere.

Uchungu wa nchi na uzalendo wa Rais John Pombe Magufuli kwa nchi ya Tanzania ni kielelezo tosha rais huyu anafuata nyayo za Nyerere.

Nyerere alipinga kila ya aina ya uovu ikiwemo rushwa, ufisadi, matumizi mabaya ya rasilimali za umma kwa manufaa ya wananchi.

Na hata rais JPM anaongoza nchi kwa kufuata nyayo za Nyerere.

JPM amejitoa kuwatumikia wananchi masikini wa Tanzania.

Mpenda maendeleo, mzalendo, mchukia rushwa, mkweli, mcha Mungu na mwenye upendo wa nchi na Wananchi.Hizi ni safi chache za Rais John Pombe Magufuli.

Hii imejidhirisha jinsi rais anavyopigania maslahi ya Watanzania katika kuhakikisha maslahi ya Watanzania wanyonge kwa kulinda rasilimali za nchi kama madini na kusimamia ujenzi wa viwanda ili Watanzania wazidi kuwa na maisha bora.

Vilevile amejitoa katika vita na mafisadi walioifilisi nchi, kwani baadhi yao wananyea debe.

Rais JPM amefanikiwa kuimarisha usalama wa wananchi kwa kuimarisha idara zote za usalama.
 
Tatizo ni kuwa watu wanatamani awe perfect kama malaika,ila anajitahidi kwa kweli.
 
sawa dada umesikika kwahyo ulikua uansemaje zaidi! au utume salaam kwa ndg na jamaa na marafiki! lazima wamlaki kwaajili kule ninkwao ! km ww unaendaga kwenu hawakufurahii bas iko shida sehem! mie naona FLAT! subiri maccm wenzio muanze kupeana mioyo zaid
 
Wanajamii jamani mimi nampenda sana Rais wangu sijui nyie...
Ni mpenda maendeleo
Ni jasiri si muoga
Anajitoa kwaajili ya Watanzania.
Mchukia Rushwa
Mchukia Ufisadi
hakika akikaa miaka kama 10 naamini Tanzania tutakuwa mbali.
Kila binadamu anamadhaifu yake ila Rais wetu mazuri yamezidi madhaifu.
Yeye kuwa Rais amewezesha Taasisi za Serikali kusimama kwani hapo nyuma zilikuwa zinakandamizwa na wasiokuwa wazalendo hadi kupelekea nyingine kuuzwa.
Anapenda mali za Tanzania wafaidi Watanzania na si Wageni.
Amejitoa hasa, na hasa wanaofaidi haya ni Masikini ila Matajiri wale waliojipatia utajiri kwa kudhulumu watanzania wengi hawafurahii hili kabisa...wanatamani atoke saa ngapi ili warudi kula tena..

1.- Rais ameleta adabu Serikalini na katika taasisi zake...Sasa hivi ukienda Muhimbili unaheshimika, Unapokewa vizuri na kuhudumiwa hakuna nyodo.

2. - Ameweza tukawatambua waliokuwa wanawadhulumu vijana waliosoma kweli kweli wenye vyeti vyao vya kweli...kwa kuwagundua waliokuwa wanatumia vyeti feki.

3. - ameweza fanya tukawagundua waliokuwa wakijilipa mishahara kwa majina feki

4. - Ameweza pambana na anaendelea kupambana na wizi unaoendelea Bandarini

5. - Ameweza kuwatumbua wasiokuwa watendaji wazuri katika Taasisi za Serikali mfano: TRA, TANESCO, etc.

6. - Ameweza kuwafanya mawaziri aliowateuwa wamuwakilishe katika kazi kuheshimu kazi zao kwani hapo awali walikuwa wafanye kazi wasifanye mshahara unaingia poa tuu...ila sasa unamsikia waziri kabisa akilalamika Jamani mimi ninawatoto msiniharibie kazi...Waziri leo hii anatamani kulia kwa watu ili wasimuharibie kazi...ila hapo awali ilikuwa kawaida tuu kutofanya kazi na kulala bungeni.

7. - Ameweza kudhibiti fedha za umma na kwenda BOT kwani watu walikuwa washazigeuza kuwa za biashara zao.

8. - Ameweza kusababisha MAFISADI PAPA wakakamatwa kama Manji, Rugemarila, na wenzake wakati ingekuwa hapo awali wangeweza kutoroka tena kwa kusindikizwa hadi AIRPORT tena kwa escort tukaambiwa wametoroka..kama ilivyo Alex Massawe alivyofanya na wenzake.

9. - Ameweza kusimamisha Kampuni ya Ndege na kununua ndege ambayo ilikuwa inafilisika..sasa imerudia uhai tena.

10. Miundo mbinu inajengwa mbali mbali ie. Barabara, Airports, Maji kama juzi katoka kuzindua mradi Mwanza n.k.

11. Maji sasa maeneo ya KIMRA na MBEZI ambapo ilikuwa historia maji kutoka japo bomba limepita huko sasa yanatoka.

Ni mengi sana kumaliza ni issue wengine waongezee..

Hakika rais wetu anastahili sifa, na anachukiwa na wengi wabinafsi wanaopenda wao na familia zao tuu zifaidike kwa mali za Tanzania.

