Mafisadi watashinda! - A somber look

JK angeweza kufanya the same thing Mwanawasa did. Kama shida yake ilikua kuingia by any means necessary angeweza kuwa tumia hao mafisadi kisha akawa geuka. Nadhani JK anacho ogopa ni kitamkuta nini baada ya kustaafu kama ata wagusa hawa watu. Maana miaka yake mitano karibia inaisha, akipewa na hiyo mingine nayo itaisha before you know it. I think JK is concerned over his retirement more than anything. Anajua akiwagusa akija kuondoka na akaingia puppet wa hawa majamaa basi shuguli itakua kwake. Sasa this also makes me wonder if JK is as clean as we think. Kama mtu hauja wahi kuiba unaogopa nini hata wakija kuamua kuku shitaki baadae? Otherwise analeta undugu wa kiCCM kuwa hawa wenzangu ni wa chama changu sitaki kuwagusa.

JK is simply are coward. I don't see any excuse for him. Kama wakina Mwanawasa na wa Muthrika wote wameweza kushitaki watu wa chama chao tena watu walio walobby wapate uraisi iweje ashindwe yeye? Bingu wa Mutharika yeye alipoona chama ndiyo tabu aka hama aanzishe cha kwake mwenyewe.

Tatizo hili bango la "Haven of Peace" lina tuumiza sana sisi. Watu hata tufanyiwe ujinga gani ili mradi tuambiwe tuna amani basi oh sisi tuna nafuu ya wengine. Kuna faida gani kama unaepuka gonjwa fulani una kuja kukwa ugonjwa mwingine? Watanzania tuamke. Hii amani tunayo jisifia wenzetu wana zidi kusonga mbele tu.

In conclusion nataka kusema JK & the forth phase gov'ment habe been a big failure & disappointment. We lack courages leaders. Hakuna leader who is ready to challenge the status quo for the better of the people. Ile ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya mwenzetu alikua ana maanisha vingine. I don't see how JK can look back on this term & say he has accomplished anything of significance. na mwakani mta sikia oh kazi tumesha ianza tupeni miaka mitano mingine ili tumalizia, NONSENSE!!! They have been asking for five more years fore the past three elections na hatuoni chochote.

JK YOU ARE SIMPLY A FAILURE & THERE IS NO EXCUSE FOR THE LET DOWN YOU HAVE SHOWN TANZANIANS. IF YOU ARE HALF THE LEADER YOU THINK YOU ARE YOU WILL JUST RETIRE NEXT YEAR(DOUBTFUL).
 
 
 
 
 
kushinda mafisad ni lazima

kwanza mafisad wote ni sampuli za watu wenye roho ngumu za ajabu. na ni kufa ama kupona kwao.

na hebu fikiria rostam, lowasa, chenge waamue waseme hatutaki kabisa kujishughulisha na siasa. na waamue kuwaacha walivyo kina kilango, seleli, mwakyembe, na wengine sampuli hiyo. unafikiri itakuwaje? pesa peke yake walizonazo haziwezi sana kuwaokoa. kinachowaokoa na kitakachoendelea kuwaokoa zaid ni ushawishi wao katka siasa/uongoz wa nchi hii.

wasio mafisad wakikosa wao kama wao wana machache ya kupoteza. lakin mafisad wakiteleza wakapoteza ushawishi wao ndo ntolee hiyo. kuna kushtakiwa na nk. kwa hiyo lazima wang'ang'ane hukohuko

jingine nikuwa akina sie huku mitaani every thing is Ok. jamaa kafanya dili la richmond, no problem. makagoda, ma rada, mikataba ya madini. yote poa. kwani kaja kuvunja chumba changu nilichopanga? hapana. kaniibia kwenye daladala? hapana. sasa je! ana mapene? ndio. sasa je! huyo ndo mtu.
kuna kazi kubwa ajabu ya kuelimishana.
 
Iwe vita endelevu yaani kizazi hata kizazi maana ufisadi haukuanza leo ni matokeo ya misingi ya tangu kale....
 

Ulijuajer kaka? All the best mkuu
 
kwanin wameshinda?
1)hakuna sehemu specific ya kum-position J.K,eidha upande wao,au wa wanyonge

2)vyama pinzani vimeamua kukaa kimya:
-vyama ni mamluki
-wamekosa financial support

3)mafisadi wamewanunua hadi members wa chama chao kiasi cha kufanya maamuzi ya kutisha dhidi ya wapiganaji

4)....................................

5)................................

karibuni kwa mawazo na sababu za ushindi huu
 
Nimerudi kuangalia kama nilisema kitu ambacho sicho; I'm really conflicted of where the nation will end up this year..
 
Mzee Mwanakiji, utabiri wako ulikuwa kweli, kwani hata dalili za awali zilionekana dhahiri kuwa waliojiita na kujipabanua kama wapambanaji walikuwa wanazuga taifa. Hawa walitumia muda wetu mwingi kutuimbisha wimbo wao wa ufisadi kwa maslahi yao kabisa na wala haikuwa kwa taifa.

