Mafundi simu wa upande wa hardware naomba tukutane hapa

Naombeni msaada jamani. Simu tangu Huawei Mate 7 imepoteza uwezo wa kushika 4G na 3G. Inashika EDGE peke take na wakati mwingine inabaki kama simu ya kitochi tu. Nifanue mini iweze kushika tena?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba kufahamu bei ya sim card holder. Nahitaji kufanya replacement maana kuna jino moja limeng'oka kati ya matatu, hali inayofanya laini kushindwa kusoma au inaweza kusoma kwa muda mchache ila haipandishi data.
 
Mwenye 6s plus yenye reactivation lock (icloud lock) au labda ina matatzo mengne lakin kioo na body viko sawa. Anicheck inbox kwa Biashara. Nichek 0763976109

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwema ndugu??

Aise Nina Samsung Grand Prime Plus inatatizo la touch kujiminya pindi tu nikiminya button ya kutoa lock hivyo inafanya iwe ngumu kweli kutumia. Naombeni ushauri maana sielewi Sasa nimejaribu kufuta screen vizuri ila ipo vile vile.
 
Mpelekee fundi akubadilishie tachi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wakuu habari zenu, nina tecno Y6 nilitaka kufanya reset kwa kutumia Power button na voice key, baada ya kuboot ikaandika NO COMMAND, ikawa inaishia hivyo hivyo nikajaribu kuwasha bado ikagoma nikaamua kutoa simu. saiz ndio imegoma kuwaka kabisa hata nikichomeka chaji haioneshi kuingiza. msaada hapa nifanyaje? ili niiflash maana inagoma kusoma info.
 
Model ya simu yako ni ipi? Na una kumbukumbu kuwa tatzo lilianza vp?

Sent using Jamii Forums mobile app

Model ni HUAWEI MT7 - TL10. Ilianza tatizo hilo mwezi Disemba nikiwa Zanzibar. Mwanzoni nilidhani ni tatizo la network kule Zenji. Niliporudi Dar, mambo yakawa yaleyale hadi leo.

Nimefanya factory restore, bado haisomeki.
 
Naomba kufahamu bei ya sim card holder. Nahitaji kufanya replacement maana kuna jino moja limeng'oka kati ya matatu, hali inayofanya laini kushindwa kusoma au inaweza kusoma kwa muda mchache ila haipandishi data.
Nenda kwa fundi mtaelewana
 
Umeipeleka kwa fundi wa software?
 
Chakula yangu hiyo ila nadhani shida itakuwa distance kati yetu.
 
Miracle box na Gsm alladin inaleta wrong password code. msaada wa kufix
Mfano.
Nikienda Kwenye tab ya Rda kwenye Rd unlock. nikichomeka simu inaleta wrong password. msaada tafadhali
hyo ni kwel nishawahi kuiona lakin kama password hazina umuhimu sana basi wewe format tu mambo yaishe
maana hapo unaweza pata code hata kumi lakin zote ni wrong

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…