Mafundi magari acheni ushamba, kuweni updated

Youtube imenisaidia na inasaidia sana, imenifanya pia niwe mpishi mzuri.

Naangalia kitu kipya kisha nafanya mambo.
 
Wanachojua wao ni kuvaa nguo chafu. Sijui nani kawadanganya ulimwengu wa sasa kuwa mchafu eneo lako la kazi.
 
Mimi naamini katika kitu wanaita Do it yourself, ki baby walker changu nimeamua kuwa fundi mwenyewe, toka huu mwaka umeanza shughuli ndogo namaliza mwenyewe, nimeanza kununua spana zangu so soon nitakuwa na full tool box, pia procedure ndogo ndogo kama kumwaga oil, kubadili breakpads, kusafisha sensors, na vingine nafanya mwenyewe, nimeagiza OBDII diagnosis tool yangu mwenyewe soon itafika, nafanya same kwenye pikipiki yangu, asante kwa Youtube tutafika, as long as najua maduka ya spea yaliko hatuna haja kuja kipigwa sana kiswahili huko garage kwenu, Mungu atusaidie.
 
Mkuu umetisha, gereji ya nyumbani muhimu sana, ukipata vitendea kazi, weekend unafanya mambo madogo madogo mwenyewe... hata wenzetu naona wengi wana gereji nyumbani...
 
Wanaoitumia youtube kiukweli ukweli wako mbali sana kwny field zao(Mechanics,finance,arts,tech etc).

Mimi ni shuhuda wa hilo.
 

OBD II yako ilifika? Je ilifanya kazi?
 
Mtoa maada upo sahihi. In 20 years time tutakuwa tunaimba wimbo mmoja kuhusu gari za japan kuwa na sensor nyingi kama za ulaya.
 
Wakiona gari hawaiwezi kuitengeneza wanakwambia usinunue haitengenezeki itakuzeesha mapema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…