Wapinzani wangekuwa na akili wasingekuwa wanapiga kelele kuhusu Rais anachokifanya sasa bali wachape kazi wamuige Rais anachokifanya ili wajiongezee CREDIT.

Tatizo la wapinzani wetu hata jambo la kitaalamu wao wanaingiza siasa ndani yake. Utakuta mwanasiasa si mtaalamu wa Afya atataka aingilie suala la afya, Si mtaalamu wa mambo ya Usalama atataka aingilie...Waachieni wenye Professionals zao wafanye kazi zao.

Wapinzani wenzangu tufanye kazi, Mmepewa jimbo la Ubungo basi tuone matunda yenu.. Fanyeni kazi. Si hadi Mkuu wa Mkoa au Rais aongee kuhusu maji ndipo maji tuletewe...Hakika kama si Uongozi huu wa sasa Kimara na Mbezi kungeendelea kuwa na historia ya kutopata maji ila sasa kwa wale walioomba maji yanatoka..Mnyika ulikuwa Mbunge muda mrefu mbona hukuleta Maji??

Barabara za majimbo ya Ubungo jengeni hasa zile barabara kuu...mfano: Mbezi hadi Mpiji magohe hadi bunju, Mbezi hadi Kinyerezi, mbezi kwa Msuguli hadi Kinyerezi..etc. acheni kuongea tuu...Wabunge tendeeni kazi ubunge wenu mlopewa, wapelekeeni watu maendeleo. Mwenzako akifanya hiki wewe fanya lile..hizi si zama za porojo tena..

MWISHO NAMALIZIA KWA..
Chunguza utabaini: Kila taifa lililokuwa maskini, wananchi wake hawaendi bila kuwaamrisha kisha likaja mpata rais ambaye alikuwa mkali katika taifa lake taifa hilo liliweza pata maendeleo..mfano: Fuatilia sera za Mao Tse-tung na CHINA YAKE ila aliinyoosha china ikasimama, Hitla na German, Gadaafi na Libya hadi kuoa vijana ilifikia wakawa wanalipiwa mahari - hahahaha ona sasa aliyewachonganisha kikowapi leo hii zile mahari hawazipati tena....etc..

Katika uongozi kuna uongozi mwingine lazima kidogo uapply udikteta ili nchi iendelee la sivyo baadhi ya watu watakurudisha nyuma....Na Rais wetu ningependa aaply hiyo kwa hii miaka kumi ili watu wanyooke...

Viongozi wa awali walipelekea hadi kila mmoja kutamani kuwa kiongozi ili aende akapate ulaji...Kwani alijua akiwa tu kiongozi ni ulaji.

Vijana wetu walikuwa wanasoma ili wakapate hela bali si kwa kuipenda kazi...Utasikia mtu anataka kuwa Mhasibu sababu ya alijua akiwa Mhasibu atapata hela za kupiga, Kijana alitaka kusomea Procurement akijua akiwa katika idara ile atapata hela za kupiga.

Hii taswira sasa kwa vijana ibadilike bali vijana wasome kwa uzalendo...

Uongozi ulikuwa unatafutwa hadi kutoa rushwa, sababu walijua mtu ukiwa Waziri, Mbunge utapata hela za kula pasipo kutoka jasho, ila sasa baadhi ya watu wanaukana uongozi / wanaachia ngazi sababu ya kuhofia wao sio watendaji wazuri...

Tanzania inaenda ikiwa ile tunayoitaka...

Nikisema kuandika nii mengiiii hata simalizi leo..naishia hapa..

Namuombea Rais wetu Maisha Mema, Mungu amuongozi katika kazi zake...
 
Wana tupigia kelele tu kumbe.wanapokea hela.
Kumsafisha mtu anayelalamikiwa na watu kwa ugumu wa maisha na ukosefu wa ajira kwa vijana walio na vigezo unafikiri ni suala dogo? Kuna malipo mkuu, hata wale wakuu wa mikoa walioandaa maandamano ya kumpongeza mkuu kuna % zao na pia kama kulipa fadhira!!!.
 

NACHUKIA HII TABIA YA KUHAMISHIWA THREAD YAKO KTK THREAD NYINGINE TENA INAKUWA KAMA COMMENT...AHHH uongozi wa jamii forum acheni hizooo...tutaanzisha jamii forum nyingine
 
Tulimuomba Mungu tupate Rais bora. Mungu amesikia kilio chetu. Magufuli amechagulia kama ilivyokuwa Kwa mfalme Daudi.
 
Salute kwako mh Dr John Pombe Magufuli. wewe ni kisu kikali sana. unatisha. hadi sasa tunapoelekea nusu ya utawala wako wa miaka mitano ya mwanzo, umefunika kila kona, umeirudishia tanzania yetu heshima mara dufu, uchumi unapaa, uadilifu unapaa, uchapakazi unapaa, ukweli unapaa, rushwa inadidimia, mafisadi wanadidimia, ulegevu legevu na kiroho vinadidimia. wezi wanadidimia, hadi say 2030 Tanzania itakuwa kama China au Asian Tigers. HUTAKI UNAACHA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…