Mshtakiwa wa epa na mwenzake jela miaka 18

Mshtakiwa wa epa na mwenzake jela miaka 18

THE CHOICE

Member
Joined
Jul 11, 2012
Posts
19
Reaction score
1
Rajabu-Maranda.jpg

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, imemhukumu kifungo cha miaka 18 jela Kada wa CCM, Rajabu Maranda na binamu yake, Farijala Hussein katika kesi ya tuhuma za kuchota Sh2.2 bilioni za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Mahakimu wawili

==

Hukumu hiyo ilitolewa jana Mahakamani ambapo waliyohukumiwa ni pamoja Rajabu Maranda na Farijala Hussein ambao ni ndugu ambapo imedaiwa ni mtu na binamu yake

Hukumu ambayo ilisomwa na Hakimu Kahyoza na aliitoa kwa kusema baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi saba wa upande wa mashtaka mahakama bila kuacha shaka imeona washtakiwa hao wana hatia kwenye makosa sita kati ya saba waliuyoshitakiwa

Mahakama imetoa hukumu hiyo baada ya washitakiwa hao kupatikana na hatia ya makosa sita kati ya saba waliyokuwa wanakabiliwa nayo ikiwemo la kujipatia fedha Sh. bilioni 2.2 za Akaunti ya malipo ya Madeni ya Nje (Epa) kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Kufuatia kifungo hicho wametimiza jumla ya miaka 18 jela ambapo awali walishahukumiwa kifungo cha miaka mitano ambapo hukumu hiyo itakwenda sambamba na kile cha awali

Hukumu hiyo ya imeainisha kuwa kwa kila kosa watatumikia miaka mitatu jela ambapo wamepatikana na makosa sita limo la kula njama, kughushi nyaraka, kuwasilisha hati bandia na kujipatia Sh. 2,266,049,041.25 kutoka katika Benki hiyo

Kwa mujibu wa Hakimu, washtakiwa hao wataanza kutumikia kiifungo hicho kuanzia jana sambamba na kifungo cha awali.

Awali katika kesi ya msingi, washtakiwa hao walidaiwa kuwa Machi 20 -25 Desemba, mwaka 2005 washitakiwa hao walijipatia hizo wakidai kwamba Kampuni ya B.Graciel ya Ujerumani imehamishiwa deni na Kampuni ya Money Planers & Consultant ya Tanzania.
 
Nilitegemea mleta habari umesoma vizuri kwenye source ya habari yako.
"Hakimu Projestus Kahyoza na mwenzake Catherine Revocate iliwatia hatiani washtakiwa katika makosa sita kati ya saba yaliyokuwa yakiwakabili, na kuwahukumu kifungo cha miaka mitatu kwa kila kosa. Hata hivyo, wakati wakisoma hukumu hiyo, mahakimu hao walisema badala ya washtakiwa kutumikia kifungo cha miaka 18, hukumu yao itaenda sambamba hivyo watatumikia kifungo cha miaka mitatu jela"

Kwa maelezo haya yaliyoko kwenye source uliyotupatia nakuomba ubadili heading yako

Source ni Blog ya THE SOURCE na wewe mwenyewe ni THE SOORCE maana yake haupo makini na taarifa zako au mimi sijakuelewa!
 
Siku za mbeleni wahusika wakuu watasogezwa mbele ya haki na hata kurejea hizi hukumu. Mahakimu na majaji wawe macho sana katika kesi za skendo za kitaifa na kimataifa
 
mie Kama sielewielewi vile kesi ya EPA ipo hii tu?
 
[TABLE="width: 491"]
[TR="bgcolor: #E1E1E1"]
[TD]
6541706.jpg
[/TD]
[TD]MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu ya jijini Dar es Salaam,

imewahukumu washitakiwa waliokuwa wanakabiliwa na mashitaka ya

kujipatia fedha isivyo halali kutoka

kwenye Akaunti ya Malipo ya Madeni ya nje [EPA] kwenda jela miaka 18 kila mmoja[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 3"]Hukumu hiyo ilitolewa jana Mahakamani ambapo waliyohukumiwa ni pamoja Rajabu Maranda na Farijala Hussein ambao ni ndugu ambapo imedaiwa ni mtu na binamu yake

Hukumu ambayo ilisomwa na Hakimu Kahyoza na aliitoa kwa kusema baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi saba wa upande wa mashtaka mahakama bila kuacha shaka imeona washtakiwa hao wana hatia kwenye makosa sita kati ya saba waliuyoshitakiwa

Mahakama imetoa hukumu hiyo baada ya washitakiwa hao kupatikana na hatia ya makosa sita kati ya saba waliyokuwa wanakabiliwa nayo ikiwemo la kujipatia fedha Sh. bilioni 2.2 za Akaunti ya malipo ya Madeni ya Nje (Epa) kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Kufuatia kifungo hicho wametimiza jumla ya miaka 18 jela ambapo awali walishahukumiwa kifungo cha miaka mitano ambapo hukumu hiyo itakwenda sambamba na kile cha awali

Hukumu hiyo ya imeainisha kuwa kwa kila kosa watatumikia miaka mitatu jela ambapo wamepatikana na makosa sita limo la kula njama, kughushi nyaraka, kuwasilisha hati bandia na kujipatia Sh. 2,266,049,041.25 kutoka katika Benki hiyo

Kwa mujibu wa Hakimu, washtakiwa hao wataanza kutumikia kiifungo hicho kuanzia jana sambamba na kifungo cha awali.

Awali katika kesi ya msingi, washtakiwa hao walidaiwa kuwa Machi 20 -25 Desemba, mwaka 2005 washitakiwa hao walijipatia hizo wakidai kwamba Kampuni ya B.Graciel ya Ujerumani imehamishiwa deni na Kampuni ya Money Planers & Consultant ya Tanzania.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Mafisadi EPA miaka 18 kila mmoja
 
Back
Top Bottom