Hili tatizo la mafua na mimi huwa linanisumbua sana. Tofauti na Baba Collin, mimi najua niko allergic na vitu kadhaa, ikiwamo moshi wa namna yoyote ingawa zaidi ni moshi wa sigara, pia perfum na sabuni zenye harufu kali, vumbi, na hata maji ya baridi (ya kuoga!!). Kama alivyosema mdau mwingine hapo juu, mafua huwa yanatibika kwa dawa kwa siku saba, lakini kama hutumii dawa yanakauka kwa wiki moja! Mara nyingi mimi natumia citrizine na flucorday (ingawa kwa siku za karibuni zimekuwa adimu sana). Dawa kama codril, coldaur, n.k. (zenye caffeine) huwa situmii kabisaaaaa, hizi hunifanya niwe kama TEJA!