Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
1. Katiba imara na taasisi imara peke yake ndio zinaweza kuwa ukuta na vizingiti kati ya demokrasia na uimla. Sio nia njema, mazoea, mila wala tamaduni za kisiasa zinazoweza kuhakikisha uhuru stahiki wa wananchi.
2. Sio wafanyabiashara tu ambao ni wasaka fursa bali asilimia 90 ya binadamu wote ni wasaka fursa wanaoweza kubadilika kadri hali inavyobadila ili tu kuzifika fursa. Wawe ni maprofesa, wanazuoni, wanasiasa, watumishi wa umma au viongozi wa dini n.k wote ni wasaka fursa tu.
3. Ukatili wa binadamu hautokani na utaifa wake, rangi yake au kitu kingine chochote. Binadamu yoyote anahitaji msukumo na hofu ya kutosha ili kutenda ukatili.
4. Maendeleo ya watu ni bora zaidi kuliko yale ya vitu ila yote hayana budi kwenda sambamba.
5. Uhuru wa binadamu ndio kitu cha thamani kuliko kitu kingine chochote. Ila Binadamu waliokata tamaa "wanyonge" wanaweza kuridhika na "trade-off" kati ya uhuru na maendeleo.