Jamani doctors poleni na majukumu. Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 27, kwa mda wa mwezi mmoja nimekuwa nikisumbuliwa na mafua hasa nyakati za usiku ninapolala na asubuhi ninapoamka, nimejaribu kutumia dawa lakini hali ni ileile. Naomba kupata ushauri wa matibabu juu ya tatizo hili maana napata sana shida!