Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mungu mpe afya na uzima pamoja na mafanikio rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh John Pombe Magufuli (Amin)
 
Mafisadi na wale waliokua wananufaika na mfumo wa kifasidi wanahangaika sana kumpunguza kasi, nachokifurahia Magufuli anamsimamo hatoki kwenye reli hata wamtikise vipi
 
Mafisadi na wale waliokua wananufaika na mfumo wa kifasidi wanahangaika sana kumpunguza kasi, nachokifurahia Magufuli anamsimamo hatoki kwenye reli hata wamtikise vipi
Well said
 
Huu ni ukweli mchungu sana.

Najua tulizoeshwa na kuzoea vibaya.

Najua tuliaminishwa kuwa hii ni nguvu ya soda lakini ukweli haujifichi na unaendelea kujidhihirisha...

This is the MAN....
tulizoea nini? kukosa madawa hospitali? kutopandishwa mishahara? kupoteza ajira sekta binafsi?
 
Wazee Wa madili wakubali kubadilika tu.. JPM endelea kukaza
 
tulizoea nini? kukosa madawa hospitali? kutopandishwa mishahara? kupoteza ajira sekta binafsi?
Umesahau kingne ULIZOEA KUIBIA NCHII HII.....sasa wameziba mirija yoyote unaanza kulialia sasa hivi....NA BADO mpaka uturudishie vyetu
 
Naunga mkono baadhi ya mambo mazuri anayofanamya lakini anakosea sehemu moja kuu, kuwanyima vijana Ajira, ajira hata wewetoa mada ni Mhanga wa kukosa ajira
 
Magufuli rais wetu inabidi awekewe ulinzi mkubwa na mkali. wako watu wamekaa mkao wa kutaka kuhujumu kila kitu..
Mkuu ana ulinzi wa kutosha kabisa
...no doubt about that.... Na sasa hivi Mkuu wa Nchi akisema.. Twajua kabisa hili limesemwa na Mh. Rais... Ngoja heshma irudi kdg.
 
MNATAKA CHUNGU AU TAMU ??
1. Tanzania hatuna ndege hata moja nchi nzima , hii ni aibu kwa serikali ya CCM !!
- Serikali ya CCM haijui vipaumbele vya watanzania yaani wananunua ndege mpya pesa yote hiyo

2. Serikali ya CCM inalinda uovu watu wanatafuna kodi za wanyonge hawafanywi lolote , tunapaswa kuwa na serikali yenye kiongozi wa kuamua bila huruma hii serikali imechoka haina maamuzi magumu

- Watu wanafukuzwa kazi bila kusikilizwa, wanavunjiwa haki zao za utumishi na kibinadamu hili halivumiliki

3. Hii serikali inapoteza muda mwingi kujadili mambo tu, kila kiongozi mpaka mkuu anaongea sana bila vitendo ndiyo maana tunasema serikali ya CCM inalea ujinga

- Hii serikali ya CCM inafanya mambo bila kushirikisha kila siku wanaibuka na mambo yao hata sisi wabunge hatujui , tunahitaji kushirikishwa kwanza kwani kuna haraka ya nini yakufanya mambo

4. Hii ni serikali dhaifu sana inashindwa hata kukusanya kodi kwa wafanyabiashara wakubwa hii ni aibu

- Hizi kodi zimezidi TRA wanakusanya kodi kibabe kwa wafanyabiashara huu ni uonevu lazima tuangalie namna ya kuwapendelea ili biashara ikue

5. Hii nchi ina resources nyingi sana kupitia bandari tu tunaweza kukusanya mapato ya kutosha , tatizo serikali ya CCM inakumbatia uozo mtu akipata kazi bandarini muda mfupi ananuka pesa za wizi !!

- Serikali imeweka masharti mengi bandarini , kodi ni nyingi, upekuzi umezidi mpaka imekuwa kero , hii serikali haina utaratibu mzuri

6. Hii serikali imeruhusu uhuru kupitiliza viongozi wanadharilishwa na vyombo vya habari, viongozi wanatukanwa hovyo, vijana wanatumia social media vibaya kutukana hasa wa CCM na serikali imewafumbia macho !!!

- Hii serikali inawanyima watu uhuru wa kusema, vyombo vya habari vinaminywa, tunahitaji uhuru wa vyombo vya habari

7. Hii serikali inaogopa watu yaani mtu anakula kodi za wanyonge anahamishwa badala ya kufukuzwa jumla, mbona kuna vijana wengi wasomi mtaani !!!

- Hii serikali inafanya uteuzi sana , watu wanafukuzwa hovyo , tunahitaji wasikilizwe kwanza

8. Rais anafanya safari za nje sana imekuwa kero , amekuwa zaidi ya Vasco sijui huko anafuata nini wakati kuna mabalozi !!
- Tunahitaji rais asafiri kwanini hasafiri , serikali inaongozwa na mtu asiyetaka kwenda nje ya nchi huu ni udhaifu mkubwa

9. Hii serikali inajitahidi kiongozi serious siyo mtu anaongea anacheka mpaka vitu serious lazima kiongozi akiongea watu waogope !!!

- Huyo kiongozi yupo serious sana mpaka anatisha siyo vzr kwa afya ya taifa kiongozi lazima awe anacheka na kuvutia anapoongea/hutubia lazima tufanye mabadiliko

10. Hii serikali inapokea ushauri hovyo ndiyo maana tunashuhudia maamuzi ya hovyo kila siku, tunahitaji kiongozi mwenye misimamo binafsi yenye faida kwa taifa siyo kupokea tu ushauri , yaani viongozi wa CCM wanampangia mpaka uteuzi

- Huyu kiongozi hashauriki yaani kila kitu anataka afanye mwenyewe, tunahitaji mtu anayesikiliza tumechoka kuamuliwa kama watoto

NB ; -Hivi ninyi wapinzani mnataka nini hasa kifanyike mfurahi ?
- Hivi aliyewaroga ni marehemu au mmeshindwa kumuomba awazindue kwa ujinga wenu ?
- Hivi mna kitu mnachomudu vyema kuliko unafiki ?

Nina hakika hata Malaika aje kutawala Tanzania wapinzani watasema wanamtaka shetani , watasema wamechoshwa na mema wanataka maovu.

Mwisho Mh Rais John Pombe Magufuli JPM , watanzania wapo nyuma yako kaza mpaka mwisho ndiyo furaha ya watanzania, tunahitaji kusonga mbele siyo sarakasi na vijembe.

Kumpinga JPM kwa hali tuliyokuwa nayo watanzania ni sawa na kumtukuza shetani na kufurahia umasikini wetu ktk Taifa tajiri, Mungu akulinde JPM hakika wewe ni ndoto ya watanzania
Ndimi mbili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…