Mafanikio ya wanaume hupimwaje?

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,421

Mke anapomjali na kumkubali mume humuongezea kujiamini…

Mahusiano kati ya mume na mke nyumbani huweza kumfanya mume afanikiwe kwenye shughuli zake au aanguke.

Kwa nini?

Ni kwamba, mtu ambaye anakataliwa na mtu au watu wanaomhusu huwa anakosa kujiamini, huwa anafikia mahali ambapo hujichukia hata yeye mwenyewe. Mke anapomkosoa mume, anapomlalamikia kila mara na kuwa na ghubu, bila kujali kama mume huyo amekosa au hapana, mume hufikia mahali huanza kujitilia mashaka kama kweli ana uwezo wa kufanya mambo, kama kweli ana thamani anayodhani kuwa anayo.

Kujiuliza huku mara nyingi kuna maana ya mwanaume kuanza kupoteza kujiamini na hata kuanza kuwa na uhusiano mbaya na watu anaohusiana nao mahali pengine kama kazini. Unaweza kumgundua mtu ambaye ana mke mlalamikaji, mkosoaji na mwenye ghubu kwa kuangalia jinsi anavyojitathmini. Kama mke ni mkosoaji na mwenye ghubu kwa mumewe ni lazima mume atakosa kujiamini katika kufanya mambo yake mengi, ni lazima ataanza kuwa na uhusiano mbaya na watu wengine kutokana na hukohuko kutojiamini kwake ambako kumesababishwa na ghubu na kukosoa kwingi kwa mkewe.

Mwanaume ambaye ana mke mkosoaji na mwenye ghubu hutokea kutowapenda watu wengine na kukosoa wengine inatokea kuwa sehemu muhimu kwa maisha yake, anatokea kuwa na hasira za karibukaribu na ni vigumu sana kwa mtu wa aina hii kuelewana na watu.

Baadhi ya makampuni huko Marekani, kabla hayajampandisha mtumishi wake cheo, humchunguza mke wa mtumishi. Hawachunguzi kama ni mzuri wa sura au kama anajua mapenzi au kupika vizuri. Mara zote huchunguza kama mwanamke huwa anampa mumewe moyo, kama hamkosoi na kumlalamikia na kama hana ghubu. Wanapogundua kwamba mke wa mtumishi siyo mkosoaji wala mwenye kulalamika-lalamika humpa cheo mtumishi kwa imani kwamba atakuwa ni mtu mwenye kujiamini.

Lakini wanapogundua kwamba mke ni mwenye kukosoa, mwenye ghubu na mlalamikaji, kamwe hawampi mtumishi cheo, kwa sababu wanaamini kwamba, mtumishi huyo hawezi kuwa makini, atakuwa hajiamini.
 
Nimeipenda hiyo picha Mtambuzi......asante kwa somo,naahidi sitakua na gubu kwa mume wangu.
 
Last edited by a moderator:
okay, ngoja tuwabembeleze watukubali, la sivyo vyeo tutavisikia kwenye bomba tu huko kazini
 
Mmmh na mke akiwa na mume mwenye gubu je naye pia haathiriki? MImi naona it works both ways, psychological effect is the same ukiwa hauna moral support haijalishi uko kwenye mahusiano au lah.

Hiyo ya cheo nimeipenda however, ninavyojua mimi ukiwa single/bachelor/unmarried hawawezi kupewa cheo kikubwa kama CEO, assuming you will have support at home which will motivate you to work hard and hard. More or less, matamanio ya mwili hayayumbisha your decision making.
 
safi.................................................
 
More or less, matamanio ya mwili hayayumbisha your decision making.

kwa hiyo na kale 'kadozi' kakitolewa vizuri home kanafanya mtu akonsetreiti na kuthink streit eeh.....
 
MadameX unaweza kudhani nimeliangalia jambo hili ki-mfumo dume, lakini sivyo hivyo, bali nilikuwa naliangalia jambo hili kutokana na kile kinachoitwa "mume ni kichwa cha familia."
Nakubaliana na wewe kwamba kisaikolojia it works both ways, lakini hebu tumuangalie mtu kama Obama, je kama angekuwa na mke mwenye 'kinyamkera' unadhani angafikia hapo alipofikia?
Upande unaohusika sana hapa ni ule wa kiume kwa sababu kutegemeana kwa wanandoa mara nyingi hutazamwa kutokana na mafanikio aliyoyapata mwanaume (Kimazoea) lakini hata kama mke ndiye mwenye mafanikio mara nyingi hilo halitazamwi kama ni mafanikio ya wanandoa bali ya mwanamke na kutasemwa mengi likiwemo la mwanamke kumtawala mume................!
Na kama mume hana busara anaweza kuivuruga ndoa yake kiasi cha kuvunjika.

Nakubaliana na wewe.......................
 
Daaah . . . . kumbe nilikuwa nakosa uhondo humu ndani?!!
 
mwanaume anayenyanyaswa na mke wake home utamjua tu na kama ni bosi mtakoma hapo ofisini kwani ananza kugomba bila mpangilio hata kabla hajashuka kwenye gari. Kisa haziivi na mke wake nyumbani.
 

nasikia rais wa ufaransa hana mke.
 
mwanaume anayenyanyaswa na mke wake home utamjua tu na kama ni bosi mtakoma hapo ofisini kwani ananza kugomba bila mpangilio hata kabla hajashuka kwenye gari. Kisa haziivi na mke wake nyumbani.

mmmmhhh una uhakika?
 
wengine mafanikio ya mume yanapimwa kwa kuijali familia i.e kuwekeza, kupeleka watoto hospital, kulipa ada za watoto mashuleni na kufanya nao home work, kucheza nao nyumbani na kuwatoa out, kuwapikia, kufanya shopping, kusaidia ndugu na jamaa, kutokuwa na vimada na kutokunywa pombe na pia kuvuta sigara na madawa mengine ya kulevya na kuongeza nguvu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…