Kilongwe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2008
- 423
- 116
Lengo la teknolojia ni kurahisisha na kuboresha maisha ya jamii. Hivyo AfroIT tukiwa kama wana jamii tumeanza kuandaa mafundisho ya kutengeneza tovuti kwa kutumia joomla.
Katika mafundisho hayo,mkufunzi Mkata Nyoni atatumia na kugawana uzoefu wake kwenye hii nyanja ya utengenezaji wa tovuti kwenye kipengele cha joomla ambapo hadi mwisho wa safari utaweza kuwa na tovuti nzuri na kuvutia.
Joomla Sehemu ya Kwanza - nenda Hapa
Walengwa wa mafundisho haya ni jamii nziima,ila ili kuhakikisha tunaenda sawia ni muhimu uwe na msingi ufuatao
- Ufahamu wa kompyuta kwa uchache wake
-Ufahamu wa HTML,PHP, na CSS kwa uchache wake(Kama hujui kabisa unaweza kusikila mafuundisho kwani mafundisho yamezingatia sana mlengo wa design na sio development)
-Ufahamu wa kucheza na picha(uhariri),Photosshop inashauriwa.
-Moyo na nia ya kupata ujuzi na kujua mambo mengi
Kozi hii ni ndefu kidogo ambapo itatuchukua mwezi mmoja hadi miwili huku tukitoa mafundisho mawili kwa wiki.
Tutachukua mtindo wa NUNU(Nini Unataka Ndio Unapata),hapa tunamaanisha,hadi mwisho wa safari basi tutaweza kuwa na tovuti bora kabisa.
Kama tulivyojiwekea malengo,baada ya kukamilisha mafundisho,tutaandaa CD na kuzigawa BURE mavyuoni na mashuleni ili kukuza hari na mapenzi ya ICT.
Hivyo kama unaona unaweza kuchangia kwa kusambaza,kuwezesha uchapaji wa CD nyingi zaidi nk basi tuandikie kwenda webmaster@afroit.com .
AfroIT Group