Mafisango mpya Msimbazi

Mafisango mpya Msimbazi

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,258
James%2BKotei.jpg


KWA waliokuwa uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam Jumamosi iliyopita wakati Simba ikicheza na Azam, watakuwa wameshuhudia kitu kimoja kikubwa. Uwezo wa Mghana James Kotei kumdhibiti vilivyo mshambuliaji hatari wa Azam, John Bocco “Adebayor” kiasi kwamba nahodha huyo hakuweza kufurukuta. Kotei ambaye ni kiungo, alicheza kama beki wa kati kukosekana kwa mabeki wawili mahiri; Method Mwanjali na Abdi Banda na hivyo Omog akaamua kumpanga Kotei ambaye alifanya kazi iliyowaacha midomo wazi mashabiki wote uwanjani.

Lakini hofu ya mashabiki wa Simba ilikuja pale Kotei alipopigwa kiwiko na Bocco na kuumia wakidhani kwamba asingerejea tena. Omog alimsimamisha kinda Vicent Costa kupasha na mashabiki wa Simba wakaanza kuguna.

Ingawaje kinda huyo hakucheza lakini mmoja wa viongozi wa Simba alisema hakupandishwa kikosi cha wakubwa kwa bahati mbaya. “Costa ni beki mwenye utulivu wa hali ya juu sana, anacheza kwa kujiamini na angecheza mashabiki mngebaki na mshangao,” amesema kiongozi huyo.

Amefichua kwamba tofauti na watu wengine wanavyofikiri, Costa ni beki mwenye uwezo wa hali ya juu na anakaba kiasi kwamba hampi mtu nafasi hata ya kupiga shuti. “Kama angecheza mngeona tofauti yake na mabeki wengine hapa nchini, siku akibahatika kucheza mtaona kazi yake maana mazoezi anafanya vizuri sana,” alisema
 
Ameshafikia kiwango cha Mafisango kweli?

Inasemekana Mafisango alikuwa anawahamasisha sana wenzake awapo uwanjani. Alikuwa mchezaji na kiongozi awapo uwanjani.

Vv
 
Ameshafikia kiwango cha Mafisango kweli?

Inasemekana Mafisango alikuwa anawahamasisha sana wenzake awapo uwanjani. Alikuwa mchezaji na kiongozi awapo uwanjani.

Vv
huyu ni mkimya lakini pia mchapa kazi uwanjani ingawa nahisi ukimya wake unatokana na mbabe aliyenaye shida ya beki ya kati ya simba ni UKIMYA
 
Tafuteni kwanza Ubingwa wa VPL hayo mengine baadaye!

Mnashinda kusifia wachezaji lakini hata hawaisaidii timu kutwaa Ligi.

Mlianza na Mavugo, akawa galasa

Mkaja kwa Kichura, akawa galasa

Sasa mnakuja kwa Kotei....
 
Tafuteni kwanza Ubingwa wa VPL hayo mengine baadaye!

Mnashinda kusifia wachezaji lakini hata hawaisaidii timu kutwaa Ligi.

Mlianza na Mavugo, akawa galasa

Mkaja kwa Kichura, akawa galasa

Sasa mnakuja kwa Kotei....
sawa
 
Ligi ilishaisha wiki 2 zilizopita,hiyo mechi ilikuwa Ndondo Cup ?
 
Maelezo yako sijayaelewa kabisa,HAYAELEWEKI.Yupi ni mafisango mpya hapo?Huyo Vincent Costa au Huyo kotei aliyemkaba vyema boko??Acheni kumfananisha marehemu Patrice mutesa mafisango"R.I.P"Na upumbavu mwingine wowote.Mimi ni timu yanga but Mafisango alifariki akiwa ktk ubora wake.
 
Back
Top Bottom