Mafungu Mafungu Preseason, Simba wawe makini!

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2011
Posts
19,675
Reaction score
33,583
Wakuu,

Timu yetu msimu huu kuna kila dalili tumekuwa serious zaidi kwenye usajili. Lakini angalizo muhimu ambalo limekuwa donda sugu ni kocha kupata wachezaji kwa mafungu na kumfanya ashindwe kuendesha program kikamilifu.

Uongozi wa Simba wajitahidi msimu huu kuhakikisha full package ya wachezaji wanawahi program ya mwalimu ili tusilaumiane.

Tumewasifu kwenye usajili mjitahidi wachezaji waungane haraka na kupunguza mafungu yanayompa tabu kocha.

Otherwise tunakwenda vizuri [emoji1666]
 
REJEA Uzi Huu na utafakari.



Bado nazidi kuona makosa makubwa kwenye usajili wa Simba. Kwa mwendo huu mashabiki jiandaeni maumivu tena na tena 2023-24

Habari ndugu ZANGU.
Mimi ni mdau WA soka.
Na mpenzi na mdau wa Simba.

Nimekuwa nikifuatilia usajili HASA WA wachezaji wa KIGENI ndani ya simba.

NIMEWEZA KUYAONA MAKOSA YAFUATAYO KIUFUNDI.

1. KOSA kubwa la Kwanza ni KUMUACHA Golikipa Beno kakolanya., Hivyo wanalazimika KUSAJILI Golikipa wa kigeni. Baada ya Manura KUUMIA. (Santos)
Hivyo kujinyima WiGo WA wachezaji wa ndani.

2. KOSA la pili Kukosa beki MBADALA WA KIGENI WA Che Malone na Inonga Incase Wana Kadi au WAKIUMIA.

Na hapohapo wamekosea MBADALA WA Mohamed Hussen.
YAHAYA mbegu ameng'ang'ania SINGIDA akiwa na GADIEL Michael ALIYE ondoka.

3 . KOSA KUBWA KABISA KABISA NI KUKOSA BACKBONE YA TIMU/ UTI WA MGONGO WA TIMU KIUNGO MKABAJI CDM 6
Tangu AMEONDOKA LWANGA , mkude, Nyoni na sawadogo hakuna MBADALA wao.

Japo Kunatetesi na Unafuu nasikia NGOMA amesaini Simba hii itakuwa nafuu Ila NGOMA ni 8.

4. KOSA LINGINE ni kujaza idadi kubwa ya Mawinga
I. Saido.
Ii. Onana.
Iii. kibu Denis
Iv. Sakho, Banda
V. Chama.
Vi Aubin Kramo.

5. KOSA LINGINE usajili WA mshambuliaji mmoja tu no 9. Jean Baleke.
Boko AMEISHA.
Ile Simba ya Makombe ilikuwa Kagere, Boko na mugalu saizi ni Baleke pekee

6 . Kosa LINGINE kubwa zaidi. MSIMU ILIYOPITA Simba ilikuwa na Mabeki WA kati. 5, ONYANGO, Inonga, KENEDY, Ottara na Sometimes Nyoni.
Leo Simba Ina Mabeki 3 WA kati hata kugawana mazoezini ni shida.

MAKOSA NI MENGI MNO MUDA NI MCHACHE.
SIMBA NA ROBERTINHO REKEBISHENI HAPA.
USHAURI WA BURE
 
Timu zote kubwa huanza pre season kwa mafungu. Mkianza nyote ujue timu ndogo. Angalia EPL timu kubwa na walioripoti hadi leo
 
Bado ninahofu na preseason kuwa na mafanikio. Wachezaji wageni wengi hawajajiunga na wenzao, muda wa kujenga combination ni mdogo wakati tumesajili wachezaji wengi wageni.

Viongozi wamalize mambo ya usajili wachezaji wapate muda wa maandalizi. Tubakia na siku 30 ambazo hatupaswi kupoteza another week.
 
Timu zote kubwa huanza pre season kwa mafungu. Mkianza nyote ujue timu ndogo. Angalia EPL timu kubwa na walioripoti hadi leo
Kama kikosi kikiwa na mabadiliko madogo sawa lakini kwa Simba tumejenga upya maeneo mengi. Msimu uliopita Yanga hawakuhitaji preseason ndefu sababu walifanya mabadiliko madogo.
 
MTAZAMO, kwa namna yeyote ile Simba haiwezi kukupa matokeo mazuri msimu huu kwa sababu namba zinakataa.
Inawezekana kama kocha akipewa timu kamili mapema. Within 7days bila kuzidi timu iwe imekamilika otherwise tutaanza struggling mapema na hiyo ndio inatuumiza. Huwa hatumalizi vibaya bali mara nyingi tunaanza vibaya.
 
Kama kikosi kikiwa na mabadiliko madogo sawa lakini kwa Simba tumejenga upya maeneo mengi. Msimu uliopita Yanga hawakuhitaji preseason ndefu sababu walifanya mabadiliko madogo.
Wapya watakaoingia kikosi cha kwanza hawatazidi 4.
 
Simba tuna shida kwenye management tena shida kubwa sana,na it looks like hatuna watu wa mpira nnaposema watu wa mpira,watu wa mpira wananielewa tuna wanasiasa tu .tusitarijie makubwa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…