joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,617
Nimekua nikisoma sehemu nyingi ambapo watu wengi sana, ndani na nje ya Tanzania wakisema kwa sauti na kwa wingi sana kwamba, kupungua kwa maambukizi ya Corona Tanzania imetokana na kumuamini Mungu, hivyo Mungu amejibu.
Hii inatokana na msimamo wa Magufuli wa kutofunga nyumba za ibada na kuwaomba wananchi wamuombe Mungu mara kwa Mara kuwalinda dhidi ya Corona, hata kutoa siku maalumu ili kuwepo kwa siku za kitaifa za kufanya maombi.
Bwana Yesu aliwahi kusikika akisema kwamba" Imani yako itakuponya", je hii inamaana kwamba watanzania ndio wenye imani lakini mataifa mengine hayana hiyo imani ndio sababu bado maambukizi yanaongezeka kwa kasi? Je, Magufuli ndiye rais pekee mwenye imani hapa duniani?
Tumeshuhudia viongozi mbalimbali duniani wakiwemo viongozi wa makanisa wengi ambao walikataa kufunga makanisa wakipoteza maisha kutokana na Corona, je hao wote hawana Mungu?
Tanzania kuna jambo au njia tofauti tuliyotumia ambayo haikuzingatiwa sana na nchi zingine, ndio chimbuko na sababu kubwa ya kupungua kwa maambukizi.