Mafisadi wamefanikiwa

Asha Abdala

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2007
Posts
1,130
Reaction score
45
Mafisadi wamefanikiwa

Kwa takribani wiki nzima hapa JF na hata kwenye baa hapa nyumbani kote mjadala ulioshika kasi ni mkopo wa Mbowe. Je, mafisadi wamefanikiwa kutugeuza mawazo? Mbona hatumuulizi tena Rostam Aziz atarudisha lini fedha za mkataba batili wa Dowans/Richmond? Je, maelezo ya kamati ya EPA yametutosheleza? Je, tumemwacha Lowassa aende nchi Takatifu badala ya kutupa majibu? Na Mkapa naye ya Kenya si yamechakwisha? Anasemaje kuhusu Kiwira? Yule Jeetu Patel amesharejea? Na Balalli naye hajapona tu? Yule Vishlani wa Rada bado haonekani kama Osama? Je, Sakata la NSSF na Manji tumelisahau? Vipi orodha ya wauza unga toka kwa Kikwete?
 

NO Asha,

Hawajafanikiwa ila hii ni part ya process. Mambo mengi yanaenda kwa circles na hii ilikuwa ya kujadili hili jambo la NSSF ambalo limefungua the whole new chapter kwenye uteuzi wa Mkullo kuwa waziri wa fedha.

Kuna wengi hawakujua kwa nini Mkullo ameteuliwa kuwa waziri wa fedha pamoja na kashfa zote alizonazo ila hii ya kuendeleza case ya Mbowe mahakamani kutaweka nafasi ya watanzania kudai uchunguzi huru wa pesa zote za NSSF na zile walizokopeshwa kina Manji na Rostam bila interest au promise ya kulipa karibuni!

Hii imefungua another front kwenye fight dhidi ya mafisadi so get ready for the fight!
 
 

Jibu: Tumetumwa, hutaki?
 
Mkuu Babah,

1. Labda tukufahamishe wewe mambo yakoje hapa JF, maana namba za michango, na tarehe za kujiunga zinajisema zenyewe kuwa betweeen mimi na wewe nani anatakiwa kumfahamisha mwingine kuhusu kumkoma nyani hapa JF.

2. Halafu hapa siamini kuwa kuna aliyetumwa na mtu yoyote kusema mawazo yake, yaaani siamini kuwa wewe mawazo yuko hapa umetumwa na mtu, halafu nimshakuomba mara nyingi sana kuwa unapotoa mifano yako ya uvyama na ku-divide watu hapa, jaribu kuniweka pembeni, sipendi jina langu kurushwa rushwa ovyo bila sababu,

Vipi mkuu tukikubaliana kuheshimiana kwenye hilo?
 
.....kwa kweli NSSF wamejipalia mkaa kanza kukumbushia madeni...kisiasa...nafikiri kama wameamua kudai watoe list ya wadaiwa wote sugu wa nssf..na mashirika mengine ya hifadhi za jamii..nahisi itakuwa EPA nyingine!!!
 
Mie siamini kama wamefanikiwa, JF mwendo mdundo. Mwenye ubavu kati ya hao mafisadi si aende pale MAELEZO naye akatoe data zake. Suala la Mbowe na NSSF haliwezi kufanya watanzania wakapoteza dira especially kwenye ufisadi unaofanywa na hao wanaoji-feel kuwa hiyo serikali ni mali yao. Mie sidhani kama pale MAELEZO unatakiwa ulipe ada ili ukutane na Reporters, na hata kama kungekuwa na fee ni fisadi gani ambaye angeshindwa kuilipa ili ajisafishe???? Mie binafsi sina ushahidi kuwa kuna waandishi wa habari baadhi wanakula dau kutoka kwa mafisadi ili wawasafishe, sasa itakuwa sembuse kulipia MAELEZO!! Ila kuna watu hapa JF wanaweza kuthibitisha huo uchafu unaofanywa na akina Balile. Hivyo kama ni kufanikiwa ingekuwa kila fisadi au mtuhumiwa wa ufisadi anakuja before Public na anaeleza anachokijua kuhusu Richmond, EPA na kwingineko na awe tayari kutoa ushirikiano kwa waendesha mashitaka pindi kesi hizo zitakapofunguliwa mahakamani. Wasifikiri kuwa mchezo umeisha, la! bado ngoma mbichi kabisa. Kama JK akishindwa kuwahudumia kwa kuwapeleka mahakamani basi sie walala pu tutakwenda mbele tukiongozwa na TIKILA na MAKANI.
FISADI HAFANIKIWI MPAKA PALE ATAKAPOPATA PIPI TAMU YAKE AMBAYO NI KURUDISHA PESA, FILISIWA NA KUNYEA NDOO KULE SEGEREA.
 
Jamani kila thread na Mjadala wake!huenda la Mbowe limewavutia zaidi wachangiaji
 

Hii ni kali,

Hilo bunge lijalo mbona litawaka moto! Kwa kweli Balile na Rostam hawakujua walichokuwa wanaanzisha hapa. The whole new front ya kukamata mafisadi hadi wakimbie nchi.

Siku chache zijazo huu uchunguzi wa mikopo na matumizi ya NSSF vitapamba headlines za bongo. Namshauri Kikwete aanze kutafuta waziri mwingine wa fedha kwani Mkullo ni time bomb right now!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…