Mafua yasiyoisha

Mafua yasiyoisha

biee

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2013
Posts
332
Reaction score
116
Ndugu, habari?
Mimi ni kijana (22), tangu nimekua na akili na uwezo wa kujitambua nimekua nikisumbuliwa sana na mafua, yaani sijawahi kustay free from mafua. Je hili ni tatizo gan? Na linaweza likawa linasababishwa na nin? Ushauri wenu ni wa muhimu sana
N.B. hosp. Nimeshakwenda sana lakini bado sijapatiwa suluhisho
 
Pole sana kijana mimi ninahisi wewe una matatizo ya allergy je umeshakwenda kupima hiyo allergy? Kwa ushauri wangu kama utaweza kila siku jaribu kuchukuwa punje moja ya kitunguu Saumu kimenye kisha ukimeze kwa maji fanya hivyo kutwa mara 3 kwa muda wa siku 7 kisha njoo hapa unipe feedback. Ukiwa bado hujapona nitumie barua ya pepe huku nilipo kuna Dawa ya mafuwa inauzwa kwenye maduka ya dawa, dawa kiboko ya kutibu Maradhi ya Mafuwa unitumie Email nitakupa maelezo yake kamili Email yangu hii hapa fewgoodman@hotmail.com
 
Mimi pia nina hili tatizo, hadi dawa situmii tena nimeacha tu! Kila siku nakuwa na mafua asubuhi had saa tano hiv ndio yanakata. Yan mchana unapoingia na mafua yanapotea.

Niliwahi kupatiwa dawa za allergy nazo hazikunisaidia. Napopata vumbi kidogo tu napata mafua makali sana. Ila kama hakuna vumbi nakuwa na mafua kiasi tu na ikifika mchana yanaisha.

Shukran MziziMkavu ntajaribu hiyo tiba ya kitunguu swaumu.
 
Last edited by a moderator:

800px-Italian_garlic_PDO.JPG

Kitunguu saumu mimi huwa ninaikiita kwa jina la kiingereza Natural antibiotic.

Kitunguu Saumu laiti ungelijuwa Faida yake basi usingelikosa kutumia kila siku japo

punje moja kwa siku.

Kitunguu thaum kimekusanya protein 49% mafuta muhimu ya sulphur 25% na kiasi flani cha chumvi, homoni (hormones) zitiazo nguvu za kiume na vinavyoteremsha hedhi.

BAADHI YA MARADHI YANAYOTIBIWA NA KITUNGUU SAUMU:

Kiuasumu:
Saga tembe tano za kitunguu thaum, changanya na asali kikombe kimoja kilichochanganywa na habbasouda na kunywa papo hapo. Kunywa asubuhi na jioni. Paka mafuta ya kitunguu thaum pahala panapouma iwapo ni sumu ya nyoka au paka nje ya tumbo iwapo umekunywa sumu.

Kusafisha tumbo:
Kabla ya kula chakula, meza tembe za kitunguu thaum na baadae kunywa maji ya shimari yaliyochanganywa na asali kwa muda wa wiki moja.

Kiyeyusha mafuta (Cholestrol):
Unapokula chakula kila siku, weka katika kachumbari kiasi cha tembe 2 vilivyosagwa ule pamoja na kachumbari.

Kiongeza mkojo chenye kusafisha njia za mkojo:
Chemsha vizuri hairi, na baada ya kupoa tia tembe 3 za kitunguu thaum zilizosagwa. Kunywa kinywaji hicho kila siku kabla ya kula na kunywa juisi ya limau/ndimu.

Kuharisha damu (Dysentery):

Chukua tembe ya kitunguu thaum uikatekate na uile; fanya hivyo kwa muda wa wiki moja na bora zaidi ukinywa na mafuta ya zaituni kijiko kimoja.

Gesi na Indegestion:
Kunywa juisi ya pea iliyochanganywa na tembe 3 za kitunguu thaum kabla ya kulala kila siku.

Kutibu Typhoid:
Kata tembe 5 za kitunguu thaum, changanya ndani ya maziwa ya moto yaliyochanganywa na asali kunywa kabla ya kulala. Pia paka uti wa mgongo mafuta ya kitunguu thaum yaliyochanganywa na mafuta ya zeti, na asubuhi vuta moshi wa kitunguu thaum kwa muda wa dakika 5.

Kidonda kilichooza:
Ponda kitunguu thaum mpaka iwe laini kama marhamu halafu jifunge nacho kwa kutumia bendeji, japo kitawasha lakini kitazuia ugonjwa wa gangrene ambao unaweza ukapelekesha kukatwa kiungo. Vilevile unaweza kusafisha kidonda kwa kuchanganya kitunguu thaum kilichosagwa kikatiwa maji vuguvugu (warm water) na kikasafishwa kidonda.

Mishipa:
Kata tembe za kitunguu thaum na umeza kwa maziwa ya moto (sio moto sana) yenye matone ya ambari kabla ya kulala kila siku, dawa hii huipa mishipa nguvu.

Homa ya mafua (Influenza):
Kunywa juisi ya machungwa na juisi ya limau zilizochanganywa na tembe 7 za kitunguu thaum kunywa juisi hiyo kabla ya kulala. Vuta moshi wa kitnguu thaum.

Mafua:
Meza tembe za kitunguu thaum baada ya chakula pamoja na juisi ya kitunguu thaum iliyochanganywa na juisi ya limau pamoja na kuvuta moshi wa kitunguu thaum.

