Mafaniko katika biashara ni mchakato wa muda mrefu

Jackson94

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2016
Posts
492
Reaction score
560
Karibu kila mtoto wa shule ya msingi utakayekutana naye leo ukamuuliza (kwa wale wanaojitambua) anataka kufika wapi kielimu, atakuambia anataka kufika Chuo Kikuu. Ni ndoto ya karibu kila mtoto anayependa shule, lakini kamwe huwezi kufika chuo Kikuu kama hutafaulu shule ya msingi na sekondari.

Hii inamaanisha kuwa, katika maisha ili kufanikiwa kufikia malengo yako kuna hatua ambazo nilazima uzipitie. Huwezi kulala ukiwa darasa la kwanza na kuamka ukiwa Chuo Kikuu, nilazima kusoma kwa bidii, kupiga umande, kuamka asubuhi, kukesha, ili kufaulu mitihani ya kila ngazi itakayokupelekea kufika huko.

Hivyo hivyo katika biashara, kila mtu ukimuuliza atakuambia nataka kufungua duka kubwa kama la flani, lakini ni wachache sana ambao hujiuliza kuwa flani alifikafikaje hapo alipo. Hawajiulizi alianza na mtaji kaisi gani, hawajiulizi alifilisika mara ngapi,hawajiulizi alitapeliwa mara ngapi, hawajiulizi alilala nnje mara ngapi?

Kama ndiyo umeanza bishara basi jua kuwa hapo ulipo ni hatua ya kwanza tu, kuna mengi yanakuja kama utaielekeza akili yako katika kuboresha huduma unayotoa na si kutaka kuwa kama flani. Yaani kama mwanafunzi ukiielekeza akili yako kuwaza chuo kikuu wakati husomi basi utafeli, akili yako inapaswa kuwa katika kuboresha biashara yako, kuisimamia vizuri na utajikuta hata huyo flani unampita.

Kabla ya kutaka kuwa na wateja 1000 hakikisha wateja kumi ulionao sasa wanaridhika na kufurahia huduma zako, hakikisha kuwa wanatamani kurudi kwako, hawa ndiyo watakuletea wateja 1000 na si tamaa zako za kutaka kufanikiwa kwa haraka. Ndiyo mafanikio ni matamu, lakini ni matamu zaidi kama uliyatolea jasho.

Kumbuka kuwa hata chakula kitamu hakichemshwi tu dakika tano na kuwa kitamu, hupikwa kwa muda mrefu na mara kadhaa unaweza kujikata wakati unamenya vitunguu au kuungua wakati unaepua chakula lakini ukiwa mezani yote unayasahau na kukifurahia chakula. Jikite katika kuboresha huduma kwani pesa hufuata ubora.
Jackson9
 
Kweli kila kitu kinachangamoto biashara ni pasua kichwa unaweza ukatoa chozi.


Ukiwa na madeni ndo usiseme.
 
Subscribe to support and motivate . 100% LEARN ICT SKILLS HERE
 
Subscribe to support and motivate . 100% LEARN ICT SKILLS HERE
 
Asante mkuu somo zuri Karibu na Mjasiriamali Desk tubadilishane maarifa haya tukuze uchumi wetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…