Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Mara nyingi sana waswahili huwa wanazungumzia mtu kupata elimu ya dini lakini kiuhalisia huwa wanamaanisha ni mafunzo/maelekezo ya dini ya mtu husika.
Elimu ya dini au kwa Kingereza "religious education/studies" ni ile elimu ya darasani mtu anayosemea kuhusu dini husika au dini mbalimbali akiwa na mawazo huru, akifanya uchambuzi wa vitabu na kupitia vyanzo mbalimbali vya dini yenyewe/zenyewe na vyanzo vingine huru.
Katika Religious education/studies Mkristo anaweza kusoma kuhusu ukristo, uislamu, uhindu, ubudha, dini za kale zilizopotea n.k Muislamu pia hivyo hivyo anaweza kusoma kuhusu Uislamu, Ukristo, uhindu na dini nyingine.
Kwa upande mwingine kama mtu yuko katika kujifunza/kuelewa dini yako kwa kutumia kitabu/vitabu na vyanzo vingine vya dini yake tu kwa minajali ya kueilewa , kuwa na imani zaidi na kuishi imani na maadili ya dini husika hiyo sio elimu ya dini tena bali ni mafunzo/maelekezo ya dini.