Leo hii mtu pekee aliyeonesha kwa vitendo kukerwa na ufisadi ndani ya CCM ni Fred Mpendazoe Peke yake, wengine wanalinda na kubembeleza maslahi pamoja na nafasi zao ndani ya CCM.

Dalili zilizo dfhahiri ni kuwa CCM kama taasisi ndiyo yenye matatizo na siyo mtu mmoja mmoja kama wanavyopenda kutuaminisha kila kukicha. Taasisi iliyo imara haiweze kukaa kimya wakati misingi yake inapoguswa. Swala la kiwira, swala Richmond, swala la rada, swala la muungano, yote haya ni katika kutekeleza sera za Chama, kama watekelezaji walitenda tofauti na maelekezo, wanachukuliwa hatua na kama hakuna hatua zozote zilizochukuliwa juu yao ni wazi kuwa walitenda sahihi. hivyo wengine kusema nai ufisadi wakiwa ndani ni kupotea uelekeo.

Sasa wabunge wenye uelewa mpana kama Mwakyembe, Seleli, Ole sendeka, Sita, Kilango Ana, na wengine wengi wanashindwa kuelewa hili? Siamini hivyo, nachoona ni maslahi Binafsi.

Mzee Mwanakijiji, njia nzuri ya kupigana na hii taasisi ya wezi ni kuelimisha watanzania wajue kuwa shida na taabu zao za kimaisha zinatokana na hili genge la wezi. Na siyo kuwa na kundi lililokosa pa kuiba linalopiga kelele ili tulionee huruma.

Utabiri wako ulikuwa kweli na utajidhihirisha zaidi kufikia october 2010.
 
Hakuna binadamu amezaliwa akiwa fisadi,ufisadi ni human manipulation,ufisadi haujengi bali unabomoa taifa.Zipo taasisi, sheria na kanuni za kupambana na ufisadi lakini ndio kwanza ufisadi umeshahimili kwa kasi,umeenea kama kansa.Kushinda ufisadi ni kuteketeza mafisadi na kutaifisha mali zao kama anavyofanya China.Fisadi hatibiki ni kumwangamiza kabla hajaabukiza jamii.Mwanakijiji mafisadi watapata ushindi wa muda lakini sio ushindi wa kudumu.
 
Nani anapambana nao? CCM? ama Wananchi? Ushinda wanaoupata mwaka huu ni wa milele na wala si wa muda mkuu.
 
Siku hizi bongo imezuka EPA mpya, nayo ni safari za nje zisizokwisha kwa viongozi na maofisa wa serikali, wakiongozwa na Muungwana mwenyewe, I mean this EPA is worse kuliko hata EPA

Hii ni kweli kabisa.... unaweza kupiga hesabu ya ofisa mmoja hela anazolipwa kwa safari mwaka mzima .... inatosha kujenga shule hata tano (5) kwenye kijiji au hospital kubwa tu kijijini - JAMANI NCHI INATAFUNWA ISIVYO KAWAIDA - HAKUNA ACCOUNTABILITY - KWANI SASA HIVI NI FROM TOP TO BOTTOM - HAMNA WA KUMWULIZA MTU -
MUNGU IKOMBOE TANZANIA NA WATU WAKE
 
Itafika wakati tutachagua kati ya kufa kwa risasi au kwa njaa,kila jambo lina mwanzo na mwisho nchi hii haikuumbwa kwa ajili ya wachache(hasa watawala na mafisadi)By Murusagamba
 
Nakubaliana nawe kabisa kwamba TATIZO LA UFISADI WA TANZANIA NI CCM, period. ni taasisi hiyo ambayo RA ameitumia kupanda ngazi za kufanya ufisadi nao wakimlinda na kulindana ili kuendeleaa kupalilia ufisadi wao ambao kwao ndo uhai wa chama hicho (CCM).

Binafsi nashangaa mkjj kwa upeo wako unavyotaka kutuaminisha kuwa RA ndio chanzo na tatizo la ufisadi hapa nchini, SI KWELI!! Yeye ni mchumaji katika kampeni ya ufisadi kama wachumaji wengine ila mbinu zake ni zaidi ya mtu kwani anaelewaa ili kuchuma vizuri lazima ushirikianee vema na taasisi inayosimamia masilahi ya wengi kwa maana ya chama chenye serikali. Kwa taarifa yako ili kuuondoa ufisadi au kuupunguza kwa kasi kubwa ni kuiondoa serikali ya CCM madarakani.

Ni Hali mbaya sana kwani mpaka katika utendaji wa umma wenye nafasi zote muhimu taasisi na mashirika ya umma wana uhusiano mwema na CCM tuu na utendaji wao unaaboresha uhalalai wa chama hicho tuu na sio masilahi ya wananchi. Mfano mzuri jaribu kutafiti nafasi za juu za mashirika ya umma na taasisi zake uongozi wapatikanaje na wanamtumikia nani???

