Habar wadah uzi huu ni kwa wajuzi na mafundi wa ujenzi wa nyumba,
Mimi nmefanikiwa kujenga kabanda kangu ka vyumba SITA natamani kabanda kangu haka nikaezeke kwa VIGAE naomba kujua kwa vyumba sita ambapo vitatu ni master na vitatu vya kawaida je ni vighae KIASI GANI NITAHITAJI KUNUNUA?JE BEI YAKE ITAKUWAJE?
NISAIDIENI KAMA KUNA ANAE UZA VIGAE TUNAWEZA FANYA BIASHARA ENDAO NTAJULISHWA MAPEMA
ILI NINIPANGE.
Sent using
Jamii Forums mobile app
...................Mkuu Sifi leo,nianze kwa kukupa pongezi kwa kuweza kujenga tena kufikia hatua hiyo kubwa ya kupaua..............................................pili,..................usiite nyumba yako kibanda.......................hapana maana umeweka muda wako na pesa zako clayhivyo naamini siyo kibanda ni nyumba hiyo.
....................turejee kwenye mada,................vigae ni moja wapo ya vifaa ya kupaua nyumba yaani roofing building materials na kwa taarifa yako vipo vigae vya aina nyingi na hutofautishwa kutokana na malighafi inayotumika kuvitengeneza mfano vigae vya udongo wa mfinyanzi(clay tiles),vigae vya saruji na mchanga(sand roofing tiles),vigae vya vinavyotokana na mbao kam shingles,vigae vinayotokana na chuma au mabati ambavyo ni vingi sana siku hizi na hutokea south africa,new zealand na china.
Kila kigae kina faida au changamoto yake.Mfano kigae cha mchanganyiko wa mchanga na saruji huwa vina uzito kulingana na vya chuma na hivyo kuhitaji mbaoa pamoja na uimara wa tofali.Ilhali vigae vya mbao vina uwezo wa kuezeka nyumba ya mviringo na paa lake huwonekana maridadi sana ila ni gharama kubwa kulinganisha na vigae vingine.
Dhana nzima la uezekaji wa mapaa pia hutegemea maeneo halisi ya ujenzi kwani maeneo has aya pwani kuna chnagamoto kubwa ya kutu,wakati sehemu za bara kama mbeya na arusha changamoto kubwa huwa ni namna ya kuzuiya joto libaki nadani ya nyumba tofauti na pwani ambapo joto hutakiwa kutoka.
Sambambana maelezo yangu,ukumbuke kuwa kazi au lengo la kuwa na paa ni pamoja na kujikinga na mvua,jua,joto,baridi na usalama kwa ujumla pamoja na umaridadi wa jengo husika.Nitafananisha paa la nyumbana nywelw za akina dada zetu kwani kuna kuchana,kusuka na hata kipara(flat roof). Mtindo upi wa kutumia ni chagua la mtu mwenyewe,ila swala la style na fashion pia lazima lizingatiwe pamoja na hali ya uchumi kwani kufuga nywele pia kuna maliza sabuni,wakati pia kunyoa kipara ni mtindo wa kisasa,usisahau kuwa lazima uzingatie maadili aya kazi kama ni mwajiriwa,ndo maana hakuna polisi mwenye rasta.
Baada ya maelezo yangu najua utaweza kuwa na chaguo la kigae unachokata ili niweze kukusaidia basi ningeomba uweke ramani ya nyumba uliyojenga pamoja na mwonekano wa paa unalotegemea ili niweze kukujuza gharama halisi na hata mmbadala wake endapo kama utahitaji kuwa nao.
natumaini utafuata ushauri wangu na usisite kuwasiliana nami kwa ushauri zaidi,
Wasalaam,
Mwenzetu