katika hali inayoonyesha kuwa ni jitihada za kufifisha moto wa vita ya ufisadi nchini, mafisadi wanajipanga kumng'oa mbunge wa kishapu ndugu fredrick tungu mpendazoe. Mpaka sasa mafisadi wakiongozwa na kinara wao wao rostam wameanza jitihada za kumchafua. Jumamosi iliandikwa katika gazeti la mtanzania kuwa mpendazoe anatengeza makundi jimboni, jana jumatano gazeti la majira limerudia habari hiyo. Mtu anayeandaliwa na mafisadi kuchukua nafasi hiyo ni katibu mkuu wa uvccm ndugu shigela ambaye ana baraka zote za mafisadi ikisemakana na mkuu mwenyewe mr handsome.
kwa hatua hii bado vita dhidi ya ufisadi ni ngumu na ndugu wana jf tuchangie kuona ni jinsi gani mpiganaji mwenzetu ndugu ft mpendazoe atabaki kuendeleza moto wa ufisadi
wana jf ni jambo la ajabu hii inayoitwa vita dhidi ya ufisadi kuwa chaka la kimbilio la kila mtu na ambao wameshindwa ku perfome wakibanwa mbavu wanakimbilia kuwa mafisadi wanataka kuwa ondoa.
Wana jf kwanza nashauri hii vita isiwe jambo ambalo lifunge demokrasia nilipata bahati nikatembelea wilaya moja inaitwa nzega nikiwa pale nilienda kikazi ktk halmashauri ya wilaya hiyo kwa siku 15 nilizokaa pale niliweza kuongea na watu zaidi ya 20 watu,swali langu lilkuwa ikiwa leo unaambiwa chagua mbunge wako utamchaguwa nani?
Nilifika nikiwa najuwa majina mawili lucas selelii na hussein bashe ambae nilisoma hapa jf ikisemekana nae anapelekwa na mafisadi kumuondoa selelii,nikitaka kujiridhisha, kati ya hao 20, 14 walisema watamchagua bashe, watu 3 walisema watamchagua selelii na mmoja alikuwa wazi alisema hategemei kuchagua mtu wa ccm.
Nikafanya uchunguzi kwa wafanyakazi wa halamshauri ambao nilikuwa nafanya nao kazi ktk idara ya uhasibu 70% walisema selelii hana nafasi.
Ktk bar n hoteli ukisikiliza mazungumzo huyu mtu ambae anasema mafisadi wanamdhoofisha hana vote,sasa hapa jf tujiulize je kila anaepambana na mafisadi ametekelea wajibu wake ktk eneo lake?.
Nilifika mwaka jana halamshauri ya kishapu mpendazoe ni kiongozi ambae ktk siasa za kitaifa amefanya kazi,tatizo ni ktk jimbo lake hajafanya jambo lolote,nachoshauri jf tusiruhusu vita hii ya ufisadi ikawa kimbilio la watu walioshindwa kutekeleza majukumu yao