Mafua na kukohoa vinamsumbua mwanangu

Mafua na kukohoa vinamsumbua mwanangu

shangwe shangwe

Senior Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
108
Reaction score
24
wadau tafadhali naombeni ushauri. Mwanangu anasunbuliwa sana na mafua na kukohoa kwa muda mrefu richa ya dawa mbalimbali nilizo mpatia kutoka hospitali, lakini bado hajapona huu ni mwezi wa 3. Nifanyeje?
 
Pole sana....umejaribu kuwaona wataalam wa magonjwa wa watoto imeshindikana? Isijekua unajinunulia tu dawa na kumpatia mkuu...watoto ni very sensitive hebu fanya hima mkuu...nadhan itakua vyema ukileta feedback ukifanikiwa
 
wadau tafadhali naombeni ushauri. Mwanangu anasunbuliwa sana na mafua na kukohoa kwa muda mrefu richa ya dawa mbalimbali nilizo mpatia kutoka hospitali, lakini bado hajapona huu ni mwezi wa 3. Nifanyeje?

mpime choo kikubwa inawezekana ana minyoo
 
mi sikohoi ila naona kama koo linawaka moto hadi nahis homa
 
Angalia mazingira anayoishi muepushe na kuchezea midoli hasa ile yenye manyoya.
 
Angalia mazingira anayoishi muepushe na kuchezea midoli hasa ile yenye manyoya.

Kuna uwezekano kuna vitu vinavyomsababishia mzio unaomletea mafua na kukohoa. Anaweza kungundua kwa kumfuatilia kwa karibu ! Je anapokohoa au kupata mafua huwa anakuwa katika mazingira gani au hata ni baada ya kuwa amekula kitu gani na unapongundua njia nzuri ni kuviepuka. Mbali ya vitu kama midoli; mablanket yenye manyoanyoa na hata matumizi ya AC au Fan yanawezasababisha tatizo husika! Kikubwa ni kumchunguza na pia kufanya uchunguzi wa kitabibu.
 
Back
Top Bottom