Mafao yangu ya PPF

SWEET GIRL

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2011
Posts
520
Reaction score
377
Jaman mimi nina maswali mengi kuhusu PPF yangu.Nilitoa notice ya mwezi mmoja kuacha kazi pale nilipokuwa nafanyia na ilikuwa mwezi wa tano.Toka wakati huo nimekuwa nikifuatilia malipo yangu na toka wakati huo sijapata malipo na nilikuwa nikijibiwa kwamba wanafanyia kazi.jana nilikwenda ofisi kwao kuulizia mustakabali wa mafao yangu nikajibiwa kuwa cheque yangu ipo tayari ila wameambiwa wastop kila kitu mpaka watapopata maelekezo kutoka huko SSRA na kwamba PPF wamewaandikia barua SSRA ili wawape mwongozo kwamba wafanyeje kwa malipo yale yaliyokuwa tayari but mpaka sasa hawajapata majibu na sijui nini kinaendelea huko SSRA.
Mimi najiuliza je hiyo sheria inaanza kutumika lini??
Na je kwa sisi tulioapply kupewa malipo yetu kabla ya sheria kusainiwa na raisi je tutalipwa malipo yetu au tusahau??
kwakweli kama kuna wadau humu au wanasheria tafadhali watupe majibu ili tujue msimamo wao.
 
Kesho kachukue hundi yako. Huyo kilaza wa SSRA kasema walioacha kabla ya 20/7 wachukue pesa yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…