Mafukara na dhana potofu ya Freemason na Wapigaji

Mafukara na dhana potofu ya Freemason na Wapigaji

Zillion

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2017
Posts
1,378
Reaction score
1,866
Wakuu asalaam,

Ni muda mrefu nimetafakari uwezo kufikiri na upotoshaji wa wanasiasa kwa jamii ya Watanzania hasa masikini.

Kwanza kuna dhana ya masikini kuwachukia waliofanikiwa. Jambo hili ni hatari kwa ustawi wa jamii na linafanyika hadharani.

Mtu fukara akipambana na kufanikiwa ataitwa freemason, mchawi au mpigaji. Dhana hii ilianza taratibu na sasa imeota mizizi miongoni mwa jamii masikini.

Pale mtu anayetoka familia kawaida akipambana na kijikwamua kiuchumi jamii yake badala ya kumpongeza nakujifunza kutoka kwake wengi wao wanamtenga na kumchukia.

Yani masikini anatafuta sababu ya kuhalalisha umasikini wake (kwa uzembe wa kutojituma) kwa kuharamisha juhudi za mwingine aliyefanikiwa kwa kumwita freemason, mpigaji n.k Tabia ya hovyo sana hii.

Mwendazake alipoingia madarakani akawaongezea mafukara sababu nyingine ya kuwachukia waliofanikiwa na kuukumbatia umasikini wao kwa kuwaaminisha kwamba watu wote waliofanikiwa ni wapigaji na mafisadi
Alienda mbali zaidi na kutamka kwamba anataka matajiri waishi kama mashetani na kujiita rais wa wanyonge, kwa maana nyingine alipendelea watu wawemasikini kwasababu ni rahisi kuwatawala.

Masikini wengi walipokea na kuanza kucheza ngoma ya .mwendazake( kwamba wanasiasa wakifanikiwa ni sawa lakini masikini akifanikiwa ni mpigaji). Huu ni ujinga uliopitiliza

Jamii inapaswa kubadilika na kujifunza na kwa waliofanikiwa na si kuwatenga, kuwatukana.

Kufanya hivyo hakuwasaidii bali kunawapumbaza na kuwafanya wajione wao ni wema kwa na wenye kipato cha uhakika ni wadhambi.
Hali hii inaongeza umasikini na umasikini ni mtaji mkubwa kwa wanasiasa wachafu hasa CCM.
 
Siku hizi anayefanikiwa ameongezewa jina lingine,anaweza kuitwa shoga hata kama hahusiki na mambo hayo.

[emoji3][emoji3]
Hii ni agenda mahsusi ya kuwasahaulisha watanzania madai ya msingi kama katiba mpya na kujadili ufisadi wa viongozi wa ccm mfano ununuzi wa mabehewa ulivyojaa ufisadi

Kila wakati ccm wakiona wametaitishwa huwa wanatafuta agenda ya kuwatoa watu kwenye mstari.
 
Back
Top Bottom