Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Raisi Masisi akila kiapo wakati akiapishwa kuwa raisi wa Botswana mwaka 2018. Picha na AFP
Maisha ya raisi wa Botswana Mokgweetsi Masisi yako hatarini baada ya mafisadi wakishirikiana na baadhi ya raia wa kigeni wenye uwezo wa kifedha kutoka nje ya Botswana kupanga kumuua kiongozi huyo.
Mpango huo wa kumuua kiongozi huyo unadaiwa kuratibiwa na aliewahi kuwa mkurugenzi mkuu wa idara ya usalama ya DISS bwana Isaac Kgosi ambae aliondolewa kwenye nafasi yake hiyo mara baada ya raisi Masisi kuingia madarakani.
Mara baada ya kuingia madarakani mwezi April mwaka 2018, raisi Masisi alianzisha kampeni ya kuwashughulikia wale wote ambao wamekuwa wakijishughulisha na ufisadi na kujitochotea maliasili ya nchi hiyo hususan madini ya almasi.
Mwezi Julai mwaka jana mahakama kuu ya nchi hiyo iliamuru kutaifishwa kwa mali zote za bwana Kgosi na pia kuamuru uchunguzi kufanywa juu ya kujishughulisha kwake na masuala ya kifisadi na uendekezaji vitendo vya rushwa.
Kwa mujibu wa mkuu mpya wa idara ya usalama DISS brigedia Peter Magosi, ulinzi wa raisi Masisi umeangaliwa na kubadilishwa kulingana na ngazi ya tishio hilo la kuuawa na tayari idara ya DISS inaajiri wanajeshi na makomandoo wa zamani kutoka jeshi la Botswana ili kuongeza ulinzi kwa kiongozi huyo.
Tishio hilo linadaiwa kuhusisha watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya Bitswana ambao maslahi yao kwa namna moja ama ingine yamegushwa na hatua kadhaa za serikali ya raisi Masisi kuweka sheria mbalimbali dhidi ya udhibiti wa maliasili za nchi hiyo.
Endapo raisi Masisi ataondolewa kiongozi ajae atakuwa na woga juu ya kuchukua hatua zozote zenye kuwabana mafisadi ambao wapo kwenye mkao wa kugawana rasilimali za nchi hiyo.
Brigedia Magosi anadai pia kuwa ndani ya idara ya DISS wamegundulika baadhi ya maofisa ambao ni ndumila kuwili au double Agents ambao wanafanya kazi mbili kati ya serikali ya Botswana na na umoja wa mafisadi.
Brigedia Magosi ambae amewahi kuwa mkuu wa kitengo cha ujasusi ndani ya jeshi la Botswana BDF amedasi kuwagundua baadhi ya maofisa ambao wengi wameonekana kutokubaliana na aina ya uongozi wake na aina ya mawazo yake mapya ndani ya idara ya DISS.
Mkurugenzi wa sasa wa sasa wa DISS Brigedia Magosi (kushoto) na mkurugenzi wa zamani bwana Isaac Kgosi(kulia)
Kutokana na hali hiyo Brigedia Magosi amesema idara ya DISS kwa sasa inaajiri maofisa wastaafu wa idara ya ujasusi wa jeshi yaani military intelligence au MI na wengine kutoka jeshi la nchi hiyo BDF.
Mpaka sasa raisi Masisi na familia yake wanaishi kwenye ikulu namba mbili ambayo hukaliwa na makamu wa raisi na makamu wake huyo sasa anaishi kwenye nytumba yenye hadhi ya uwaziri.
Rekodi nzuri ya uchumi wa Botswana inajengwa na misingi mizuri ya usimamizi wa uchumbaji madini ya Almasi.
Ni nchi inayoaminika kuwa na kiwango kidogo sana cha vitendo vya rushwa na ufisadi, hivyo kuifanya kuwa nchi oekee inayoweza kugundua kwa uharaka mara raia wake wanapojishirikisha na vitendo hivyo kwa kushirikiana na wageni.
Richard na vyombo vya habari vya Botswana nikiwa Gaborone.