Kwanza lazima ujenge tabia ya kulifahamu gari lako. Hii itakusaidia kuweza kupata angalau mwangaza kidogo wa nini hakiko sawa wakati unaliendesha. Hii itakusaidia hata unapokwenda kwa fundi, unamuelezea sehemu unayohisi ni tatizo badala ya kugusa kila kona.
Pili usiache gari lako kwa fundi wakati linatengenezwa. Mafundi wetu wengi hawajali saana mali za wengine. Sinama kila process, huku ukiuliza maswali, hii itakusaidia kujua kama fundi anajua kazi yake. Na pia itakusadia siku likitokeza tatizo kama hilo na uko sehemu tofauti au fundi mwingine, utakua unajua nini hasa kinatakiwa kufanya.
Tafuta maintenance manual ya gari lako, au ingia kwenye forums za gari husika, au forums kama hizi. Kuna watu wana uzoefu saana wa magari, na unaweza pata mwenye uzoefu wa gari kama lako, hivyo ukapata ushauri wa nini hasa kinatakiwa kufanyika.
Pia jenga mazoea ya kuwa na fundi mmoja. Sio kuhama hama. Hii itasababisha ujenge uaminifu kwa huyo fundi kiasi kwamba ataweza kukushauri vizuri nini cha kufanya.
Na mwisho, jaribu kufanya repairs ndogo ndogo mwenyewe. It takes time and passion, ila ukiamua utaweza. Kuna kila kitu on the internet. Jaribu kutafuta utajifunza. Hii itasaidia kuepuka mafundi wababaishaji.
Mimi sio fundi, ila angalia collection yangu ya tools hapo chini.
View attachment 910268