Saratani (Cancer):
Katika kitunguu thaum kuna kiini kinachozuia saratani, kwa kila mgonjwa wa saratani anashauriwa ale kwa wingi kitunguu thaum na karoti (carrot).

Kifua kikuu (cha mapafu):
Kila asubuhi kabla ya kula chakula meza tembe 3 za kitunguu thaum, saga ule pamoja na mkate na jioni vuta moshi wake.

Kipindupindu (cholera):
Ili kujikinga na maradhi hayo wakati kikienea, kula kijiko kimoja cha kitunguu thaum kilichosagwa na kukorogewa katika asali baada ya kila chakula.

Kutoa minyoo:
Ponda tembe 3 za kitunguu thaum, tia ndnai ya maziwa na kunywa (bila kutia sukari) jioni kabla ya kulala na asubuhi kunywa mafuta ya mbono.

Upele:
Chukua tembe 5 za vitunguu thaum uvisage na uvikoroge katika shahamu na paka pale penye upele kuazia jioni mpaka asubuhi na ukoshe kwa maji ya moto tumia kwa muda wa wiki moja.

Mbaa kichwani:
Ponda uzuri vitunguu thaum 3 na uvikoroge katika siki ya tofaha (Apple vinegar) katika chupa ya bilauri (sio plastiki) na uache juani kwa muda wa wili moja. Baada ya hapo jipake kichwani pamoja na kusugua kwa muda wa wili 1 na baada ya wiki jipake mafuta ya zeituni.

Nguvu za kiume:
Saga kitunguu thaum kitie ndani ya mafuta ya zeti na weka katika moto mdogo mdogo mpaka iwe rangi ya manjano na tia katika chupa na wakati wa haja jipake katika dhakari na osha baada ya saa moja.

Kujenga misuli na kutia nguvu:
Kila siku kabla ya kula kunywa kikombe kikubwa cha maziwa ya ngamia yaliyotiwa tembe 2 za kitunguu thaum iliyosagwa. Kunywa kwa muda wa mwezi mmoja mfululizo.

Kinga ya taunni na ukimwi:

Chanzo.MziziMkavu
 
Nashukuru sana jaman. Nitaanza hyo dozi mapema leo. Nitawashauri na ndugu zangu wafanye hivo maana katk familia yetu tuko watatu wenye hlo tatizo yaani mim, baba na mdogo angu.
Thank you JF..
 
Wana jf, nashukuru wote mlionipa ushauri wakuondokana na mafua.
Doz nilianza kama nilivyoelekezwa lakini tofauti nikwamba mimi ninatafuna hivyo vitungu.
Je kuna tatizo hapo??
Pili, siku ya kwanza nilivyotumia hii dawa mambo yalikwenda vibaya sana, kwanza nilichoka sana, nilijisikia hovyo sana, kichefu chefu sio kichefu yaani hali ilikua tafran ad nikaogopa, maana nilisweat vibaya sana. Lakini gud thing baadae nikawa okey.
Tatizo linakuja kwamba mafua ndo yamezidi yaani chafya za kutosha kama usiku wa leo ndo hali imekua mbaya zaidi lakin sa hivi navoandika niko na mafua ya kawaida.
Je hivyo ndivyo inavyotakiwa kuwa au ni dawa haijanipenda??
 
Kitunguu Saumu unakula siku ya kwanza itakutokea hali ilivyo kutokea baadae ukiendelea utakuwa kama kawaida matatizo yako yatakwisha tumia kama nilivyokueleza unaweza pia kutafuna sio mbaya kitunguu saumu.
 
Mkuu@mzizi mkavu...ninaleta feedbak...aise mafua bado yako palepale...yan ata sijui tena
 
Mimi pia nina hili tatizo, hadi dawa situmii tena nimeacha tu! Kila siku nakuwa na mafua asubuhi had saa tano hiv ndio yanakata. Yan mchana unapoingia na mafua yanapotea.

Niliwahi kupatiwa dawa za allergy nazo hazikunisaidia. Napopata vumbi kidogo tu napata mafua makali sana. Ila kama hakuna vumbi nakuwa na mafua kiasi tu na ikifika mchana yanaisha.

Shukran MziziMkavu ntajaribu hiyo tiba ya kitunguu swaumu.

Tatizo watu wanakunywa dawa siku chache alafu wanaacha. Kama unaallergy elewa ni ugonjwa wa kudumu. Kunywa antihistamine kama cetrizine kidonge kimoja wakati wa usiku tu,...kila siku maisha yako yote. yaani utasahau hilo tatizo. pia kwepa vumbi, sigara, perfume na mengineyo yanayokuduru.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu@mzizi mkavu...ninaleta feedbak...aise mafua bado yako palepale...yan ata sijui tena

Kama unaallergy elewa ni
ugonjwa wa kudumu. Kunywa antihistamine; kama CETRIZINE 10mg Nocte, (kidonge
kimoja wakati wa usiku tu),...kila siku
maisha yako yote. yaani utasahau hilo
tatizo. pia kwepa vumbi, sigara, perfume
na mengineyo yanayokuduru.
 
Dr mimi sisikii harufu nlikua napata mafua mara kwa mara mwaka jana nlipata ambayo yalidumu miezi miwili toka yalivopona mpaka leo si smell. Nisaidie
 
Back
Top Bottom