Mafikizolo waupa wimbo wao jina la kiswahili, video kufanyika hapa Tanzania

Mafikizolo waupa wimbo wao jina la kiswahili, video kufanyika hapa Tanzania

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
Kundi la muziki la Mafikizolo kutoka Afrika Kusini ambalo lipo nchini kwajili ya show moja itakayofanyika leo Mlimani City, lina mpango wa kufanya video ya wimbo wao mpya ‘Nakupenda’ hapa Tanzania kabla ya kuondoka.

“Tungependa kufanya video ya Nakupenda hapa Dar kwani jina la wimbo ni la kiswahili na itapendeza hivyo, bado hatujapata director wa kufanya video hii ila ndio mpango wetu”
Pia Mafikizolo wamesema wamefanya mabadiliko makubwa katika muziki wao ili kukidhi haja za bara zima la Afrika.

“mabadiliko ya muziki wetu yalifanyika ili kuteka soko la bara lote la Africa na zaidi ikiwezekana ndio maana Khona na Happiness zina miondoka tofauti”. Alisema Nhlanhla Nciza

Katika hatua nyingine Mafikizolo wamethibitisha kuwa wanampango wa kufanya kazi na msanii mkubwa kutoka Tanzania atakaye tajwa hivi karibuni na collabo hii ndio chanzo cha kuboresha mahusiano mazuri na wasanii wa Tanzania.
 
Wanawaza biashara. Good for them....
 
Huyo msanii atakua ni domo tuuuu
 
Kila msanii maarufu anakuja bongo.

inamana soko la bongo linalipa sana au mapromota wapo siriaz na kazi zao?
 
hao bila shaka wanampango wa kufanya kazi na twenty pa mzee wa cha Arusha...
 
Kila msanii maarufu anakuja bongo.

inamana soko la bongo linalipa sana au mapromota wapo siriaz na kazi zao?

Mkuu hao wanazunguka dunia nzima pia kwa Tanzania na hiyo nyimbo yao ya kiswahili watakuwa wametageti nchi za Afrika mashariki na kati.
 
Back
Top Bottom