Pia imekuwa mbaya zaidi hata watumishi wengi wa umma kwa makusudi ya kuneemesha nafsi zao ni vibaraka wa chama tawala ili waweze kufanya vema ufisadi katika maeneo yao.. Hapa sioni RA akiwa tishio zaidi ya CCM kutumia ufisadi kama uhai wa kuendeleaa kututawala ili kutunyonyaaa...
 
Hakuna shaka kwamba mfumo wa uendeshaji nchi ambao miaka nenda miaka rudi umejikita katika kuimarisha CCM kama ndiyo njia pekee ya mtu kupata mafanikio kiuchumi Tanzania ndio haswaa kiini cha ufisadi Tanzania. Hiki chama kimetengeneza mfumo wa kimafia ambapo uadilifu, uchapaji kazi na uzalendo vimebakia kuwa kauli mbiu tu za kuwazuga mazoba ilhali wajanja wakiwahi siti ndani ya treni la CCM (kama ilivyothibitishwa na payuka ya Sumaye) ili kuendelea kula urojo - hata kuambulia makombo tu - bila soni wala kificho.

Ndio maana ukiwataka wakulu waimarishe mfumo wa mapato halali kama mishahara, kurekebisha kodi na pensheni hawataki kabisa kusikia kitu hicho kwani, kwa mtazamo wao, huko (kwenye kutegemea mshahara) ndiko walikokukimbia na waliobakia huko ni ama wachovu au wavivu wa kufikiri. Kwa bahati mbaya kuna idadi kubwa ya Watanzania imeaminishwa kutegemea mfumo huu wa janjajanja wakitarajia kupata fursa ya kuudandia (one day, yes) na kukogana mara wanapodondokewa na makombo ya kifisadi. Lakini wanasahau kwamba kuendesha uchumi kwa mfumo wa ubabaishaji hauwezi kuwa endelevu. Ndio tunaelekea ukingoni hivyo.
 
Ukienda vitani hujui adui yako ni nani lazima utashindwa tu. Hiki ndicho kinachotokea kwa wale wenye nafasi wanaojiita wapambanaji wa ufisadi. Ufisadi siku zote duniani upo hata mbinguni unawza pia kutokea ufisadi. Ufisadi utafanywa na watu pale tu TAASISI husika katika kusimamia misingi ya haki na usawa itaacha kufanya kazi yake sawaswa. HIKI NDANI YA CCM HAKIPO TENA. Hakuna kikao chochote cha kichama kinachoweza kuukemea ufisadi kwa nguvu zake zote.

Nasema hivi kwa sababu: 1. Kamti ya maadili ya chama ina watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi. 2. Kamati kuu ya chama, wale wenye nguvu za ushawishi wanatuhumiwa kwa ufisadi. 3. Halimashauri kuu inahusisha wote wenye kutuhumiwa kwa ufisadi. 4. Mkutano mkuu unafanya yanayoamuliwa na wakubwa wanaotuhumiwa kwa ufisadi. 5. Bungeni kamati ya chama ikikaa, wabunge wanafyat mkia kama mbwa koko.

Kwa hali hii vita inayopiganwa na wapambanaji wanapigana na nani? Kama ni Rostam hawatashinda, kama ni Lowasa Hawatashinda na Kama ni Mkapa hawatashinda. kwa sababu hawa si wahusika wa ufisadi, hawa ni sehemu tu ya ufisadi.

Tunachotakiwa kufanya wote pamoja na wapambanaji ni kuitia nyufa Tasisi hii ya ufisadi kila kona, ili siku moja isiwe rahisi kwao kuikarabati na mwisho itaanguka tu. Nyufa ni pamoja na wapambanaji wote kutoka CCM, Wananchi kupungu idadi ya wabunge wa CCM, na Raisi kupata ushindi mdogo wa kuiba kura.
 
mkuu nimeingalia makala yako yenye mkato wa tamaa uliopitiliza. katika kusema hayo yaani umewapa ahueni hao manyang'au kwa kiasi kikubwa sana bila ya wewe kujua hilo. mtu anapoonyesha dalili ya kushindwa katika lolote lile, huwa anampa mshindani nguvu mpya ua kuongeza mashambuizi. lakini umeongea kama vile hakuna tena mbadala wa uongozi huu uliopo. unadhani watanzania bado wana mawazo ya chama kushika hatamu? hata wakipangwa mafisadi katika safu za NEC, bado kuna ngumi za wananchi ambao zitaamua ni nani wa kwenda Dodoma kuwawkilisha. Tusiwape mafisadi huu uhuru wa kupumua kwa namna hiyo. Nadhani mnamkumbuka Al Sahaf wakati wa Vita vya Iraq. Yule jamaa aliwatia tumbo joto wamarekani na ulimwengu kwa ujumla kupitia Aljazeera hadi tukajua wamarekani na allies wake wamekwisha! So bado kuna mbadala katika kuona kuwa huu ufisadi unapungua kama si kutokomea KABISA!:angry:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…