Mkulima wa kawaida
Senior Member
- Dec 22, 2012
- 167
- 37
Nilianza kuuza karanga kwenye maeneo ya stand za mabasi, nikahamia kuuza saa, baada ya kupata kidogo nikatafuta shule ya evening class nikasoma hadi kidato cha nne nikapata div II: 20. Nikachaguliwa kidato cha tano (PCB), Nikahitimu 4m 6 nikapata div III:13, Nikaomba SUA (B.SC. Agriculture General), baada ya hapo nilifungua kampuni na ninafanya biashara ya maza (agribusiness) na wakati huo huo nimepata shavu serikalini. Wadau hayo ni machache lakini tujitume zaidi.