Kasi ya Rais John Pombe Magufuli ni zaidi ya 4G na hakika sisi kama wananchi tunamuunga mkono katika kutatua kero za wananchi kwa kuwaondoa au kuwatumbua watumishi ambao hawaendani na kasi yake. Wengi walikuwa wanasema Rais Magufuli hawezi kuwatumbua watumishi aliowachagua kwa kuwa eti ni marafiki zake. Alianza Eliakimu Maswi ( ingawa alikuja kupewa wadhifa mwingine ) akafata mama Anne Kilango Malecela na sasa ni zamu ya Charles Kitwanga kukaa nje ya uongozi wa awamu hii ya tano.
Tujuzane viongozi watakaofata kutumbuliwa ambao kwa kiasi flani wameshindwa kwenda na kasi ya Rais Magufuli ya kutekeleza ahadi ya " hapa kazi tu "